Mabasi ya abiria: Ufisadi wa hali ya juu

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Tangazo la serikali kuzuia mabasi uingizaji wa mabasi ya abiria yenye zaidi ya miaka 5 ni Ufisadi wa hali ya juu na hujuma kwa sekta ya usafiri Tanzania.
Nataka kuingiza mabasi ya bairia ya kibashara lakini nimetembelea mitandao ya wauzaji magari maarufu wa Japan ili kupata magari hayo lakini wote wameniambia siwezi kupata mabasi hayo.

Nimegundua hata Ulaya, Asia na Afrika Kusini ambao ni bora kuliko sisi kiuchumi wanaruhusu uingizaji wa Mabasi yaliyotumika kwa zaidi ya miaka 5. Sisi tunakipi cha kutufanya tuwe jeuri kiasi cha kukataa mabasi hayo na barabara za kulazimisha watu kutembeza magari mapya?

Nadhani hapa kuna mkono wa Mtu, nisaidieni Wana JF nataka kuingiza mabasi lakini nimeshindwa kuyapata kwa ajili ya Ufisadi huu wa waziwazi na hujuma dhidi ya WaTz.
 

Attachments

  • SKMBT_C35308080716160.JPG
    SKMBT_C35308080716160.JPG
    265.9 KB · Views: 52
Imekuwa kero sana kuhusu suala la wanafunzi kulipa nauli wakati kuna mi jibaba na mijimama na mijikaka haina hata iabu imevaa miguo ya kijeshi inataka kutimiza uana jeshi wao kwa kutolipa nauli ya daladala na matokeao yake kupanda kibaba kwenye magari ya watu.

hayo magari yamelipiwa na yamenunuliwa kwa ghalama na hakuna kitu cha bule miaka hii kama unalipwa na wewe lipa kama unataka kula na wewe uliwe .

kwa kweli kikwete huo msemo hakukosea.

sasa wanajeshi mlipe nauli na wanafunzi ni free.

leteni hoja.
 
LABDA MAFISADI WANATAKA WAO NDO PEKEE WAWE NA HAYO MAGARI YA ABIRIA KWANI NDO WENYE UWEZO WA KUNUNUA MAPYA.....!
KIZAZI HIKI CHENYE KUFANYA MAAMUZI KUNA KITU INAELEKEA WALIKULA UTOTONI MWAO AMBACHO KINAATHIRI MAAMUZI MUHIMU HIVI SASA (joke) KWANI MAAMUZI MENGI MABOVU HUFANYWA NA WATU WA RIKA FULANI (45-60's?)
 
Suluhisho la tatizo hili ni kuwafuata mafisadi huko huko juu waliko na kutwaa viti walivyokalia.
Hatuwezi tatua matatizo ya nchi yetu kwa kutegemea kwamba mafisadi kadhaa watatuonea huruma na kuamua kutupigania kwa moyo mmoja.
Hakuna yeyote kati ya viongozi tulionao alizaliwa kuongoza, wengi wapo hapo kwa ajili ya matumbo yao yasiyoshiba.
Zaidi wapo ili kuwatumikia Mabwana zao wenye nia ya kunyonya damu na musuli ya uchumi wa Tanzania.
Tuwafuate huko huko juu, kama hakutoshi tutabanana hivyohivyo.
 
bora wangezuia malori na si mabasi, mabasi mengi ya tanzania yameundwa kutokana na malori.

wanaoleta hizi sheria za ajabu ajabu sijui huwa wanalalia ubavu mbaya, kuna time ilisemwa, eti mabasi ya scania yote ni marufuku kuwa na engine za 113, ni za 93 tu, utekelezaji hakuna na mambo yanakwenda tu.

ushauri wa bure kabisa, ni bora waruhusu watu kuagiza mabasi kutoka nje na kupiga marufuku kuunda basi kutokana na lori!
 
bora wangezuia malori na si mabasi, mabasi mengi ya tanzania yameundwa kutokana na malori.

wanaoleta hizi sheria za ajabu ajabu sijui huwa wanalalia ubavu mbaya, kuna time ilisemwa, eti mabasi ya scania yote ni marufuku kuwa na engine za 113, ni za 93 tu, utekelezaji hakuna na mambo yanakwenda tu.

ushauri wa bure kabisa, ni bora waruhusu watu kuagiza mabasi kutoka nje na kupiga marufuku kuunda basi kutokana na lori!

Regulation yenyewe inasema hivi:
"Under the said regulations, passenger vehicle means a vehicle that is constructed or adopted solely for carriage of more than seven persons and a driver"
 
Back
Top Bottom