Mabalozi wajuta kuwakilisha Tanzania nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabalozi wajuta kuwakilisha Tanzania nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 11, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inatuhumiwa kuwatelekeza mabalozi wake wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na kuwakumbatia mabalozi wa heshima.

  Taarifa kutoka kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Ushirikiano wa Kimataifa iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni pamoja taarifa zingine kutoka kwa baadhi wa wajumbe kamati hiyo, zinasema upendeleo huo umesababisha mabalozi wengi watamani kurudi nchini baada ya maisha yao kuwa magumu.

  Chanzo cha habari kilidai kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo waliofanya ziara katika balozi mbalimbali nje ya nchi walishuhudia kuwepo kwa hali mbaya ya ofisi za balozi.

  Chanzo hicho kimeleza mabalozi wengi hawathaminiwi kiasi ambacho hata maafisa mbalimbali waanapokwenda kwenye nchi hizo kwa ajili ya shughuli za kiserikali hawamshirikishi balozi husika.

  “Imekuwa kawaida kwa maafisa wa serikali wakienda kwenye nchi hizo, hawatoi taarifa kwa Balozi kitu ambacho kinaawaauma sana wawakilishi wetu,” kilisema chanzo hicho.

  Hata kwenye taarifa ya kamati hiyo iliweka wazi kwamba kuna tabia ya maafisa wa serikali wanaokwenda kama timu ya kitaalamu kutoshirikisha balozi zetu, hivyo uwepo wao hakuna anayejua.

  Katika kitu ambacho kimewafanya mabalozi hao kukata tamaa, ni kufuatia mabalozi wa heshima wanavyonyenyekewa, inafikia wakati balozi huyo anajulishwa kila hatua endapo Rais anatembelea moja ya nchi hizo wakati balozi husika hana habari.

  Wakitolea mfano, balozi wa heshima wa Uholanzi amepewa madaraka ya kumpokea Rais mara anapotembelea nchi hiyo au kupita, wakati Balozi mwenye makazi yake nchini Ugiriki hana taarifa zozote.

  “Ni jambo linalosababisha balozi zetu kukosa hamu tena ya kuendelea na kazi, ikiwa balozi wa heshima anapewa taarifa zote huku balozi husika hajui, kitu hiki tulipoelezwa tulishangaa sana,” chanzo hicho kilisema.

  Aidha, kutokana na kupewa madaraka makubwa, balozi huyo hivi sasa anashinikiza jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuuzwa, kitu ambacho ni hatari kwa maslahi ya nchi.

  Taarifa ya Kamati hiyo inaeleza kwamba kwa ujumla majengo ya ofisi za mabalozi yamekuwa katika hali mbaya na kunatakiwa juhudi kubwa za kuzifanyia ukarabati mkubwa ili kuongeaa hadi ya nchi.

  Ufumbuzi wa tatizo hilo sio kuuza majengo hayo kama inavyoshauri na baalozi huyo ili kukwepa kuwepo na maslahi binafsi ya kibiashara.

  Kamati iliishauri serikali iwe na utaratibu maalumu wa kuwalipa mishahara na posho zingine kwa mabalozi pamoja na watumishi wa ubalozi katika kipindi kifupi.

  Ilisema hivi sasa inawachukua muda wa mwaka mmoja kupewa pesa au kupata majibu kwa suala la kikazi, kitu kinachosababisha wawe na maisha magumu.

  Wakati akifunga majadiliano ya Bajeti ya Wizara yake, Waziri Membe alisema utaratibu wa kuwatumia mabalozi wa heshima unaweza kuangaliwa, lakini uwepo wao kuna manufaa makubwa katika Taifa.

  Alisema Wizara pia itaboresha njia za mawasiliano kwa balozi za Tanzania nje ya nchi ili kuongeza tija ya utendaji wa kazi.

  Hata hivyo Membe alisema kuchelewa kwa mishahara na pesa za kugharamia majengo inasababishwa na Wizara hiyo kupatiwa fungu dogo la fedha lisilokidhi matumizi.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jambo moja ninaloshangaa balozi wamemweka wa nini katika nchi au ukanda husika wakati serikali haimtambui wala kumtumia na badala yake kumtumia balozi wa heshima tu, basi wamweke huyo wa heshima badala ya viinimacho vinavyoendelea.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sikujua pia kuwa tuna balozi Ugiriki.
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Majungu kwa membe tu je ni kwanini wasiongee wenyewe mpaka kamati isafiri!
   
 5. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  hapo sasa! mi naona hii stori imechanganya
  ukweli na fitna.
   
 6. D

  Dopodopo Kadopo Senior Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Viapo wanavyo apa huwa vinahusu nini? utendaji wa viongozi wa wizara katika hili lazima utiliwe qn mark.
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  duh! Unless wamechanganya habari..siyo Ubelgiji kweli?!!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii itakuwa lile gazeti la udaku linaloitwa Tanzania Daima, kama kawaida yake.
   
 9. a

  andrews JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  udaku unaozidi uhuru na mzalendo itakuwa wale madada wa sinza tu
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tumuulize Candid Scope. Angalia usije ukaumbuliwa bure na chuki zako dhidi ya Tanzania Daima. Picha inaonyesha ni IPP media.
  Lini Tanzania Daima likawa IPP media?
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Ni jitihada za mafisadi kumchafua mhe Membe maana wanajua he is the cleanest of leaders.
  Mti wenye matunda ndio upigwao mawe.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe unaongelea picha iliyowekwa? zuga hiyo!
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Tunao Ubalozi hadi Nepal we unashangaa Ugiriki?!
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mabalozi siku hizi hawana umuhimu sana.
  Mataifa mengi hutumia PR companies (lobbysts) ambazo zipo nyingi tu States, Euro, Asia .... unawalipa fedha, unapata access. Mabalozi huwa hawapati access congress au white house bila kutumia lobbysts, kwa hiyo kwanini serikali isiende straight to lobbysts?
  The era of ambassadors is almost gone. Let it go!!!
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Wote warudi nyumbani hawana kazi ya maana wanayoganya huko.tubakize balozi zimbabwe na syria
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Sasa badala ya kutesea kwenye misitu ya pande mmebadilishia kwenye balozi
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  lakini kiukweli balozi zetu zinatia aibu sana niliingia beiljing china huwezi amini kama ni ubalozi wetu yaani ni aibu sana. yaani mpaka nyasi mlangoni sijui wameshindwa hata kuajili mtu wa kufanya usafi kwa mazigira ya nje. balozi zetu ndio nchi nchi yetu tukiwa ughaibuni ila ukweli huwezi amini kama ni balozi za tanzania ninayotoka au la!
   
 18. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kma kweli hali imefikia huko si wakatalie teuzi zao,hakuna kitu kama hicho hela inatosha sema tu ni kwa kuwa mabalozi wengi walikuwa watumishi wa serikali na walikuwa wameshazoea 10% sasa wakishakuwa mabalozi wamezikosa kutokana na sheria za nchi walizomo sasa wanapiga kelele.Ntaamini nikiskia kuna balozi amejiuzulu kwa kuwa maisha ni magumu
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  ...Juzi juzi ubalozi wetu wa Russia dari lilianguka hiyo ndio aibu ya mwaka...Balozi kakoswa koswa kuangukiwa na dari.
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  unavomsifia membe.................how far r u sure kuwa yeye ni msafi???NENDA MTAMA
   
Loading...