Mabasi yaendao kasi na huu mradi wa treni hapa jijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabasi yaendao kasi na huu mradi wa treni hapa jijini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kwamtoro, Oct 31, 2012.

 1. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  Upi ni sululisho sahihi wa kupunguza kero na kutokomeza kabisa usumbufu wa usafiri toka katikati ya jiji la Dar es salaam.

  Je miundombinu ya reli ifanikishwe kuwa na reli ya kuelekea mbagala na nyingine Tegeta toka katikati ya jiji. Kutakuwa na ulazima kweli wa mradi wa miaka nenda rudi wa mabasi yaendao kasi

   
 2. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfano wa stand za magari ya mwendo kasi
   

  Attached Files:

 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  @kwa mtoro, nilikuwa na mjadala huu majuzi na mtu. Nimejiuliza kulikuwa na haja ya kufurumua vibarabara vyetu kuongeza njia za mabasi yaendayo kasi wakati kuna idea ya treni? Ingeweza kuwa investment kubwa na ya longterm kuongeza reli na kuimarisha feeder roads tu.

  Anyways, najua kutengeneza barabara ya single lane kwa 1 km ni around 1 b tshs. Kutengeneza reli kwa 1 km ina gharimu sh ngapi?
   
 4. zenmoster

  zenmoster JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mi nadhani sulhisho la kupunguza foleni ni pamoja na kutengeneza good network ya bara bara mjini.... then wakiweka treni toka posta mpaka tegeta na nyingine toka ubungo hadi mbezi analog... then nyingine hadi mbagala tutamaliza kabisa usumbufu wa usafiri maana watu wengi watapaki magari yao na kugombani kwa hudumu kutapungua
   
 5. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  mi nadhani kwa upande wa tegeta au tuseme hadi bagamoyo ingejengwa pantoni ambayo ingeambaa along the coast hadi posta na so kupunguza msongamano wa magari along ally hassan mwinyi na bagamoyo roads.
  Ni maoni tu jamani and i stand to be correctd
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Katika miji mikubwa si rahisi hata kidogo kupata njia moja ikawa ndio dawa ya kutokomeza kero za usafiri.

  Kunahitajika treni zitakazochukua watu kutoka viunga vya mji na kuwafikisha kwenye sehemu za kibiashara na uchumi lakini pia kunahitajika mabasi yatakayoweza kuwa na vituo vifupi fupi zaidi, ambayo yatasaidia kurahisisha kufanya shughuli ndani ya mji wenyewe.
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  Huduma zote zinapaswa kuwepo...ila kwa habari ya train inabidi tuanze kufikiria treni ya kasi "Metro", na wala tusiweke fikra zetu kwenye gogo la TRL au TAZARA. Suala la kutandaza mtandao wa reli za Kigoma hapa mjini hiyo itakua ni akili ndogo hata kama gharama yake iwe ndogo kama kulima tuta la mchicha.
  Kwa sasa tuache treni ifanye kazi kama mpango wa muda mfupi wakati huo tujiwekee malengo ya kuwa na underground metro trains.
   
 8. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu watu8, Nakubaliana na mpango wako wakufikiri mbali, wakati usafiri huu wa (gari moshi), sijui ya umeme inaitwaje mtanisahihisha ukiwa ndio usafiri bei rahisi duniani hapa kwetu itakushangaza kidogo. Nachelea kusema hata mipango ya muda mrefu yakuandaa vyanzo vya nishati ya umeme haipo. Metro train inahitaji Terabites of joules za umeme kujiendesha, wakati sisi hata wa birika lakuchemshia maji unatushinda.

   
 9. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  hahaha...sasa si ndio inabidi tubadilike mkuu, sisi si ndio tumegundua tuna Uranium huko kusini...
   
 10. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu, usiseme kwa nguvu mambo ya Urani ni mazito, kwanza sheria yakutupa taka za Urani unaijua?
  Sisi labda tukomae na kaa letu la mchuchuma liganga, vyura wa kihansi na maji yasiojaa kila siku, na mabo ya geothermal.
   
 11. B

  BLB JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  honestly umetisha mkuu,
  ila kiukweli mi bado cjaelewa huu mradi wa rapid bus utakuaje, alafu ctak m2 aniambie hela inayotumika ni kiac gan nahic kichwa kitaniuma,
   
Loading...