Mabalaa humuandama mtoto wa kike tangu akiwa tumboni…………

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,332
Tatizo hili hufahamika kama Female Infanticide, yaani mauaji ya kukusudia yanayofanywa kwa mtoto wa kike. Achilia mbali kile kitendo cha mtoto kuuawa muda mfupi tu baada ya kuzaliwa, utelekezwaji wa mtoto wa kike mara tu anapozaliwa na kutoa mimba baada ya ugunduzi kwamba, ni mtoto wa kike, zote ni njia za kumuondoa mtoto wa kike duniani. Tatizo hili liko katika jamii zote zinazomchukulia mtoto wa kike kama balaa na yule wa kiume kama Baraka kwa familia.

Kwa hapa nchini mtoto wa kike huuawa kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Watoto wa kike hudharauliwa na kuachwa linapokuja swala la elimu katika familia. Ukichunguza hata wewe utabaini kwamba, katika familia nyingi, ambapo watoto wa kiume wamepata elimu bora, watoto wa kike katika familia hizo wamepuuzwa na hata kutopewa kabisa elimu.

Watoto wa kike, haswa wale wanaozaliwa nje ya ndoa wametelekezwa kirahisi, wamekataliwa na baba zao kirahisi, ukilinganisha na watoto wa kiume. Idadi ya watoto wa kike wanaokufa kutokana na kutelekezwa na kukataliwa na baba zao ni kubwa kuliko ya watoto wa kiume. Hata zile kesi nyingi za watoto kukataliwa na baba zao zinahusisha watoto wa kike zaidi. Ni jambo la kushangaza kwamba ndoa ambayo ina watoto wa kike watupu hutazamwa kwa bezo na dharau ukilinganisha na ile yenye watoto wa kiume watupu. Hata wale wanawake wanaozaa watoto wa kike watupu hujihisi vibaya na kuamini kwamba walistahili kuzaa watoto wa kiume pia.Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike hutazamwa kama, ‘biashara ya kesho' ambapo watauzwa kwa njia ya mahari.

Kwa hiyo thamani yao ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Na ndio maana mtoto wa kike anaposhindwa kuolewa huanza kuonekana kama mzigo usio na thamani, na hata kuzongwa hutokea. Ili kujinasua na tatizo hili, msichana huenda kwa mwanaume yeyote kama kwa kujilazimisha. Kila mtu anajua kuhusu wazazi hapa nchini, ambao wamekuwa wakiwalazimisha binti zao kurudi kwenye ndoa za mateso kwa hofu ya kurejesha mahari. Kinachotokea ni binti hao kuuawa na waume zao. Ni wazi hii ni njia ya makusudi ya kuwapunguza wanawake, bila kujali mtu ataieleza vipi……………….
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Mvumbuzi article yako ina ukweli kiasi kikubwa. Na naweza ku relate na sababu za wanawake wengi kuwa na low self esteem. Self esteem inakuzwa toka utoto. Ukishajua position yako kama binti kuwa you are always the second and best to none; huwezi kujiamini hata kidogo. Wanawake wengi wamelelewa kujiona kuwa wao ni second best.

Unaweza kupitia hiki chanzo hapa chini:

Untitled Document
 

Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Mtambuzi aksante sana. I wish ningewezakuishi na Binti yangu wa kufikia............... !

Ila natafuta jamani Binti!!

MJ1 si uzae na we ujilelee kabinti kako! Au nisubiri mi nikizaa nikuletee.......lol! Yaani article ya mtambuzi imejaa ukweli alafu imegusia kwa kiasi kikubwa halisi ya maisha ya mtoto wa kike!
 

HAZOLE

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,552
691
mtambuzi naona umetambua ...nilikwambia ukabisha ona sasa unakubali maneno yangu.safi, jamani tubadilike. RIP prof. wangari
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,812
12,406
Ni kweli kabisa licha ya kuwa zipo familia chache zinazowathamini watoto wa kike kuliko/sawa na watoto wa kiume.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
I don't see the women empowerment here, post nyingi zina discuss wanawake tu!
 

shalis

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
271
64
Siwezi sema sanaaa, ila mtoto wa kike katika familia akisoma na kujitambua huwa wanaleta maendeleo sana katika family zao tofauti na wakiume nimeona wengi hasa wachaga
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,332
Siwezi sema sanaaa, ila mtoto wa kike katika familia akisoma na kujitambua huwa wanaleta maendeleo sana katika family zao tofauti na wakiume nimeona wengi hasa wachaga

@Shalis.........., Uliyoyasema yana ukweli mkubwa. kuna msemo mmoja huw anaupenda sana, wanasema, 'Ukimwelimisha mtoto wa kike, umeielimisha jamii' , naupenda sana msemo huu, kwa sababu umethibitisha juu ya jambo hilo. Ipo mifano mingi sana inayoweza kuthibitisha ukweli huo.
Nimeshuhudia sana pale ambapo baba ni msomi ni mara chache kukuta elimu ikipewa msukumo katika familia kwa sababu sisi wanaume tunakuwa bize sana na majukumu mengi na mengine hata yasiyo na tija, lakini pale ambapo mama ni msomi hata kwa kiwango cha wastani, elimu katika familiya hiyo hupewa msukumu mkubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom