Mabasi ya Abood

smartfocus

Member
Oct 4, 2015
62
50
Wapendwa wana jamvi.

Nakubaliana kabisa na kauli mbiu ya Jeshi la Polisi ya Mwendo Kasi unaua.

Ila sasa haya mabasi ya Abood yana kero sana hasa baada ya kupita Chalinze au kama yanakuja Dar es Salaam yanakua yanaendeshwa kwa mwendo wa pole pole mno kama 20km/hr.Yani mahali ambapo hakuna kibao kinachozuia mwendo huo lakini utakuta ndiyo mwendo mabasi haya yanatembea nayo. Hii nimeexperience kwa mabasi yote ya abood kwa madereva tofauti na kwa wadau zaidi ya watatu. Abiria wanalalamika ila ndiyo hivyo tena ..

Muhisika embu lifanyie kazi hili.
Mwendo Kasi Unaua japo Mwendo Pole Unachelewesha.Mwendo wa Kati Salama kama kanuni zingine zikizingatiwa.
 
Siku hizi hakuna safari kuanzia Chalinze mpaka Dar. Wenzako tunafanyaga hivi. Toka Moro hadi Chalinze unatembea mpaka 130. Hapo unatumia dk 45 tu. Toka Chalinze hadi Dar, unatembea Average ya 60_70 Hapo utatumia masaa mawili. So within three hours safari yako inakamilika.
 
Yanayokimbia ni Yale yanayoka Ubungo au Morogoro kuanzia SAA kumi na mbili jioni japo kwa Dar Moro safari za Usiku ni risk.Kuna abiria sio waaminifu nilishawahi ibiwa kila kitu nilienda kuzindukia siku ya pili nikiwa nimelazwa hospital ya mkoa Morogoro
 
Polepole ndiyo mwendo.... waswahili bhana tuna shida sana.. basi likiendeshwa na derava mmoja hapana aaa aaa abiria wote twataka tuwe madereva au tushuke usukani....
Rais JPM anatumbua majipi.... huku wengine wanakurupuka kuchafuwa hewa !!!
 
Siku hizi hakuna safari kuanzia Chalinze mpaka Dar. Wenzako tunafanyaga hivi. Toka Moro hadi Chalinze unatembea mpaka 130. Hapo unatumia dk 45 tu. Toka Chalinze hadi Dar, unatembea Average ya 60_70 Hapo utatumia masaa mawili. So within three hours safari yako inakamilika.

bangi za kuvutia uchochoroni mbaya sana aisee
 
Yanayokimbia ni Yale yanayoka Ubungo au Morogoro kuanzia SAA kumi na mbili jioni japo kwa Dar Moro safari za Usiku ni risk.Kuna abiria sio waaminifu nilishawahi ibiwa kila kitu nilienda kuzindukia siku ya pili nikiwa nimelazwa hospital ya mkoa Morogoro
Pole sana mkuu
 
morogoro aliyekuwa akitembea kwenda dar ni kibedui tu na alikuwa chizi,dudubaya anamjua,na madereva wa abood,hood,islam wakimkuta njiani tu lazima wambebe,sasa ww dar moro utembee utakuwa upo timamu kweli sheikh??
Aah. Ukiwa dereva utajua kutumia lugha za kitaalam. Kutembea means kuendesha chombo katika spidi fulani. Hujasoma kwenye kiswahili juu ya matumizi ya maneno kulingana na muktadha au mazingira? Mfano mtu wa hotel atasema, lete chai moja etc
 
morogoro aliyekuwa akitembea kwenda dar ni kibedui tu na alikuwa chizi,dudubaya anamjua,na madereva wa abood,hood,islam wakimkuta njiani tu lazima wambebe,sasa ww dar moro utembee utakuwa upo timamu kweli sheikh??
da kweli ni kibedui pekee ndiyo alikuwa akitembea kuelekea dar.
 
Niliwahi kuluzungumzia hilo humu.
Mim nime experience ktk hiz yutong mpya afadhal hata zile marcopolo kidog zinatembea.
Sijui wamepigwa mkwara gan siku hiz sio zileAndate ninazozijua,bora ya BM analuwa mmbadala wa Abood,Al Saed tatizo lake n kama daladala kusimama njian kwa sana
 
Siku hizi hakuna safari kuanzia Chalinze mpaka Dar. Wenzako tunafanyaga hivi. Toka Moro hadi Chalinze unatembea mpaka 130. Hapo unatumia dk 45 tu. Toka Chalinze hadi Dar, unatembea Average ya 60_70 Hapo utatumia masaa mawili. So within three hours safari yako inakamilika.

Toka Chalinze kwenda Dar barabara ni mbaya na askari wa usalama wanavizia magari na kuwasingizia maderefa makosa ya uwongo.. it totally unethical
 
Tatizo tochi nyingi kipande cha Chalinze - Dar, yange yange wanazingua sana njiani af utakuta wengine wanajificha hadi vichakani na mitochi yao. We utashangaa tu kuluputi wamechomoza unaambiwa weka chombo kushoto.
Nakumbuka week kadhaa nyuma tulikuwa na safari ya moro tukaenda na gari private yani ilikuwa kila baada ya km5 mpk km7 tunasimamishwa eti kipimo kinasoma mmezidi mwendo, tukachoka huo ujinga tukakubali kulimwa fine tukapewa form flani ya kudhibitisha hilo ndio tukawa tunaitumia kama reference kwenye next checkpoint kuwa tushawapa chao watusamehe tu!
Tulitoka Dar saa2 tukafika Moro saa6 kwa private car, wakati ilibidi iwe safari ya masaa mawili tu!
 
Back
Top Bottom