Mabaraza ya mawaziri yaliyopita

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,227
113,583
Kuna watu ambao hawajafurahishwa na saizi ya baraza la mawaziri lililotangazwa leo. Sasa mimi nauliza, hili baraza ukilinganisha na mabaraza mengine yaliyopita, ni kubwa kiasi gani?

Nakumbuka enzi zile za mawaziri wasio na wizara maalumu. Sijui hawa kazi zao zilikuwaga nini.
 
Mawaziri vivuri nasikia wapo Zenji, CUF, watatusaidie kujua kazi zao ni zipi. Makamu wa Kwanza zenji ndo najua, kupambana na ukimwi, madawa ya kulevya, na mazingira la mwisho sitaji.
 
Ni vizuri pia kujiuliza kazi za waziri nini? Hii inatia mashaka hasa pale mtu anachaguliwa kuongoza wizara wakati hana utaalamu wa mambo yanashughulikiwa na wizara hio. kwa mantiki hio hakuna haja ya kuwa na wizara lukuki wakati watendaji (wakuu wa idara) ni walewale.
Tumeishaona Mawaziri ambao wanapelekewa maazimio kusaini bila hata kusoma au wakisoma hawaelewi maana yake nini. Inabidi tujifunze toka kwa nchi zilizoendelea jinsi wanavyojenga mabaraza yao ya mawaziri ambayo ni madogo na yamejaa ufanisi.
 
Mimi nataka kujua tu saizi ya mabaraza yaliyopita ukilinganisha na hili la sasa....
 
Back
Top Bottom