Mabaraza ya Kata hayana mamlaka ya kusikiliza na kuamua migogoro ya ardhi

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Kwa mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya Sheria namba 3 ya mwaka 2021, WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENT NO 3 ) ACT, 2021

Kwa mujibu wa SHERIA hii ambayo ilikifuta kifungu Cha 15 Cha THE LAND DESPUTE COURTS ACT, CAP 216 R E 2019 ambacho kiliwapa mamlaka Baraza la Kata (Ward Tribunal Kusikiliza mashauri yanahusiana na masuala ya ardhi.

Ambapo kifungu hicho lazima kisomwe pamoja na kifungu Cha 10 Cha SHERIA YA MABARAZA YA KATA SURA YA 206 MAREJEO YA 2002
(THE WARD TRIBUNAL ACT CAP 206 R.E 2002)

Ambapo vifungu vyote hivyo viliwapa mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yote yanahusiana na mambo ya ardhi yasiyozidi thamani ya shilingi million tatu (3,000,000/=)

Hivyo Baraza La Kata lilipewa nguvu za kimahakama ambapo tunaweza kusema ilikuwa ni kama Mahakama ya mwanzo.

Kwahiyo sehemu ambayo mtu alikuwa anaanzia kufungua Kesi inayohusu mambo ya ardhi ilikuwa ni Baraza La Kata.

Sasa Mtu asiporidhika anakata rufaa kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya(DLHT) rufaa yake inaenda Mahakama Kuu Kitengo Cha Ardhi na Kisha Mahakama ya Rufani. (Hivyo ndivyo ilikuwa kiutaratibu)

Sasa mwaka Jana 2021 Kuna mapendekezo ya mabadiliko ya SHERIA mbalimbali ambayo yalifanywa na kawaida sheria haiwezi kuwa sheria Hadi pale raisi atakavyoidhinisha.

Sasa takribani miezi mitatu iliyopita Hangaya aliidhinisha mabadiliko hayo na Sasa yanafanya kazi ikiwa ni pamoja na _Kuruhusu Mawakili Wa Kujitegemea Kuingia Mahakama ya Mwanzo.

Mabadiliko mengine ni Kutokuwahusisha wazee waungwana Wa Mahakama kwenye Mahakama ya Mwanzo.

Sasa mabadiliko hayo yaliikumba pia vyombo vinavyohusika kushughulikia masuala ya ARDHI.

Mabadiliko yaliyofanyika ni kwamba Kwa sasa Baraza La Kata halina mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yoyote ya ardhi Kwa Maana ya kutoa Hukumu au nguvu za kimahakama na kiufupi tunaweza kusema wamenyang'anywa MAMLKA ya kimahakama

Kwa sasa Baraza La Kata linafanya kazi kama Baraza la usuluhishi tu.

Yaani ikitokea Kuna watu wana Mgogogro unahusiana na ardhi akienda Baraza La Kata watawasikiliza na wanatoa ushauri tu kuwa labda kwenye suala hili mtu B umeingilia Kwa Mtu A na hivyo Hilo shamba uliache basi.

Kwa namna nyingine tunaweza kusema Baraza La Kata watawasikiliza na kutoa ushauri tu au kuwasuluhisha na kuhakikisha suala lenu linashughulikiwa Bila kufikia kwenye vyombo VYA kisheria.

Baraza la Kata watakuwa Hawana mamlaka hata ya kuandaa hukumu/ Kwasasa baraza la kata haliwezi kutoa hukumu

Na baraza la kata wanatakiwa Kusuluhisha suala Hilo Kwa muda wa siku 30 na watakiwa kutoa cheti ikiwa watu wenye mgogoro wameshindwa kufika hitimisho au maamuzi.

Ambapo kama mgogoro haujasuluhishika basi mmoja wapo asiyeridhika basi ataenda na cheti ambacho kimetolewa na Baraza la kata na Kisha ataenda kufungua shauri rasmi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ulipo Mgogogro husika ambapo litasikilizwa rasmi ikiwa ni pamoja na kutolewa hukumu.

Kwa mashauri ambayo YALIKUWA yakiendelea kwenye Baraza la kata hayo yataendelea Kwa utaratibu wa zamani na yatatakiwa kumalizika Hadi kufika hatua ya hukumu.

