Mabango yasemayo 'Tunaongeza nguvu za kiume' Yapigwa Marufuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabango yasemayo 'Tunaongeza nguvu za kiume' Yapigwa Marufuku

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,222
  Likes Received: 4,018
  Trophy Points: 280
  SERIKALI imepiga marufuku matangazo na mabango yaliyozagaa barabarani yanayotangaza kuwa tunaongeza nguvu za kiume kwa kuwa yanapotosha jamii na kuharibu watoto nchini. Hayo yalisemwa jana katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Benjamini Mkapa Shule ya Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Serikali imesema matangazo hayo yanapotosha jamii na kuharibu watoto Kwa kuwa watoto wanajikita kwenda huko na kujikuta wanaharibika na kuharibu kizazi tulichokuwa nacho.

  Akisoma hotuba hiyo kwa niaba ya Serikali ,Julius Mndolwa alisema kuwa matangazo hayo yanaharibu watoto kwa kuwa watoto wanakwenda kwa waganga hao ili kujaribu na baadae kuharibika kwa kuwa yamekuwa yakiwaletea matatizo kwa kushawishika na ngono muda wote.

  Hivyo wenye mabango hayo wanatakiwa wachukue tahadhari mana wanatarajia waanze msako wa kuwasaka wanaohusika na matangazo hayo.

  Vilevile amesema kuwa waganga hao huwa hawachagui wateja wa kuwahudmia mana wao nia yao ni pesa hata watoto wadogo wanaofika sehemu hizo huwapa dawa hizo na kuharibu watoto.

  Amesema lengo la kuzuia mabango hayo ni kuboresha kizazi cha Tanzania na kupata maadili yaliyo mema ya kutohatarisha maisha ya watoto.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2263474&&Cat=1
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  A good start..
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,348
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Zinafanya kazi au ni biashara tu? I mean hizo dawa....
   
Loading...