Mabalozi wa CCM Igunga wataka kujivua gamba; Wadai rushwa ilitumika

Hao mabalozi ndo wamegundua hilo,c walifurahia kuchukua kadi za watu,hapo magamba Nape na mukama cjui watasemaje!shame on u Magamba
 
mabalozi 18 wa ccm wa igunga wamejivua gamba.wamesema ccm imeshinda kwa sababu walikuwa wanatoa rushwa na ushahidi upo na wanaeleza pia jinsi m/kiti wao alivyokua anasambaza 45mil.wasema ijumaa ijayo watatangaza wanaenda chama gani.
wakati huo huo aliyekua mgombea wa ubunge kupitia cuf kasema hatagombea tena kwa sababu hana hela.anasema angekua na hela angeshinda.anasema kura zake 9000 zimenunuliwa na ccm.
source;ABDALLAH RAMADHAN WA WAPO RADIO
MY TAKE;
hela za rushwa zinaisambalatisha ccm.mia

Wakuu mimi bado siamini,hebu ngoja tupate taarifa kutoka vyanzo makini zaidi,hizi WAPO nk mh!! naogopa kushangilia....
 
Hao uliwataja walikuwa wapi na wao si ndo CCM C,D na E washafunga ndoa nao

Hawa ndio wale ambao walikosa mgao au walipata mgao mdogo naona wameamua kumwaga mboga! Nadhani safari bado ni ndefu sana na hakika tutasikia mengi mwaka huu huu kabla ya december
 
Aisee kabla sijanunu chupa ya mvinyo niinywe kwa furaha naomba nipe source ya hii taarifa!
 
Hilo ni bomu moja tu bado la kukiuka sheria (Iliyosainiwa kwa mbwembwe na M.kwere) ya gharama za Uchaguzi, ambapo kwa jimbo la Igunga ilitakiwa isizidi Milioni 800, CCM wametumia Bilion 3! CCM Yatagonga Chup*** mwaka huu.
 
waache wajivue magamba kama ukweli wameshaujua madudu ya ccm wana haki ,my take kuwa chadema wawe makini hawa watu wasijejifanya wanajiunga chadema kumbe wana lao jambo kuja kuharibu chama kama mheshimiwa zizu, ccm b,
 
Yameanza kuvuja sasa ndoo imeshatoboka,CCM ni wezi na wadhurumaji wakubwa.
 
hao walipunjwa mgao au walinyimwa kabisa ila tusubiri tutasikia mengi sana hao ni mabalozi tu
 
Aisee kabla sijanunu chupa ya mvinyo niinywe kwa furaha naomba nipe source ya hii taarifa!

Jimbo limeisha enda hilo acheni kujiliwaza , wenzenu sasa hv wanazunguka nchi nzima kusherekea ushindi, nyie mwategemea ushindi wa mezani ambao haupo . Umeingia kwenye game umeshindwa jipange. Njoo mie nikununulie huo mvinyo
 
hao walipunjwa mgao au walinyimwa kabisa ila tusubiri tutasikia mengi sana hao ni mabalozi tu

It seems walipunjwa maana wanadai kulikua na laki tano na watu walikua 48 Sasa nadhani kuna mahali wengine walipata donge nono zaidi yao ndio chanzo cha tatizo
 
HAWA WATAKUWA HAWAJAPEWA MGAO WA MWISHO BAADA YA KUSHINDA, NCHEMBA KAKIMBIA NA CHOA KAWAACHIA MANYOYA.....sasa wanaamua kumwaga ugali na mboga! walale njaa wote
 
Unaweza kuona jinsi gani inchi yetu ilivyokosa uzalendo kuanzia magogoni hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi. Unadhani tutaweza kuurudisha uzalendo kwa kuendelea kujipendekeza kwa hawa wazee wetu wa CCM! Tusahau.

Ni kuamua liwalo na liwe, 2015 ni mbali sana ila kwa vile wengi wetu bado tunaona shida tulizo nazo hazijasababishwa na serikali yetu, basi ngoja tuendelee kuelemishana kwanza.
 
Hao mabalozi wanasumbuliwa na njaa. Kama walidhani fedha waliyopewa itakuwa ya kudumu wamekwisha kabisa. Hawa ndio waliolia Rostam alivyotoka. Waende waendako hata SAU waende tu.
 
Laki 5 kwa watu 48 kila mtu anapata 10416,tuseme buku 10 kamili kila kichwa kilikula.hawa ndio magamba.na bado mpaka hapo mbongo atakaposhtuka anauza haki yake itakuawa too late.cdm ina kaz ya ziada kuelimisha umma juu ya hili,elimu ya uraia ni muhimu saaana kwa sasa.
 
Back
Top Bottom