Mabasi ya AL SAEDY yanatapeli wateja

vamda

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
865
535
Ndugu wana jf. Salamu kwenu. Niende kwenye mada. Leo jumamosi tarehe 19. 01. 2019 nilipanda basi LA AL SAEDY lenye namba T 990 DGZ kutoka morogoro kwenda dar es salaam. Mnamo saa 10 alasiri basi liliendelea kujaza abiria tukidanganywa basi lingetoka baada ya dakika 5. Nilitoa noti ya elfu 10 sikupewa chenji ingawa nilipokomaa kudai nilipewa. Tuliambiwa kwamba basi lina kiyoyozi na huduma ya kuchaji simu. Niliingia ndani ya basi vitufe vya kuchaji simu vyote vibovu. Kiyoyozi kiliwashwa kwa muda tu. Basi liliondoka saa 12 jioni. Kiyoyozi kikazimwa. Tukaambiwa tufungue madirisha. Tulilalamika lkn hatukusikilizwa. Wafanyakazi wa basi la SAEDY namba T 990 DGZ walituonesha shoo ya KIBABE. Sijui km tajiri anajua yanayotendeka kwenye mabasi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom