Mabasi ya Mwendo Kasi(DART): Ukiukwaji wa taratibu za utendaji kwa madereva na wakata ticket

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Habari Wanajamii na Uongozi wa DART!
Nimeshindwa kufika ofisi zenu kutokana na majukumu lakini nimeona ni vyema kulifikisha hapa ili wengine wapate kuwasilisha kero zao nanyi mzifanyie kazi.

1. Utaratibu wa Wakata ticket kusitisha huduma saa nne usiku na ticket kuuzwa kinyemela kama unasaidiwa kwa gharama ile ile:
- Kituo cha jiji ndicho mara zote nimekuwa nakutana na hali hii mara nyingi nafika hapa saa nne nanusu ama tano kasoro, Gate la upande wa magharibi mara nyingi linakuwa limefungwa na la upande wa mashariki kunakuwa na askari na mwanamama ambaye anaonekana ni mtendaji wenu. Sasa Swali langu ni kwanini hamuweki wazi muda maalumu wa kufunga ukataji wa ticket na kutoa mwanya kwa watendaji wenu kufanya vile wanavyotaka kufanya?

2. Uharaka wa madereva kabla ya kuhakiki usalama wa abiria:
- Nimelishuhudia hili mara nyingi dereva kuondoa gari kabla ya kuhakiki usalama wa abiria wake. Ni jana tuu begi langu lilibanwa na kupitilizwa kituo. Nikishangazwa na dereva si ana monitor kule anaona kila mwenye kutaka kushuka sasa iweje aondoe gari. What if angenibana mimi na kuniburuza? Naomba ile course mliyowapa wakati wanaanza kutoa huduma muwape tena maana watatuumiza saana.

3. Kituo cha mwendakasi kufungwa kabla ya wakati:
- Nimeshuhudia kuona kituo cha DIT na Mwanamboka vikiwa vimefungwa na kwa mwanamboka abiria tulilzimishwa kutokea pembezoni kwa kuruka mtaro bila ya kuwa na tangazo la dharura.. Shahidi wa hili ni Askari wa kike aliyekuwa lindo usiku wa 04/02/2017 majira ya saa tano kasoro.

Mimi binafsi noamba watendaji wa DART kwa pamoja kushirikiana na kusimamia kwa ukamilifu uendeshaji wa mabasi yetu ambayo Serikali yetu imeweza kutatua kwa kiasi kikubwa adha ya usafiri DSM.
Naamini wanajamvi wenzangu nao wataweka kero zao hapa.
 
Uongozi wa DART tusaidie malalamiko ni mengi lakini hayatatuliwi.
 
Naunga mkono yote uliyoandika na zaidi ni:-
1. Mimi binafsi niliwahi kuripoti tukio la Dereva kuondoa gari kabla ya kufunga milango ili nisiingie ndani ya basi!
2. Wakati huu wa joto, ni wajibu wa madereva kuhakikisha vioo vyote vimefunguliwa pamoja na madirisha ya juu( sunroof).
3. Wakati mwingi mabasi ni machafu, je hayakaguliwi kabla ya kuanza safari?
4. Taa za 'Solar' haziwaki kwenye vituo vingi! Kwa nini hazifanyiwi matengenezo ili ziwake umeme unapokatika?
5. Uratibu mbovu wa safari, hawajali wingi wa watu kwenye vituo. Kazi nyingine ya wauza tiketi kwenye vituo iwe ni kutoa taarifa ya wingi wa abiria kwenye vituo, hasa vya kati kati ili kupunguza muda wa kusubiri mabasi.
 
UDART tunadanganyana tu.......METRO BUS zipo huko kwa wenzetu mpaka raha.
 
Back
Top Bottom