Mabango ya CCM... Milions of US$

YoungCorporate

JF-Expert Member
Apr 30, 2010
391
113
Kampeni za mwaka huu zina mambo ....mabango mji mzima ........yaani nasikia yameagizwa canada kwa mamilion ya dola........kazi kwelikweli......hakuna hata moja la wapinzani...hapa kuna fair play kweli??
 
wapinzania hawana pesa za mabango !!!!!??? au wanabaniwa na wenyewe; wasije wakafirisiwa kwa kuzushuwa kisa wataonekana ni wapinzania; au makampuni yote yanamilikiwa na wana-ccm???!!
 
Ni sehemu ya matumizi ya fedha za kampeni zilizochangishwa, ni sahhihi kabisa.
 
Watu hatudanganyiki tena. Mabango yao wayaweke mpaka ******, lakini kura zetu kuipa CCM NO.

NCHI MOJA, NIA MOJA NA CHAMA KIMOJA = CHADEMA
 
Hii ni dhahiri kabisa kuwa masikini hawana chao katika nchi hii. Ukiangalia tu mabango ambayo yamewekwa sehemu mbalimbali kuwanadi wagombea wa CCM inaonyesha wazi kabisa kuwa matajiri wanazidi kuungana ili kuendelea kuwanyonya masikini. Gharama zilizotumika kutengeneza mabango na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kampeni vinagharimu fedha nyingi sana ambapo inaonyesha wazi kabisa kuwa huu ni umoja wa matajiri ambao wamewekeza kwa ajili ya kuvuna baada ya uchaguzi.
 
Tafadhali Kebepa usiseme ni umoja wa matajiri waliounganisha nguvu kuinadi ccm, hizo ni fedha zetu sisi walala hoi. Ni kodi zetu zinazotumika na wala hazitoki mbali ni mifukoni mwetu sisi.
 
mmh, possible! lakini, mbona asilimia kubwa ya wafadhili au hata wagombea wa CCM ni matajiri?
 
Na huo utajiri wameutoa wapi kama si kuufisadi umma wa watanzania kwa namna moja au nyingine?
 
Na huo utajiri wameutoa wapi kama si kuufisadi umma wa watanzania kwa namna moja au nyingine?

Hawa ni wale wanaoingiza mizigo bandarini na kukwepa kodi au kulipa kodi isiyo fanana na gharama halisi, wakiwaacha wafanyakazi na wakulima kufidia hilo gepu la kodi,,...Ni wale wanaongiza madawa ya kulevya na kuharibu vijana wa nch hii,,,,,Ni wale wanaoingiza Mitumba na vipodozi feki na kufanya soko la pamba na viwanda vyetu vy nguo kufa,,,,,Ni wale waoingiza vifaa feki vya kichina, achilia mbali madawa feki...Ni wale wanaowalipa waajiriwa wao ujira kiduchu huku wao wakinnemeka zaidi kwa kukwepa kodi....Ni wale waopata dili na zabuni ya miradi ya serikali wasiyo stahili baada ya kutoa kitu kidogo.,,,Ni pamoja na wachakachuaji wapetroli
Watu wote hawaatakuwa tayari kuona mfumo wa utawala ukibadilika kwa namna yoyote, ndio maana watatumia nguvu kubwa sana kuulinda, wamejaa ubinafsi na maumivi ya matendo yao ni kwa wananchi wa kawaida ambao aidha kwa makusudi au kwa kutokujua wanaendelea kuchagua wale wanaowanyonya
 
Mnanijaza hasira tu, maana siku hizi nimejikuta nikipiga campagin ya kutoipigia kura ccm utadhani nalipwa na chama chochote. Na nitaendelea kwa uhakika kabisa kumwambia kila nayeonana naye.
 
Mnanijaza hasira tu, maana siku hizi nimejikuta nikipiga campagin ya kutoipigia kura ccm utadhani nalipwa na chama chochote. Na nitaendelea kwa uhakika kabisa kumwambia kila nayeonana naye.

Kumbe tupe wengi...! Na wala si hasira ndugu Mess, hii ni hali ya kuwa mjasiri na responsible. Huwezi ukaona wapuuzi wachache wanaudanganya umma na kuna hatari ya umma kudanganyika na wewe uneujua ukweli ukakaa kimya, lazima utafanya kitu. Mimi na wewe ni mmojawapo wa hao tusioweza kukaa kimya. Tuungane tuwaonyeshe kuwa kwenda ikulu kunawezekana bila fedha (ambazo nyingi ni za kifisadi).
 
Watanzania wezangu- kufahamu ukweli na kukaa kimya ni dhambi; ebu tueleze ukweli kwa watu wengine hawa wanyonyaji waondoke - mabasi ya kasi yako wapi? tunaongozwa kwa Uongo
 
Hii ni dhahiri kabisa kuwa masikini hawana chao katika nchi hii. Ukiangalia tu mabango ambayo yamewekwa sehemu mbalimbali kuwanadi wagombea wa CCM inaonyesha wazi kabisa kuwa matajiri wanazidi kuungana ili kuendelea kuwanyonya masikini. Gharama zilizotumika kutengeneza mabango na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kampeni vinagharimu fedha nyingi sana ambapo inaonyesha wazi kabisa kuwa huu ni umoja wa matajiri ambao wamewekeza kwa ajili ya kuvuna baada ya uchaguzi.
kibaya zaidi ni kwamba tunaona picha zao badala ya picha za kazi zao

hatununui sura!!!
 
kibaya zaidi ni kwamba tunaona picha zao badala ya picha za kazi zao

hatununui sura!!!

Umeona eeehh....

mwambie na jirani yako sasa...........safari hii hatununui sura. Watu wanacheka cheka tu halafu watanzania wanakufa maskini, huduma mbovu, eti uwanja mkubwa wa ndege Bukoba, umeme wa kuaminika kijijini, wakati kila siku kwa Dar yenyewe umeme wa shida, barabara mbovu, uwanja wa ndege sio wa hadhi ya kimataifa....! Hivi hawa Chama Cha Mafisadi wanawaona watanzania kuwa wehu sio?
 
Mnanijaza hasira tu, maana siku hizi nimejikuta nikipiga campagin ya kutoipigia kura ccm utadhani nalipwa na chama chochote. Na nitaendelea kwa uhakika kabisa kumwambia kila nayeonana naye.

Kumbe tupe wengi...! Na wala si hasira ndugu Mess, hii ni hali ya kuwa mjasiri na responsible. Huwezi ukaona wapuuzi wachache wanaudanganya umma na kuna hatari ya umma kudanganyika na wewe uneujua ukweli ukakaa kimya, lazima utafanya kitu. Mimi na wewe ni mmojawapo wa hao tusioweza kukaa kimya. Tuungane tuwaonyeshe kuwa kwenda ikulu kunawezekana bila fedha (ambazo nyingi ni za kifisadi).

What a coincidence!
 
Wadau,

Hii dhana ya CCM ya kutumia resources zao nyingi kuweka mabango lukuki kunadi wagombea wao, hasa ya huyu mgombea wao wa urais ni nini?

Je wananchi hawamjui? Je hawajui utendaji wake wa kazi? Je hawajui uadilifu wake, Je hawajui anavyojali makundi yote katika jamii yakiwemo ya vilema, ma albino, watoto yatima, wafanyakazi, wakulima, mama wajawazito, vijana na wazee kama mabango yanavyomtangaza?

Mimi naona CCM kulikuwa hakuna haya kupoteza mamillioni kujaribu ku justify utendaji kazi wa mgombea wao bali wangeacha tu wanachi wamrate sababu wanamjua miaka 5 amekuwa akiwaongoza.

Na ndiyo maana mwaka 2005 sikushangaa hayo mabango sababu walikuwa wanamleta mgombea wao kwa mara ya kwanza, sasa hii mara ya pili naona kulikuwa hakuna haja kwani wananchi tayari wameshapima uwezo wake wa kiuongozi kwa kipindi hiki cha miaka mitano.

Kujaza Mabango kiasi cha kuwa KERO kwa wananchi wengine haibadilishi mtazamo wao juu ya rating waliyonayo kwa huyu mgombea.

Ni wazo tu kwa hawa wana CCM - haya mambango hayatabadilisha uamuzi wa wananchi juu ya PERFORMANCE RATING ya huyu mgombea.
 
Kuna bango Moja la Mwalimu J. K. Nyerere (Tumuenzi Mwalimu Nyerere ) lipo pale Boma karibu na Mwalimu house limedondoka chini kwa uchakavu wameshindwa kulirudishia, ila ya Mkuu wa kaya mpaka miti inakatwa ili yaonekane.
 
Back
Top Bottom