Mabasi yaendayo haraka yaanza kazi Rasmi LAKINI... Mabasi 50 yanaanza kazi Ijumaa Aprili 22, 2016

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,949
4,638
Mabasi 50 yanaanza kazi rasmi Ijumaa April 22,2016.Ratiba ndefu imetangazwa. Lakini Lakini Kiwango Cha Nauli Hakijawekwa Wazi. Kulikoni? Zisije Kuletwa Zile Za Awali Maana Rais Alishazikataa Juzi Wakati Anazindua Fly Over Pale Tazara.
Ratiba Hii Hapa Chini:

MABASI YATAANZA SAFARI SAA KUMI NA MBILI KASORO ROBO ASUBUHI IJUMAA APRIL 22,2016, KUTOKEA DEPOT YA JANGWANI KWA MPANGILIO UFUATAO.

1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.

2. RUTI YA KIMARA - KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO - KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.

5. RUTI YA UBUNGO - MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

6. RUTI YA MOROCCO - KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)

3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

JUMLA NI MABASI HAMSINI (50)
 
Kwa test drive ni sawa, ila kiuhalisia hayo mabasi ni machache sana!
Wanahitaji angalau mabasi mia 300 kufanya usafiri uwe comfortable na watu wasigombanie huo usafiri
Sina hakika mabasi haya kama yatatosha... abiria tuko weng mno.
Ni kweli hayatoshi.
Abiria takribani million 1.5 watatumia haya mabasi na italeta shida kubwa sana kama idadi ya mabasi haitakuwa ya kutosha.
Mabasi 50 hayatoshi kabisaaa.
 
Jamani hebu tuweke akiba ya maneno kwanza, tuone mpango wao utakuwaje.
Ni mapema sana kusema kuwa hayatoshi.
Na kama wanasema kuwa sehemu ya hayo mabasi makubwa yanaweza kupakia mpaka abiria 140 kwa wakati. Hapo ni vyema tukajua bus litachukua muda gani toka kimara-k'koo au kimara-kivukoni.
Yakishajulikana hayo tunaweza kutoa maoni yetu hapo.
 
Mkuu kwa muda huo wa kuanza kazi wanatuambiaje tunaopeleka uji muhimbili kwa wagonjwa wakati saa moja wodi zinafungwa na mimi nimeanza safari saa 12 kamili ambapo wodi zinafunguliwa!?
 
Ni kweli hayatoshi.
Abiria takribani million 1.5 watatumia haya mabasi na italeta shida kubwa sana kama idadi ya mabasi haitakuwa ya kutosha.
Mabasi 50 hayatoshi kabisaaa.
Hayo ni majaribio. Mabasi yapo zaidi ya 50.
 
Jamani hebu tuweke akiba ya maneno kwanza, tuone mpango wao utakuwaje.
Ni mapema sana kusema kuwa hayatoshi.
Na kama wanasema kuwa sehemu ya hayo mabasi makubwa yanaweza kupakia mpaka abiria 140 kwa wakati. Hapo ni vyema tukajua bus litachukua muda gani toka kimara-k'koo au kimara-kivukoni.
Yakishajulikana hayo tunaweza kutoa maoni yetu hapo.
Vizuri japo hata yangepakia watu200 hayo mabasi machache
 
Wameamua kuleta machache baada ya bei kubwa waliyokuwa wamependekeza awali kukataliwa, wanaogopa kufanya biashara katika mstari wa hasara ndiyo maana mnaona basi zipo chache na gharama ya maintainance ipo juu sana kwa hizi bus...
 
Baada ya kukamilika kwa mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka, taarifa zilizopo ni kuwa kuanzia leo Ijumaa ya April 22 2016 mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka ndio utaanza kufanya kazi rasmi na ruti zake zimeorodheshwa hapo chini mtu wangu.

1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.

2. RUTI YA KIMARA – KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO – KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.

5.RUTI YA UBUNGO – MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

6. RUTI YA MOROCCO – KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

MUDA WA KUONDOKA KITUONI SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)

3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

CHANZO: issamichuzi
36deb491eadb28f4fd87875ed3abe6bc.jpg
 
Japo mradi umechelewa sana kiasi imefikia kuwa sio jambo jipya tena sasa unapoanza rasmi, ila tunapongeza juhudi zilizofanyika mpaka kukamilika kwake,
Ni jambo jema tunashukuru....
Hatutarajii kupatikana figisu figisu zingine, bali matarajio yetu mradi ujitanue zaidi ktk maeneo yaliyobaki kufikiwa kama mbagala na vitongoji vyake...
 
Sisi wakazi Wa mkwajuni hayatuhusu, hatuna ruti hata Moja ya Posta. ukitaka kwenda Posta panda bus hadi magomeni au hadi manyànya kisha ndo upande LA Posta. tulitegemea haya ya mwendo kazi yangepitia hapa mkwajuni hadi kivukoni lakini wapi.
 
Back
Top Bottom