Mabasi Arusha - Dar Acheni maringo

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Kuna kamtindo kameanza siku hizi hasa msimu huu sikukuu zinavokaribia makondakta wa mabasi ya Arusha Dar wanakataa kupakia abiria wa Moshi. Na ikatokea ukipanda wana kauli chafu za kukera. Kuna watu wengi wanaishi Arusha ila wanafanya kazi Moshi na wanategemea mabasi haya makubwa kuwahi Kazini Moshi maana ukipanda hizi coaster lazima uchelewe kazi maana zinasimama kila kituo na hata sehemu ambazo hazina vituo
Marangu luxury coach, Extra luxury coach, Skyline ndio yanaongoza kwa dharau
 
Bus ni arusha-dar. Wewe unapanda unaishia moshi, ni sawa bus la dar-arusha uishie kibaha.
Kwanza unalipa nauli ya arusha-dar au arusha-moshi?
Kama unalipa nauli ya moshi huoni unawasumbua wakifika moshi waanze kupoteza muda kutafuta abiria anaeenda dar?
 
Wapo sahihi. ..basi limeandikwa ARUSHA-DAR wewe unataka kupanda ushukie MOSHI upooz...hapa mawili uwahi kuamka upande coaster ama utumie usafiri binafsi uwahi ofisI.
 
Panda mabasi ya kilimanjaro hawana maringo ila ujieleze mapema unashukia moshi, mchaga haachi hela jombaaa
 
Bus ni arusha-dar. Wewe unapanda unaishia moshi, ni sawa bus la dar-arusha uishie kibaha.
Kwanza unalipa nauli ya arusha-dar au arusha-moshi?
Kama unalipa nauli ya moshi huoni unawasumbua wakifika moshi waanze kupoteza muda kutafuta abiria anaeenda dar?

Wapo sahihi. ..basi limeandikwa ARUSHA-DAR wewe unataka kupanda ushukie MOSHI upooz...hapa mawili uwahi kuamka upande coaster ama utumie usafiri binafsi uwahi ofisI.
Hili ni jambo la kawaida sana kwa wakazi wa moshi na arusha wanaofanya kazi mkoa mwingine na kulala kwingine wengi wanategemea kupanda mabasi ya masafa marefu ili wawahi kazini kwa muda kwani ukitegemea usafiri na coaster hapo andika maumivu ya kuchelewa... Hilo kusema utasumbua wakushushe njiani ni upuuzi kwani mabasi yote yanayotoka Arusha kwenda dar lazima yapitie moshi kujaza abiria ndipo waendelee na safari so hapo sioni kama kuna tatizo...
 
Ni kweli ila sikukuu zikipita wanabeba hata abiria anaeshuka usa
 
Hili ni jambo la kawaida sana kwa wakazi wa moshi na arusha wanaofanya kazi mkoa mwingine na kulala kwingine wengi wanategemea kupanda mabasi ya masafa marefu ili wawahi kazini kwa muda kwani ukitegemea usafiri na coaster hapo andika maumivu ya kuchelewa... Hilo kusema utasumbua wakushushe njiani ni upuuzi kwani mabasi yote yanayotoka Arusha kwenda dar lazima yapitie moshi kujaza abiria ndipo waendelee na safari so hapo sioni kama kuna tatizo...
Upuuzi pia ni kulazimisha bus la arusha-dar ligeuke daladala za arusha-moshi. Ndio maana huwezi kufanya chochote zaidi ya kulakamika kwasababu hawavunji masharti ya leseni yao. Kama unahofia kuchelewa wahi kuamka kuliko kulazimisha bus la watu 65 lifuate ratiba zako kinyume na leseni yao. Walioweka coaster za arusha-moshi sio wajinga.
 
Sielewi ni kwanini huu mjadala umefika hapa. Suluhisho ni moja tu, nunua usafiri wako.
 
Upuuzi pia ni kulazimisha bus la arusha-dar ligeuke daladala za arusha-moshi. Ndio maana huwezi kufanya chochote zaidi ya kulakamika kwasababu hawavunji masharti ya leseni yao. Kama unahofia kuchelewa wahi kuamka kuliko kulazimisha bus la watu 65 lifuate ratiba zako kinyume na leseni yao. Walioweka coaster za arusha-moshi sio wajinga.
Haina haja ya kubishana yawezekana hujui unachokiongea, arusha na moshi ni route ya mkoa to mkoa hapo inaondoa dhana yako ya kusema yanageuzwa daladala... by the way huu ni utaratibu wetu wa miaka mingi kuwahi kazini asubuhi kwa huo usafiri kwani nauli tunalipa wenyewe usitupangie tupande nini...
 
Mimi wala sikupangii. Anaepangia watu ni anaelazimisha bus lifuate anavyotaka yeye. Wakikubali kukupakia sawa, wakikataa huwezi kuwalazimisha. Wengine wamesema Kilimanjaro bus hawakatai si lazima kupanda wanalokataa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom