Mabalozi wa CCM na Vitambulisho vya Uraia: Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabalozi wa CCM na Vitambulisho vya Uraia: Hii imekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Amiliki, Aug 3, 2012.

 1. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wakati najaza fomu ya kuniwezesha kuja kupata Kitambulisho cha Uraia, niliona Watu wawili wakija pale bila ya kuwa na Viambatanisho vilivyoorodheshwa kwenye fomu, lakini wakiwa na barua za Mabalozi wao wa Nyumba kumikumi ambao ni waajiriwa wa CCM (Na si kutoka kwa Watendaji wa kata ambao wanatambulika Kiserikali).

  Je hawa Mabalozi wa nyumba kumi kumi wa CCM bado wanatambulika Kisheria na kwenye shughuli nyingine za kiserikali kama Mahakamani pia? Maana nimeambiwa kuwa huwa wanatoa pia barua za kudhamini mtuhumiwa mahakamani na zinakubalika.

  Hivi kama wanafanya pia kazi za kiserikali, ni nani anawalipa? Je CUF na CDM viongozi wao wa huko mitaani wana nguvu hizo hizo pia, yaani wanaweza kutoa barua za Udhamini na zikakubalika?
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nadhani itakuwa nzuri sana kama hii ikafanyika practically, nikimaanisha kuwa mtu mmoja achukue muda wake aende akatafute barua kutoka kwa balozi wa nyumba kumi kumi kutoka CUF au CDM then atie mguu kutaka kitambulisho. Matokeo nadhani 60% wanaweza kukataa. Vipi hiyo barua ilikuwa inatoka kwa balozi kweli au M/kiti wa mtaa/kitongoji?
  NB: Kama mtaa fulani una balozi wa nyumba kumi kutoka CCM ni lazima pia wawepo wa CDM na CUF au vyama vingine au navyo vinashindaniwa? Kama kila chama kinalazimika kuweka balozi wake basi ni makanjanja bado mfumo wa chama kimoja unatutafuna.
   
 3. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu Barua zinazokunaliwa ni za kiongozi wa serikali za mitaa, hao wajumbe wanamwandikia barua mwenyekiti wa serikali za mitaa kuwa hawa watu ni wakazi wa shina langu then mWenyekiti anaiandikia NIDA, nimefuata hii process kwenye mtaa wangu..
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Hapo kwenye bolded black unamaanisha mabalozi si ndiyo; kama nii Ndiyo je hao wajumbe ni kutoka chama chochote au ni lazima awe kutoka CCM tu? Na kwenye bolded red nako unamaanisha M/kiti wa kitongoji/Mtaa.
   
 5. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi mwenyewe nimeshuhudia mtu akija na barua ya Balozi wa CCM wa Mtaa watu ambaye ninamfahamu na si ya Mwenyekiti wa Mtaa. Kwa hiyo ninazungumza kitu ninachokijua.
   
 6. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160

  hiyo barua ilikublika ya kutoka kwa mjumbe wa nyumba 10? hapa nadhani ni makosa kuwatumia hawa wajumbe wa myumba 10 kisheria wanatambuliwa na sheria ipi ya nchi? tatizo letu watanzania tunaishi kimazoea tunaishi kama tuko enzi za chama kimoja ambapo kila mwaananchi alikuwa mwanachama wa ccm, tubadilike viongozi wanaotambulika ni wenyeviti wa mitaa/vitongoji.
   
 7. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  NIDA kwa ujumla hawakujipanga...Bora wangekuja na Affidavit..Kiapo cha mahakama kama hauna kitambulisho chochote
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kuna thread nyingine humu inazungumzia suala hili hili. Mimi nilikataliwa kuandikishwa nikidaiwa lazima niwe na barua ya balozi wa CCM. Nilijaribu kumwambia yule dada kwamba kwanini atake barua ya balozi na sio barua kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa, lakini alisisitiza kwamba anataka barua ya balozi. Kwa kuwa mabalozi hawalipwi mishahara, wanalazimisha kwa kila barua wanayoandika walipwe Tshs. 2,000

  Huu ni uhuni uliopitiliza!!!!

  Tiba
   
 9. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa mabalozi wanatumika kwa sababu ndiyo wanawajua wkazi wao hapo mtaani tofauti na m/kiti wa Serikali ya mtaa ambao una maelfu ya watu ambao ni ngumu kuwatambua.Japo hawa watu hawapo kisheria ingekuwa wakati mwafaka kuwaweka kisheria ili watambulike kwa vyama vyao kwa kupigiwa kura na watu wote.
   
 10. G

  GWAMWAJA Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 11. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Kimsingi hao hawatambuliki na si viongozi halali. Mimi nimeshagombana nao sana na hadi tukapelekana mahakamani na nikawashinda.Katiba haiwatambui hao.

  Tatizo linakuja kuwa viongozi wengi wa serikali wanawaogopa sana hawa jamaa kana kwamba ni viongozi.

  Wanaiogopa CCM. Mimi siwaogopi na hata wanapojifanya kupita majumbani kuleta mambo yao huwa nawaambia sitofanya kwani nyie ni watu wa ccm na mimi si mwanachama wenu.Elimu ya uraia wengi hawana.

  Bado wapo enzi za "viongozi wa chama na serikali". Wagomee hao wakija kwako na wakitaka kwenda mahakamani waambie wakimbie badala ya kutembea ili wafike haraka mahakamani. Watanzania tuna woga sana na ccm.
   
 12. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Unachokisema si sahihi.Hao ni mawakala wa ccm. Kwanza leo hii hakuna tena nyumba kumi kumi.Mwenyekiti serikali za mitaa anawajua kwani zipo kamati ndogo ndogo ambazo wengi wao wanaishi hapo hapo mtaani.Hawafai hao jamaa.Tambueni kwa sasa kuwa hatutawaliwi tena na mabalozi kama ilivyokuwa enzi za chama kimoja. Ukitaka mabalozi wapitishwe basi vyama vyote viwe vimeingizwa katika utaratibu huo.
   
Loading...