Lakini Kesi yoyote inayoenda baraza la kata Kwasasa basi sheria mpya itatumika.

Ikiwa ni ule utaratibu wa Kusuluhisha Tu na kupewa cheti pale ambapo mmoja wao hajaridhika ili kumruhusu kuendelea mbele kufungua shauri na Kusikiliza.

Sasa ikiwa mfano Baraza La Kata la wakasikiliza na kuandaa hukumu Hilo litakuwa ni kosa kisheria na utaratibu huo utakuwa ni batili na hautakuwa na jambo lolote kisheria.

Kwa Maana ya Kuwa The procedure and proceedings shall be nullified so becomes fatal.
 
Bora. Hawa wajumbe wa baraza wameleta shida sana kwa kuwa na wered dhaifu. Kias kwamba unakuta rufaa zinagonga mwamba kwa facts dhaifu za baraza la kata
 
Hapo awali mabaraza yalishughulika na mgogoro usiozidi sh.3,000,000/=.
Utaratibu wa sasa ukoje?
 
_________________________________________

Kwa mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya Sheria namba 3 ya mwaka 2021, WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENT NO 3 ) ACT, 2021
.
Kwa mujibu wa SHERIA hii ambayo ilikifuta kifungu Cha 15 Cha THE LAND DESPUTE COURTS ACT, CAP 216 R E 2019 ambacho kiliwapa mamlaka Baraza la Kata (Ward Tribunal Kusikiliza mashauri yanahusiana na masuala ya ardhi.
.
Ambapo kifungu hicho lazima kisomwe pamoja na kifungu Cha 10 Cha SHERIA YA MABARAZA YA KATA SURA YA 206 MAREJEO YA 2002
(THE WARD TRIBUNAL ACT CAP 206 R.E 2002)
.
Ambapo vifungu vyote hivyo viliwapa mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yote yanahusiana na mambo ya ardhi yasiyozidi thamani ya shilingi million tatu (3,000,000/=)
.
Hivyo Baraza La Kata lilipewa nguvu za kimahakama ambapo tunaweza kusema ilikuwa ni kama Mahakama ya mwanzo .
.
Kwahiyo sehemu ambayo mtu alikuwa anaanzia kufungua Kesi inayohusu mambo ya ardhi ilikuwa ni Baraza La Kata.
.
Sasa Mtu asiporidhika anakata rufaa kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya(DLHT) rufaa yake inaenda Mahakama Kuu Kitengo Cha Ardhi na Kisha Mahakama ya Rufani. (Hivyo ndivyo ilikuwa kiutaratibu)
.
Sasa mwaka Jana 2021 Kuna mapendekezo ya mabadiliko ya SHERIA mbalimbali ambayo yalifanywa na kawaida sheria haiwezi kuwa sheria Hadi pale raisi atakavyoidhinisha,
.
Sasa takribani miezi mitatu iliyopita Hangaya aliidhinisha mabadiliko hayo na Sasa yanafanya kazi ikiwa ni pamoja na _Kuruhusu Mawakili Wa Kujitegemea Kuingia Mahakama ya Mwanzo.
.
Mabadiliko mengine ni Kutokuwahusisha wazee waungwana Wa Mahakama kwenye Mahakama ya Mwanzo.
.
Sasa mabadiliko hayo yaliikumba pia vyombo vinavyohusika kushughulikia masuala ya ARDHI.
.
Mabadiliko yaliyofanyika ni kwamba Kwa sasa Baraza La Kata halina mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yoyote ya ardhi Kwa Maana ya kutoa Hukumu au nguvu za kimahakama na kiufupi tunaweza kusema wamenyang'anywa MAMLKA ya kimahakama
.
Kwa sasa Baraza La Kata linafanya kazi kama Baraza la usuluhishi tu.
.
Yaani ikitokea Kuna watu wana Mgogogro unahusiana na ardhi akienda Baraza La Kata watawasikiliza na wanatoa ushauri tu kuwa labda kwenye suala hili mtu B umeingilia Kwa Mtu A na hivyo Hilo shamba uliache basi.
.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema Baraza La Kata watawasikiliza na kutoa ushauri tu au kuwasuluhisha na kuhakikisha suala lenu linashughulikiwa Bila kufikia kwenye vyombo VYA kisheria.
.
Baraza la Kata watakuwa Hawana mamlaka hata ya kuandaa hukumu/ Kwasasa baraza la kata haliwezi kutoa hukumu
.
Na baraza la kata wanatakiwa Kusuluhisha suala Hilo Kwa muda wa siku 30 na watakiwa kutoa cheti ikiwa watu wenye mgogoro wameshindwa kufika hitimisho au maamuzi.
.
Ambapo kama mgogoro haujasuluhishika basi mmoja wapo asiyeridhika basi ataenda na cheti ambacho kimetolewa na Baraza la kata na Kisha ataenda kufungua shauri rasmi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ulipo Mgogogro husika ambapo litasikilizwa rasmi ikiwa ni pamoja na kutolewa hukumu.
.
Kwa mashauri ambayo YALIKUWA yakiendelea kwenye Baraza la kata hayo yataendelea Kwa utaratibu wa zamani na yatatakiwa kumalizika Hadi kufika hatua ya hukumu.
.
Lakini Kesi yoyote inayoenda baraza la kata Kwasasa basi sheria mpya itatumika.
.
Ikiwa ni ule utaratibu wa Kusuluhisha Tu na kupewa cheti pale ambapo mmoja wao hajaridhika ili kumruhusu kuendelea mbele kufungua shauri na Kusikiliza.
.
Sasa ikiwa mfano Baraza La Kata la wakasikiliza na kuandaa hukumu Hilo litakuwa ni kosa kisheria na utaratibu huo utakuwa ni batili na hautakuwa na jambo lolote kisheria.
.
Kwa Maana ya Kuwa The procedure and proceedings shall be nullified so becomes fatal.

