Mabaki ya Umakini/Attention Residues: Jinsi Mitandao ya Kijamii inavyodhoofisha BONGO

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Vitu viwili vikubwa ambavyo ni hazina katika dunia hii ya kiushindani ni,

1:WILLPOWER/ Uwezo wa Kuamua/kuchukua maamuzi na kuyasimamia bila kuyumba katikati ya Upizani/changamoto na vikwanzo.


2:UMAKINI wa KINA/DEEP ATTENTION - kuwa makini kwa kitu unachofanya hadi kifanikiwe.

ADUI MKUBWA WA HAYO JUU AMEJIFICHA KATIKA MITANDAO

UTAFITI: UMAKINI NA MITANDAO
Utafiti uliofanywa na Sophie Reloy (Business Proffessor) na kukubalika na wengi, Unapoacha kazi A na kukumbilia kazi B mabaki ya umakini wa kazi A,huwepo wakati unafanya kazi B. Sasa fikiria kila unachokifanya au kufungua kwenye mitandao ni kazi/activity kwa siku unafungua mara ngapi. Basi matokeo yake ni UMAKINI HAFIFU KWA KAZI INAYOFUATA.

UTAFITI:WILLPOWER/Uwezo wa kimaamuzi na mitandao

Utafiti uliofanywa na wanasaikolojia Wilhelm Hofmann na Roy Baumeister uliochukua sample zaidi ya 7500. Ulikuja na yafuatayo;
1: Kiwango cha uwezo wa Kuamua hupungua(finite/limited) .
2:Willpower ni tofauti na TABIA ambayo unaweza kuitumia bila kikomo(infinite/unlimited).

WILLPOWER INAPUNGUA VIPI,
Mfano umepanga kufanya shughuli flani ya Muhimu, ukajikuta umeacha umeanza kutangatanga mitandaoni, JF,Wassap groups etc, Emails, etc Itakuhitaji kiwango kikubwa cha WILLPOWER kurudi kwenye Kazi yako. Wakati kama ukitenga muda wa kufanya kazi Muhimu na ukafika wakati ukaifanya kama ROUTINE au ratiba bila muingiliano, utatumia WILLPOWER kidogo sana.
Fikilia kati ya hawa wawili nani atawahi kuishiwa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.

Nini Kifanyike,

1:Kama kazi zako zinahitaji Mitandao: Tengeneza mazingira katika ratiba yako ya maisha ya kazi na nyumbani kuwa nje kabisa ya mitandao hii.

2:Kama kazi yako haina ulazima wa kuwa mitandaoni, Tengeneza mazingira unapokuwa katika kazi zako, uweke mbali kabisa hii kitu.

Ushauri Mgumu kwa wanamitandao lakini ni wathamani SANA
Kuna kitu kinaitwa DIGITAL DETOXIFICATION wengine wanaita INTERNET SABBATH. Yaani kama wayahudi au Wasabato wanavyotenga siku moja ya kupumzika kwa wiki.Chagua siku Moja ambayo hautakuwa kwenye mitandao kabisa sio kusoma emails,wassap, fb,jf,etc. Hii iwe kama siku ya usafi wa UMAKINI ULIOJEUHIWA. Hii itawasaidia sana wengi ambao wana huu Ugonjwa INTERNET DISTRACTION ADDICTION ambao unaleta ATTENTION TOXIFICATION na WILL POWER DEPLETION. Zao lake ni mtu hafifu katika kila unachokifaya.

Hii ni sehemu tu ya elimu niliyokutana nayo huku duniani, ukitaka kwenda ndani zaidi PM utumiwe maelezo ya kina zaidi ya Page 100 kutoka kwenye chanzo halisi.
Nawakaribisha wenye uelewa na yoyte mwenye jambo.
 
Back
Top Bottom