Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapigakura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapigakura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 18 September 2011 20:35

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]WABUNGE WA CHADEMA WAHAMISHIWA MJINI TABORA

  Geofrey Nyangoro na Boniface Meena, Igunga

  WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo a Igunga likiendelea kupanda, Chama cha Wananchi (CUF) kimekituhumu CCM kuwa kimeanza kukusanya na kuorodhesha kadi za wapiga kura na kwamba, kimemkamata mmoja wa mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wakati akifanya kazi hiyo.Tuhuma hizo dhidi ya CCM zilitolewa jana na mgombea wa CUF, Leopold Mahona, ambazo tayari zimeshapingwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba.

  Akiwa katika kijiji cha Imalilo, Kata ya Nguru, jimboni humo, Mahona alisema kazi kuorodhesha majina ya wapiga kura na kadi zao inaratibiwa na kusimamiwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM.

  Mahona aliwataka wakazi wa kijiji hicho kukataa mpango huo kwa kutotoa vitambulisho vyao vya kupigia kura, kwani wakikubali kufanya hivyo watashindwa kuchagua mwakilishi mwenye uwezo wa kuwasaidia.

  Kauli ya Mahona imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kuwataka wakazi Igunga kujiandaa kukabiliana na hujuma zinazotarajiwa kufanywa na CCM kwa lengo la kulazimisha ushindi, kutokana na chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi.

  "Wakija kuwaomba shahada kataeni, hata wakiwatisha msikubali, mkae kimya na msiwafanye chochote. Subirini siku ya kupiga kura na mnichague mimi nikaletee maendeleo,'' alisema Mahona.

  Mahona alidai kuwa, wajumbe hao wanawatisha wakazi wa jimbo hilo wanaounga mkono upinzani na kulaani kuwa, kitendo hicho kinakwamisha maendeleo na juhudi za mabadiliko ya kidemokrasia.

  Hujuma sehemu mbalimbali
  Wakati mgombea huyo wa CUF akilalamikia kitendo hicho, mwandishi wa habari hizi imeshuhudia tukio la uandikishaji kadi hizo ukiendelea katika maeneo mbalimbali.

  Mwandishi alishuhudia kijana mmoja, mkazi wa kata ya Iborogero, nje kidogo ya mji wa Igunga akiorodhesha majina ya wenye vitambulisho vya mpiga kura pamoja na namba za vitambulisho vyao vya mpigakura.

  Kijana huyo alipoulizwa na Mwananchi, huku akisita kutaja jina lake, alisema kazi hiyo amepewa na wakubwa wake ambao alikataa kuwataja na kusisitiza kuwa, anachofanya ni kuorodhesha majina ya wapiga kura na vitambulisho vyao kupigia kura kisha kuviwasilisha kwa wakubwa.

  ''Mimi kazi yangu kukusanya taarifa za watu wenye vitambulisho vya mpigakura. Ninaandika majina yao pamoja na namba ya kitambulisho nawasilisha kwa wakubwa, wao watatoa maelekezo na hatua za kuchukua,'' alisema kijana huyo.

  Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuwa, kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.

  Kadi hiyo ambayo mwananchi iliona kumbukumbu zake Ikiwa na namba 05262605 inaonyesha kuwa, ‘Chritina Kaloli alijiandikisha kuwa mpiga kura Desemba 26, 2004 katika Shule ya Msingi Mpogoro, Wilaya ya Igunga'.

  CCM wakanusha
  Mratibu wa kampeni wa CCM, Nchemba alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alisema ni kitu kisichoweza kufanywa na CCM.

  "Hivyo vyama vingine vinatapatapa, sisi ndio wenye wanachama wengi Igunga, tukifanya hivyo tutakuwa tunapunguza wapiga kura wetu, hatuwezi kufanya hivyo bali wao,'' alisema.

  Alisema kitambulisho ni mali ya mwenye nacho na kwa mujibu wa sheria za nchi, hakuna mtu anayeruhusiwa kuchukua kitambulisho cha mtu mwingine.

  Nchemba alisisitiza kuwa, suala la kukusanya vitambulisho vya wapiga kura linaweza kufanywa na vyama vingine visivyo katika jimbo hilo kikiwamo CUF kwa lengo la kupunguza wapiga kura.

  Kafumu alipuliwa
  Katika hatua nyingine, Mahona alimrushia kombora mgombea Ubunge kupitia CCM, Dk Dalaly Kafumu akidai alihusika katika mpango wa kuwahamisha wakazi wa kijiji cha Ihomelo chenye utajiri wa madini.

  Alisema lengo la mpango huo uliobuniwa na Serikali ulikuwa kuwaondoa wakazi wote wa kijiji hicho kwa kuwalipa fidia ya Sh500,000 na kutoa eneo hilo kwa mwekezaji ili aweze kuchimba madini ya dhahabu.

  Wabunge Chadema wapelekwa Tabora
  Katika tukio lingine. wabunge wa Chadema wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa, jana wamehamishiwa Tabora mjini kwa ajili ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi leo, kujibu mashtaka ya shambulio la aibu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.

  Wabunge hao, Susan Kimwanga (Viti Maalumu) na Sylvester Kasulubai (Maswa Mashariki) ambao Ijumaa walihojiwa na polisi na kuachiwa huru, walikamatwa juzi walipoenda kituo cha polisi kuripoti na kutupwa korokoroni hadi leo watakapofikishwa mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema hicho, Tundu Lissu alilaani kitendo hicho cha polisi kuwapeleka Tabora wakati wanajua kuwa, mahakama ya Wilaya ya Igunga ina uwezo wa kusikiliza mashtaka ya wabunge hao.

  Lissu alisema kuwa, atakuwepo katika Mahakama ya Tabora kuwatetea wabunge hao ambao anaamini kuwa hawakutenda kosa lolote na wana haki ya kufanya hivyo kwa kuwa Sheria inatambua hilo.

  "Kama polisi wanadhani kuwa wanaweza kuitetea CCM, wajifunze kwa wenzao Kenya walivyoshindwa kuitetea Serikali. Jana polisi walijawa hofu baada ya kusikia nipo hapa na wamewapeleka Tabora Mjini ili wasipate msaada wa kisheria hapa Igunga," alisema Lissu na kuongeza:

  "Kesho (leo) nitakuwepo Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na nitahakikisha wanatoka."

  Alisema kuwa kinachotokea kwa viongozi wa chama hicho si jambo geni kwa watetea ukombozi wa nchi, kwani hata Julius Nyerere na Bhoke Munanka walionja joto ya jiwe kwa dola ya kikoloni wakati wakitafuta ukombozi.

  "Ningependa Mkuu wa Wilaya afike mahakamani ili aeleze jinsi alivyovuliwa nguo katika tukio hilo," alisema Lissu.

  Alisema kuwa walichokifanya wabunge hao walikuwa na mamlaka ya kisheria kukamata mhalifu kama wahalifu wengine wowote kwa sababu polisi hawakuwepo.

  "DC alikuwa kwenye eneo ambalo Chadema walipaswa kuwepo, huo ulikuwa ni uhalifu, ndiyo maana raia walitumia nguvu zao kumkamata," alisisitiza Lissu.

  Uthibitisho wa polisi
  Akizungumzia tukio suala hilo, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Tathimini (Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai), Naibu Kamishna wa Polisi, Issaya Mungulu, alisema kuwa ni kweli waliwahamisha wabunge hao jana kuwapeleka Tabora.

  Alisema kuwa wamewahamisha kwa sababu za kiusalama na kwa kuwa mjini hapa siyo mahali panapofaa kushughulikia suala hilo.

  "Ni sehemu ya utaratibu wa polisi, itatumika mahakama ya hakimu mkazi pale Tabora," alisema.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. R

  RMA JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 410
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"].[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]:mvutaji: Hivi huyo Mwiguru Njemba pamoja na kushikwa ugoni bado hajawa na aibu tu!
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yeah si Mkuu wa Wilaya alikuwa na Mkutano na hao Wajumba wa Nyumba kumi kumi na Mabalozi? na Ajenda yao ya nne ni Uchaguzi

  CCM knows how to steal elections... na Watajiita Waungwana kweli...
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,742
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mimi mwaka 2000 nikiishi Msasani nilifatwa na mjumbe wa mtaa akataka nimwonyeshe kadi yangu ya kupiga kura na akiiorodhesha atanipa elfu 10 nikamfukuza,kwahiyo janja hiyo ipo na walioorodheshwa wote siku ya kupiga kura jina lako halionekani.
   
 5. M

  MCHARA Senior Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ccm wamefikia mwisho wa kufikiri ndo mana wana2mia masaburi kuhakikisha wanashinda! Ktk uharifu hakuna cha dc wala nani na washukuru wana cdm ni wastaarabu sana vinginevo wangempa dc kipigo cha mbwa mwizi!
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 6,369
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  <br />Hili zoezi la kununua shahada wamelianza kwa kasi mno wanaitisha mikutano ya mitaa na kuorodhesha majina ya watu kisha kumpitia mmoja mmoja na kumshawishi awauzie shahada. Mfano jana juma pili mtaa wa stoo mwenyekiti Abdala Mikingamo na mabalozi wake walifanya hujuma izo baada ya kuitisha mkuutano wa wanawake wa mtaa huo mkutano ulifanyika eneo la bomba la maji. Mikingamo ni kichomi waandishi tunaomba ahojiwe juu ya habari hii wakati juhudi
  za kumnasa zikiendelea. Ova! <br />
   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 6,369
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa wilaya naye alikuwa akiratibu zoezi la ununuzi wa shahada. Ova!
   
 8. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,742
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nyie mnafikiri wale milioni 10 waliojiandikisha 2010 na hawajapiga kura mambo ni haya haya,wajinga wanauza kabisa, wakorofi na wanaohisiwa upinzani namba yao hazionekani siku ya kupiga kura.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  CCM hawaonagi aibu!
   
 10. O

  Ochutz JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  This tym kitaeleweka tu
   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,232
  Likes Received: 1,100
  Trophy Points: 280
  Tulijadili jambo hili mwaka jana katika Uchaguzi mkuu.
  Kuna walioona ya kuwa halikuwa tatizo as long as kadi ya kupigia kura mtu anabaki nayo na kuna walioona ni kosa.
  Kwa bahati mbaya watu wa NEC hawakupenda kulitolea ufafanuzi kwani lillihusu zaidi Chama tawala.
  Haya ni mambo ambayo tunayaona madogo sasa lakini repercussion yake itakuwa kubwa mbele ya safari,nahisi zaidi ya kuvuliwa hijab DC.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 11,747
  Likes Received: 3,451
  Trophy Points: 280
  <br />
  Alaaa kumbeeee!!!
   
 13. Blandes

  Blandes JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Uyo mama,alpaswa apewe kichapo mpaka ajue kuvuliwa nguo nini maana ke,lakn bado tunaendelea watapigwa wengi tu.
   
 14. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,414
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani dawa ni hiyo hiyo moja, mkong'oto tu!
   
 15. E

  ESAM JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hawa CCM watazidi kuumbuka lakini kama kawaida yao watu waliopagawa na mapepo huwa hawaoni aibu, ni wanafiki na waongo wa kutupwa. Ndiyo maana hata DC (kada wa CCM) anadiriki kusema uongo mchana kweupe.

  Polisi nao kwa kuwa na akili kama za mbwa (hawafikirii wanatii amri ya 'KAMATA' nao wanakamata) wanafanyia kazi uongo wa wazi.
   
 16. I

  Igembe Nsabo Member

  #16
  Sep 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tupe hizo nyuzi kashikwa UGONI wapi mie ni mtu wake wa kalibu sina hizo!!!!
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,918
  Likes Received: 1,697
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ipo siku watu watachoka kuonewa watajiingiza katika vita mbaya ambayo hata jeshi hawataweza kuzuia CCM ijue huwezi ukawakandamiza watu kwa miaka yote hiyo (Mungu aipushie mbali)
   
 18. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwa suala la wananchi/wapiga kura kuuza shahada zao kwa kupewa alfu kumi Upinzani wajitahidi kuelimisha wananchi juu ya haja ya mabadiliko,waachane na njaaa ndogo ndogo kama hizi, wakijitambua wananchi kwa ujumla wao hata ktk chaguzi zijazo itasaidia
   
 19. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ccm inaelekea kushinda,kama wamekamatwa jana je hilozoezi limeanza lini na wangapi wamesha uza?poor tz
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,342
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Alikuwa mchovu fulani UDSM huyo,siasa kazirukia ukubwani.
   
Loading...