__________________________________________

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ya ovyo kabisa hayo mabaraza.
Mwenye pesa ndio mshindi.
 
Gharama za kuleta baraza la kata kwenye eneo la tukio Kwa mfano Kuna mgogoro wa mpaka wa majirani wawili jirani mmoja ndiye aliyekwenda kushitaki baraza la kata gharama anazibeba nani
 
Wale ni wazee wa ccm,maneno meengi,ila kichwani weupe?rushwa ndio kipaumbele chao.

Wahuni sana wale jamaa aisee

Mzee mmoja kanifata akanambia mwenzako katoa 800k kama unataka kumshinda toa 1.5m tukupe ushindi tukuandikie na hukumu nzuri ambayo hata akikata rufaa mahakamani utashinda...... almanusura nimzabe kibao
Sikwenda hata kwenye hukumu yao nikanyoosha goti mahakamani
 
_________________________________________

Kwa mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya Sheria namba 3 ya mwaka 2021, WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENT NO 3 ) ACT, 2021
.
Kwa mujibu wa SHERIA hii ambayo ilikifuta kifungu Cha 15 Cha THE LAND DESPUTE COURTS ACT, CAP 216 R E 2019 ambacho kiliwapa mamlaka Baraza la Kata (Ward Tribunal Kusikiliza mashauri yanahusiana na masuala ya ardhi.
.
Ambapo kifungu hicho lazima kisomwe pamoja na kifungu Cha 10 Cha SHERIA YA MABARAZA YA KATA SURA YA 206 MAREJEO YA 2002
(THE WARD TRIBUNAL ACT CAP 206 R.E 2002)
.
Ambapo vifungu vyote hivyo viliwapa mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yote yanahusiana na mambo ya ardhi yasiyozidi thamani ya shilingi million tatu (3,000,000/=)
.
Hivyo Baraza La Kata lilipewa nguvu za kimahakama ambapo tunaweza kusema ilikuwa ni kama Mahakama ya mwanzo .
.
Kwahiyo sehemu ambayo mtu alikuwa anaanzia kufungua Kesi inayohusu mambo ya ardhi ilikuwa ni Baraza La Kata.
.
Sasa Mtu asiporidhika anakata rufaa kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya(DLHT) rufaa yake inaenda Mahakama Kuu Kitengo Cha Ardhi na Kisha Mahakama ya Rufani. (Hivyo ndivyo ilikuwa kiutaratibu)
.
Sasa mwaka Jana 2021 Kuna mapendekezo ya mabadiliko ya SHERIA mbalimbali ambayo yalifanywa na kawaida sheria haiwezi kuwa sheria Hadi pale raisi atakavyoidhinisha,
.
Sasa takribani miezi mitatu iliyopita Hangaya aliidhinisha mabadiliko hayo na Sasa yanafanya kazi ikiwa ni pamoja na _Kuruhusu Mawakili Wa Kujitegemea Kuingia Mahakama ya Mwanzo.
.
Mabadiliko mengine ni Kutokuwahusisha wazee waungwana Wa Mahakama kwenye Mahakama ya Mwanzo.
.
Sasa mabadiliko hayo yaliikumba pia vyombo vinavyohusika kushughulikia masuala ya ARDHI.
.
Mabadiliko yaliyofanyika ni kwamba Kwa sasa Baraza La Kata halina mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yoyote ya ardhi Kwa Maana ya kutoa Hukumu au nguvu za kimahakama na kiufupi tunaweza kusema wamenyang'anywa MAMLKA ya kimahakama
.
