Mabasi kulala njiani chanzo cha ulevi na ngono zembe

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Salam kwenu nyote, wapendwa wa Bwana!

Kuna hili swala la mabasi yatokayo mikoani kwenda Dar es Salaam (na mikoa mingine ya mbali) kulala njiani, either Morogoro, Shinyanga, Makambako nk. Mfano basi za Mwanza/Bukoba - Dar es Salaam huwa zinalala Morogoro mjini eneo la Msamvu, au yale ya kwenda Kanda ya Ziwa kulazimika kulala Shinyanga nk.

Kwakweli abiria wanapofika vituo hivyo, wengi hulala kwenye mabasi wakiwa na watoto, ndugu na marafiki. Wengine wakiwemo na makonda, madereva huanza kulewa tu. Mbaya zaidi, na wengine kufanya mapenzi.

Utakuta mwanaume amekaa siti moja na mwanamke toka Mwanza wakielekea Dar es Salaam, njiani huongea mengi na hatimae kufahamiana vizuri zaidi mwishoni kutongozana. Sasa wanapofika Morogoro saa 2 usiku halafu gari inapack mpaka kesho yake, wengi huingia sehemu za kulala wageni na kufanya yao.

Unaweza pia ukampakia mtoto wako wa kike anaporudi toka likizo, anajinafasi vizuri anaposikia gari huwa inatia nanga maeneo (mkoa) fulani.

Jana nikiwa eneo la Msamvu Morogoro, nilishuhudia madereva na raia wengine wakipiga mvinyo. Pia wengine wakawa busy kutafuta sehemu za kulala wageni ili wajipumzishe tayari kwa kuendelea na safari ya leo.

Naishauri serikali iruhusu safari za moja kwa moja ili abiria wasiwe wanalala njiani maana ni chanzo cha ulevi, uzinzi, na mambo mengine.
 
Ajali zikiwa nyingi lawama kwa serikali,zikipunguzwa(kwa maderava kupunguziwa speed ya kuendesha) lawama kwa serikali.
 
wala siyo tatizo ili mradi wafike salama na watumie salama!!
kwa upande wa madereva hawatakiwi kunywa kabisa bila kujari anaendesha basi au gari ndogo.
 
Na ni determinant kubwa ya kuenea kwa maambukizi ya VVU, utakuta saa 3 tu mabasi yameshazuiwa, wakati yana madereva wawili. Hatari sana
 
Wakilala wote na kunjunjana ni makubaliano yao. Mimi nimelala Kahama na Msamvu zaidi ya mara 20 nikiwa natoka ama naenda Bukoba lakini sijawahi kulala na mwanamke gesti.
Kweli hata mm huwa sioni mantiki ya kulala na mtu from nowhere eti kisa gari inatakiwa kupaki njiani nyakati za usiku
 
Hivi Kenya na Uganda kuna amani sana?Maana kule mabasi yanatembea usiku.Nakumbuka enzi za Nyerere tulikuwa tukipanda basis saa 2 usiku kutoka mza kuelekea msm,Sikh hizi usiku serikali inakuwa imelala?
Mkuu Hali kwa sasa ni mbaya sana juzi nimekoswa kutekwa kwa hiyo nashauri bora kulala kuliko kutembea usiku
 
Back
Top Bottom