Mabalozi wa nyumba 10 ndio chanzo cha ubakaji wa Demokrasia Tanzania


Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
2,468
Likes
374
Points
180
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
2,468 374 180
Mabalozi wa nyumba wamekuwa wakitumika kwenye kila uchaguzi kukisidia chama cha Magamba kuiba kura au kuwatisha wapiga kura hasa wanaonekana kuwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani. Hii tabia inahitaji kukomeshwa haraka sana, hawa mabalozi ndio chanzo cha ubakaji wa demokrasia nchini Tanzania. Wanatumiwa au wanatumika kuiba kura, kulazimisha wananchi kuwapigia kura Magamba, kutoa taarifa kwa Magamba kuwa watu au mtu fulani asiandikwe kwenye daftari la upigaji kura kwa kushirikiana na kitengo kidogo cha Magamba wasimamizi wa chaguzi (NEC), kuwauwa wapiga kura wangali hai na vituko, kuiba au kununua vitambulisho vya wapiga kura na vituko vingi vya kubaka Demokrasia kama wanavyotumwa na CCM. Hii tabia Vyama vya upinzani wanatakiwa kuikomesha haraka iwezokanavyo kwa sababu ndio ccm wanaowatumia mabalozi wa nyumba 10-10 kufichia kura zao za wizi pamoja na kutumia ofisi za Serikali hasa za ma-DC. Mabalozi wa Nyumba kumi kazi zao ni kutumikia Jamii (Community) ya kitongoji alichochaguliwa na wakazi wa hayo maeneo au mtaa sio Chama, Tabia hii ikomeshwe na wapewe darasa

Watanzania wenzangu tuanzeni na Mabalozi kuwatolea Macho na sio Kila balozi atumikie chama.
 

Forum statistics

Threads 1,213,565
Members 462,207
Posts 28,482,498