Kwa sasa Baraza La Kata linafanya kazi kama Baraza la usuluhishi tu.
.
Yaani ikitokea Kuna watu wana Mgogogro unahusiana na ardhi akienda Baraza La Kata watawasikiliza na wanatoa ushauri tu kuwa labda kwenye suala hili mtu B umeingilia Kwa Mtu A na hivyo Hilo shamba uliache basi.
.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema Baraza La Kata watawasikiliza na kutoa ushauri tu au kuwasuluhisha na kuhakikisha suala lenu linashughulikiwa Bila kufikia kwenye vyombo VYA kisheria.
.
Baraza la Kata watakuwa Hawana mamlaka hata ya kuandaa hukumu/ Kwasasa baraza la kata haliwezi kutoa hukumu
.
Na baraza la kata wanatakiwa Kusuluhisha suala Hilo Kwa muda wa siku 30 na watakiwa kutoa cheti ikiwa watu wenye mgogoro wameshindwa kufika hitimisho au maamuzi.
.
Ambapo kama mgogoro haujasuluhishika basi mmoja wapo asiyeridhika basi ataenda na cheti ambacho kimetolewa na Baraza la kata na Kisha ataenda kufungua shauri rasmi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ulipo Mgogogro husika ambapo litasikilizwa rasmi ikiwa ni pamoja na kutolewa hukumu.
.
Kwa mashauri ambayo YALIKUWA yakiendelea kwenye Baraza la kata hayo yataendelea Kwa utaratibu wa zamani na yatatakiwa kumalizika Hadi kufika hatua ya hukumu.
.
Lakini Kesi yoyote inayoenda baraza la kata Kwasasa basi sheria mpya itatumika.
.
Ikiwa ni ule utaratibu wa Kusuluhisha Tu na kupewa cheti pale ambapo mmoja wao hajaridhika ili kumruhusu kuendelea mbele kufungua shauri na Kusikiliza.
.
Sasa ikiwa mfano Baraza La Kata la wakasikiliza na kuandaa hukumu Hilo litakuwa ni kosa kisheria na utaratibu huo utakuwa ni batili na hautakuwa na jambo lolote kisheria.
.
Kwa Maana ya Kuwa The procedure and proceedings shall be nullified so becomes fatal.

__________________________________________

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mtu aliyeshitakiwa anatakiwa afanyeje kama baraza la kata halijasuluhisha mpaka siku 30 zimepita. Hii ni kwa sababu ya usumbufu anaoupata kwa madai ambayo kwake yeye si ya kweli. Kwa mfano kama alikuwa kwenye mipango ya kuwekeza kwa mfano kujenga nyumba za biashara akashitakiwa baraza la kata kuwa siyo mmiliki halali wa eneo linalohusika lakini hata baada ya siku 30 baraza la kata baada ya kusikiliza pande zote mbili ikiwa ni pamoja na site visit bado lipo kimya.
 
Haya mabaraza yalikua ya kikonyo sana

Almanusura nidhulumiwe shamba langu nika songa mbele mahakamani ndio nikapata haki yangu

Wana njaa sana wale wazee
Mabaraza ni ya hovyo sana,yaani wao walikua hawangali haki iko wapi,wao wanaangalia kwenye mgogoro nani mwenye pesa ndiyo wanampaa ushindi,hata Kama vielelezo vilivyoletwa ni vya kugushi wao Baraza hawajali hilo kabisa,wao shida yao ni pesa na unapewa ushindi wa giza!!
 
Back
Top Bottom