Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Dawa ya kudumu ni kuacha kabisa kutumia taulo, au kama ukiamua kuendelea kulitumia lazima uhakikishe kuwa unalianika nje kila linapotumika. Ila nakushauri usilitumie kabisa tumia kanga tuu.
Hzo dawa njengine ni za muda tuu.
Kuna tofauti ipi kati ya kanga na tauro?
 
Mkuu nilipata tatizo kama lako, mimi lilinipata kwenye dushe, nikaamua kwenda hospitali wakanipa dawa na kuniambia sio ugonjwa wa zinaa ila ukikutana na mwenza ambaye sio msafi anaweza kukuletea fangasi.

Nilitumia dawa za hospitali bila mafanikio, kama ilikuwa inazidi, bahati nikawa nasoma sana google.

Nikaona sehemu wanayasifia sana mafuta ya nazi, wakasema ni tiba ni kubwa, wiki tu nikapona kabisa kabisa.
haya mafuta watu hawaelewi umuhimu wake lakini ni mafuta safi sana aisee, kwa ngozi na tiba mbali mbali, nahisi hata ebitoke hupaka yale mafuta
 
Kuna dawa moja nilipewaga na docta inaitwa gresefulvin ya vidonge, spell huenda nimekosea. Pamoja na gentrisone ya kupaka. Hii ya vidonge dozi yake ni mwezi 1. Kwa Mimi ilinitibu vizuri sana. Dozi ilikuwa sh. 3500/
Ni nzuri sana hiyo dawa shida yake sisi wa bila bia usingizi ni shida inakuwa mtihani kweli
 
Kaka hayo mafuta ni yale wanayonunua dukan au ya kutengeneza mwenyewe na kama ni ya dukan ni aina gani maana kuna kampuni nyingi zinauza mafuta ya nazi
ingawa hainihusu nahisi ni yale natural ya bila kemikali yoyote, zanzibar yako mengi sana na bei rahisi sana, chupa la lita na nusu elf 3 tu
 
Jf doctor naombeni kujua ni dawa gani inatibu fangasi za sehem za siri.... Maana nna fangasi mpaka mkojo unatoka una rangi ya njano
Dawa ni nyingi inategemea na severity ya ugonjwa..tumia vidonge vya Griseofulvin au ketaconazole au Fluconazole
 
Jamani wanajamii naomba mnisaidie mwenzenu haraka sanaa...Ni hivi siku za karibuni nimekuwa na tatizo kwenye ngozi ya korodani (scrotum) tatizo lenyewe ni kwamba hiyo ngozi inakuwa ngumu kidogo ya kujikunja na inawasha sanaa kiasi kwamba ukikuna unahisi rahaa.

Na kibaya sahivi naona imeanza kubabuka yaani kama ile nyoka akifa ile ngozi inavyotoka na haitoki na nyama wala nini.

Sasa wajameni nauliza hili ni tatizo ganii? au ni Fangas??? na situmii dawa yeyote mimii au ni Joto la DSM maana mm Wa Arusha.

PLease help me peoples!
The mason ninatatizo kama hili kk ulitumia dawa gani mzee
 
Habari zenu wandugu,ninatatzo ambalo ni zito na kero kwangu kama linavyojieleza hapo head above, ninatatizo hilo la kuwashwa kwenye korodani na kutokewa na ukungu katika eneo hilo kwa muda mrefu.

Sasa na nishatumia kila aina ya dawa za hospitali na dawa za kisuna znazopatikana katika maduka ya dawa za asili za kiislam lakini napata afadhali kwa wiki moja ama mbili then tatizo linajirudia.

Naombeni msaada wenu ninasumbuliwa na hili tatizo kwa muda mrefu sasa yaweza kuwa hata ni mwaka na nusu sasa,naombeni msaada wenu tafadhalini ndugu zanguni.
Naomba kusaidia kidogo:
Tatizo lako laweza kuwa ni fungus wanaosababisha Tinea cruris na huwashambulia zaidi jinsia ya me. Hawa huanzia kwenye scrotum na kusambaa mpaka kwenye groin wakati mwingine mpk matakoni.

Kikubwa ni kuzingatia usafi wa hali ya juu sana i.e fua boxer kila siku na suruali zako ziwe safi always as uchafu hubeba spores ambazo hu-hatch na kutengeneza uyoga huo. Pia epuka ngono kipindi cha matibabu maana utamuambukiza mwenzako mkigusana naye atakuambukiza mkirudia tendo!!!

Matibabu: tumia tabs za Griseofuvin 500mg/siku mpaka upone. Hii dawa hutumika kwa muda wa week 4-6. Kila siku means utumie 500mg kila baada ya masaa 24.

Dawa nyingine ni Terbinafin, itraconazole au fluconazole.

Onyo: usikatishe dawa hata kama kuna dalili za kupona, hakikisha unamaliza dozi. Hii itakusaidia ugonjwa kutojirudiarudia.

Pole sana!
 
kapime HIV maana kuna uhusiano wa karibu kati ya hiv na fungus (ukungu)

Tena kama zinajirudia baada ya kutibu cheki mkuu
 
Tumia dawa mfululizo kwa muda mrefu fungus huwa hawafi haraka.

Pia naweza paka ute wa majini ya alovera pamoja na mafuta ya nazi yanayouzwa dukani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom