Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Ndugu pole kwa hilo,

Fungus ikiwa niya uken haina haja ya tubes hizo cz hao fungus wako ndan tayar na huenda wako kwenye mfumo wa dam,
Hiyo kuna haja ya kutumia dawa za kumeza siyo za kupaka tena


Atumie dawa inaitwa
Griseofulvin,,,ni vidonge vya kumeza


Weny utalaam zaid wanakuja,lakin hiyo nakuhakikishia atapona,


Zingatia,kama ana mtu wake wakumwingia,lazima watumie dozi wote,
USAF na maji ya kunywa ni lazm,


Uguza pol
Safi sana
 
Habari JF DOCTORS, samahani naombeni msaada, mpenzi wangu anasumbuliwa sana na muwasho ukeni mara kwa mara, kaenda sana hospitali wanampa dawa na cream za kupaka, lakini hali inajirudia jirudia, akitumia dawa anapata nafuu temporary baada ya siku kadhaa hali inaanza tena, je tatizo hili linasababishwa na nini? suluhisho la kudumu ni nini? naombeni hata kama kuna tiba mbadala mtushauri ili atumie maana za hospitali naona kama zimemzoea sana
atumie dawa inaitwa gynozol za Egypt. Inakuwa vidonge 3 anatumia kwa siku 3 kila siku anaingiza kimoja wakati wa kulala(atapewa maelekezo na muuza). na akishamaliza dozi azingatie mambo yafuatayo, chupi zake awe anaanika nje kwenye jua asivae chupi iloanikwa ndani, baadhi ya condoms pia zinasababisha fungus, baadhi ya pad pia zinasababisha fungus.
 
Jaman nauliza kwa mara ya pili tena mdogo wangu anasumbuliwa na mba yan kama vile mbwa za kwenye nywele zmekuwa kama zmehamia usoni nilimunulia sonaderm/getraderm sijui kama nimepatia spelling inakaa poa tuu kwa mda asipojipaka hali inajirudia inafika time asipojipaka chochote usoni akijisugua uso unakuwa kama unatoa chembe chembe za ngozi refer mtu mwenye mba akiwa anajikwangua kichwa jinsi ngozi ya kichwa inavyokuwa nyeupe so hali inataka kukaribiana na hyo katika uso msaada wenu tena
 
Kama jina linavyojieleza kuna ndugu yangu anasumbuliwa na fangasi ambao wako sehem zá siri yeye ni mwanaume

Tatizo ni kwanza Amekuwa akitumia dawa kama fullconaze na gentallene c lakini zinapona kwa muda kisha zinajirudia mpaka Sasa ni miezi 9 tangia ili Tatizo limemuanza akitumia izo DAWA nilizotaja Apo juu wanapona kwa muda baadae wanarudi kwa kasi

Ivyo kwa yeyote ambayo Ana uzoefu na ili Tatizo plz naomba tusaidiane ili tuweze kumpa ndugu yetu tiba muafaka ili aondokane na ili Tatizo
 
Tatizo hilo linaweza kuwa nimeanzia ndani siyo hapo anapoziona hizo fangas, kwa hiyo, atumie dawa za kumeza


(Options include terbinafine (Lamisil) and itraconazole (Sporanox). These drugshelp a new skin grow free of infection, slowly replacing the infected part. You typically take this type of drug for six to 12 weeks.)
 
kama kichwa chá habari kinavyosema NATAFUTA DAWA YA FANGASI sugu wasiopona kwa DAWA zá kawaida lama izi full conaze, conaze na gentallene c

mwenye kujua DAWA YENYE UHAKIKA wa KUPONYESHA FANGASI anisaidie maana wamekuwa kero sababu nktumia DAWA wanapona baada YA muda wanarudi tena tafadhali mwenye kujua DAWA Kali zaidi YA nilizozitaja hapo juu basi anisaidie

Kiukweli wamekuwa Wasumbufu Sana sana maana hawataki kupona moja kwa moja dawa nilizozitaja hapo juu nishazitumia mara nyingi sana lakini wanapona na baada ya wiki mbili tatu wanarudi tena
 
Kwa anaye fahamu dawa ya FANGASI sugu tofauti na fullconaze, conaze, gentallene c anisaidie plz

FANGASI wamekuwa wakipiga wanamrudia akinywa dawa wanapona baadae wanarudi tena izo dawa tajwa hapo juu ndo anazotumia so kwa anayefahamu kali zaidi ya izi msaada plz
 
Hoja hapa si dawa Bali ni namna gani unaitibu hiyo Fungus , Kwa Maelezo yako inaonekana kuwa wewe huna tatizo la dawa Bali ni mbinu unazotumia wakati unapotibu hiyo fungus
JARIBU HII
Tumia dawa hizo hizo zilizokuwa zikikupa nafuu Na kurudi lakini safari hii Fanya kazi ya kutibu viabata vyako . Tunapotibu magonjwa ya juu ya Ngozi Mara nyingi huwa tunaacha kutibu NGUO Na taulo tulizozitumia wakati tunaumwa .Kwa BAHATI mbaya hatutendi Yale yatakayotokomeza ugonjwa huu SASA FANYA HAYA @@ Chovya NGUO zoote ulizozivaa kabla ya matibabu kwenye MAJI ya MOTO YAMOTO HASWA ili kuwauwa vimelea Vya fungus ambavyo Mara zoote usipofanya haya ,utameza dawa saana Na kupaka lakini baada ya muda tatizo litarudi palepale kwa sababu source haikushughulikiwa
USHAURI WANGU
Panga au chagua NGUO za kuvaa kipindi cha week ya kwanza unapoanza matibabu Na wakati huo huo andaa nguo za kuvaa kutandika , kulalia had I taulo zichovywe kwenye MAJI ya moto Na baada ya hapo zianikwe Na kuzitumia baada ya kukauka . UKIFANYA HIVI TANGAZA USHINDI
 
Kuna dawa nimetumia inaitwa Anti-Dandruff Shampoo.
Selsun selenium Sulfide. Naona imeng'arisha kichwa.Sasa sijui muda utajirudia au lah.100ml inauzwa 25000 Na 50ml inauzwa 15500 JD Pharmacy
d2b4f8c995d8da480fbd48c5e986dd91.jpg
 
Msaada kwa yule anayejua dawa au tiba jamani,niko DAR ES SALAM huwa nikija dar huku ugonjwa huwa naupata abao na dalili zake .........

(1)muwasho

(2)maumivu

(3)kutoka kwa mabaka meusi kama unba sehemu za korodani
 
Msaada kwa yule anayejua dawa au tiba jamani,niko DAR ES SALAM huwa nikija dar huku ugonjwa huwa naupata abao na dalili zake .........
(1)muwasho
(2)maumivu
(3)kutoka kwa mabaka meusi kama unba sehemu za korodani
Ulishawahi kwenda hospitali kuonana na matabibu??

Walikushauri nini??

Kama bado hujaenda, kwanini??
 
Maduka ya dawa zipo katika vichupa dawa ina rangi ya kijani inauzwa 2000 hiyo kiboko, ni ya kupaka uliza dawa ya mba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom