Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
*KWA HILI MABALOZI WAJITAFAKARI*.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za *Uingireza, Denmark, Ujerumani, Uholanzi, Italy, Sweden, Ubelgiji na Norway* nchini *Tanzania* wamejikuta wakiumbuka kwa kutuma ujumbe unafanana kwa maneno na sentensi wakihoji kufungiwa kwa gazeti la kiingereza la *The Citizen*.
Inawezekana walifanya hivi kwa makusudi na inawezekana kabisa kuwa kuna mpango mahususi nyuma yake, lakini hii haiondoi ukweli kuwa kitendo hicho kimewaumbua na kuwapaka taswira yenye mashaka kuwa hawakuwa na dhamira njema.
Gazeti hilo limefungiwa na Idara ya Habari, Maelezo kwa siku saba kuanzia tarehe 28.02.2019 baada ya *kutenda kosa la kuchapisha taarifa zisizo rasmi za kushuka kwa thamani ya shilingi na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani*.
Kwa wasiojua, *utaratibu wa kidiplomasia unawataka Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wanapokuwa na jambo ambalo wanaliona lina ukakasi wawasiliane na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi husika ambayo ndio mlezi na msimamizi wao*.
Ilitarajiwa kuwa kama walikwazwa na gazeti la *The Citizen* kufungiwa, wangeuliza wizarani kumetokea nini na bila shaka wangepewa majibu ya Serikali.
Na hili ni jambo la kawaida kabisa, hata Mabalozi wa Tanzania waliopo katika nchi zao wanafanya hivyohivyo. Na lengo kuu ni kujiepusha kuingilia mambo ya ndani ya nchi husika.
Aidha, kupata ufafanuzi wa Serikali pia kuna epusha Mabalozi kujikuta wanatoa kauli, kwa jambo ambalo linafanywa kwa mujibu wa sheria. *Tanzania ni nchi huru, haipaswi kuingiliwa katika uendeshaji, usimamizi wa sheria na upangaji wa mambo yake*.
Kwa jambo hili Mabalozi wamenaswa katika mtego wa kukiuka msingi huo, wametanguliza mbele maslahi yao na mazoea yao ya kusoma gazeti la *The Citizen* kila asubuhi. Wamejikuta wakihoji jambo ambalo ni utekelezaji wa kawaida wa majukumu ya Serikali.
Na kana kwamba hiyo haitoshi, imedhihirisha wazi kuwa Mabalozi hao wa nchi 8 waliketi pamoja na kujadiliana ujumbe watakaoandika na inaonekana wazi kuwa waliandika na kusambaziana ili wauweke kwenye akaunti zao za *Twitter*.
Ujumbe unaofanana ni huu;
*Today haf to change our morning routine: usually we start the day with a fresh copy of the #citizen. Unfortunately it has been banned in #Tanzania for a week. Is this sanction proportionate to the offence purportedly commited?*
*#PressFreedom #TheCitizenBanned #DefendMediaFreedom*
Inawezekana katika mpango huu Mabalozi walishirikiana na gazeti la *The Citizen*, hii inaleta mashaka kuwa kumbe gazeti la *The Citizen* hutumika na Mabalozi wa baadhi ya nchi kutekeleza matakwa yao kwa sababu yamekuwepo mengine mengi ambayo gazeti hili huchapisha kwa kuonesha dhahiri kuwa linalinda maslahi ya nchi fulani fulani, na kutojali maslahi ya Tanzania.
Vyote kwa vyote, naipongeza Serikali kwa kuchukua hatua dhidi ya gazeti la *The Citizen*, naamini Serikali itatupia jicho pia kwa gazeti la *Mwananchi, Nipashe na Mtanzania* ambayo yameonesha dhihiri kuwa na mwelekeo wenye kuidhohofisha Serikali ya Tanzania ambayo kwa sasa sio siri imeamua kusimamia maslahi ya Tanzania ambayo kwa muda mrefu yamechezewa.
Nampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri ambapo amemuondoa Balozi Mahiga na kumweka Prof. Kabudi.
Nimefurahishwa sana na kauli ya kwanza ya Prof. Kabudi ambapo ameweka msimamo wake mapema wa kutotaka kuona nchi inabagazwa na kuchafuliwa. Na yeye kama mwanadiplomasia namba mbili na msimamizi wa sura ya nchi kimataifa ana wajibu wa kutoruhusu nchi kuchezewa.
Ni bahati mbaya sana Mzee wangu Balozi Mahiga hakuonesha msimamo katika jambo hili pamoja na sifa yake kubwa katika diplomasia ya kimataifa. Ndio maana nchi ilikuwa inachezewa sharubu na Mabalozi wakawa wanajisahau na kuvunja taratibu bila kujali athari wanazosababisha kwa Tanzania kimataifa.
Kwa wasiojua kitendo walichokifanya Mabalozi hawa 8 cha kuandika ujumbe unaofanana na kuuweka hadharani kupitia akaunti zao za *Twitter* ilitosha kabisa kwa Waziri kuwabana hadharani ili waombe radhi na waahidi kutorudia. Katika nchi nyingine ingeweza hata kufikia hatua ya Waziri wa Mambo ya Nje kuibua hoja kwenye Serikali za nchi zao ili wabanwe na waonywe. Mahali pengine ingeweza hata kufikia hatua ya kuzitaka nchi hizo ziwarudishe Mabalozi wao.
Gazeti la *The Citizen* lilifanya makosa ya kuchapisha habari zenye takwimu ambazo sio rasmi, zilizoonesha kuwa thamani ya shilingi imeanguka sana. Lilichapisha habari hiyo ikiwa na dosari zifuatazo;
*Kwanza halikuchukua wala halikushughulika kuonesha viwango vya kubadilisha fedha vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa siku hiyo. Na hapa ieleweke vizuri kuwa kuna wakati viwango vya kubadilisha fedha hupandishwa kwa njama za wafanyabiashara bila sababu za msingi ama kuzidisha viwango ilimradi wapate faida zaidi*.
*Pili, gazeti hili halikuonesha kuwa sio shilingi pekee yake iliyoanguka kwa wakati huo, zipo fedha nyingine ambazo pia zilianguka zaidi ya shilingi. Na yapo maelezo kuwa katika siku za Karibuni Dola ya Marekani imeimarika sana. Lakini The Citizen sio tu halikuchukua takwimu rasmi bali lilichochea zaidi kwa kuandika viwango vya juu zaidi hali iliyowaogofya wageni na wananchi*.
Madhara ya gazeti hili la *The Citizen* ni makubwa kwa uchumi kwa sababu unapoonesha fedha ya nchi imeanguka ujumbe unaoupeleka kwa jumuiya ya Kimataifa ya wawekezaji ni kuwa Tanzania sio mahali salama pa uwekezaji.
Pili kwa kufanya hivyo ni kutaka kuonesha kuwa hali ya Tanzania ni mbaya kiuchumi.
Mkurugenzi wa Maelezo alieleza vizuri kuwa adhabu iliyotolewa kwa gazeti la *The Citizen* imefuata utaratibu wa sheria ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016 ambayo inaeleza kuwa adhabu ya kufungiwa itafikiwa baada ya chombo husika kuonywa mara tatu. *The Citizen* ilionywa mara tatu. Lilifikia hatua ya kufungiwa.
Mwisho naomba kuwasihi waandishi wa habari wa Tanzania waache kutumika, natambua kuwa wakati mwingine wanashinikizwa na wamiliki wenye nia mbaya dhidi ya Serikali na Tanzania. Hao dawa yao ni mkono wa sheria.
Watanzania tuendelee kupigania nchi yetu tuunge mkono juhudi za Rais na Serikali, uzuri ni kuwa Rais alishatuambia kuwa ameamua kupigania maslahi ya Tanzania. Hii ni vita ya uchumi na katika vita hii watu waliokuwa wakinufaika hawatapenda na watatupiga vita kila upande.
Na sasa tunaona wapo wanaojaribu kuwatumia wanasiasa, wapo wanaotumia vyombo vya habari, wapo wanaotumia kumuiya ya kimataifa na wapo wanaojaribu kuchochea chuki kati ya Serikali na wananchi. Muhimu ni kusimama kidete.
Nawatakia Kwaresma Njema.
Amb. Joseph G.P
Balozi Mstaafu
Dar es Salaam.
Sent using Jamii Forums mobile app