Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Speaker, there you are; Hakuna aliyepitia Pugu na kutumia maji ya "pondi" ambaye hakupata dhahama ya severe pumbu fungus

hahahahahaha,dah unanikubusha rafiki yangu mmoja jinsi alivokuwa anateseka nao aisee!

Kumbe sasa sio uchafu tu unao weza kusababisha lakini na maji tunayo tumia au mabafu tunayo changia uswahilini!
maana unaweza kusema uwe msafi lakini pale unapo enda kuji safishia ni pachafu sana
 
Ndugu wana JF, Ninasumbuliwa na Fungus za kwenye ngozi katikati ya paja na testicles, imeshambulia na testicles pia( Tinea cruris). Nimejaribu kutumia ketoconazole,Miconazole creams zote zimeshindwa kutibu. Naomba mtu anayefahamu dawa itakayoweza kuniondolea tatizo hili anisaidie. Natanguliza shukurani.
 
Mchawi ni wewe mwenyewe unajua kabisa Fungus wanaendana na hali ya hewa
Kama ulikuwa unavaa Chupi acha hakikisha hapo mahala pakavu 24/7 pili hakikisha unatumia
antibacteria soap kwa kuogea na hii lazima ifanyike si kwa mda mchache ni lazima kama miaka 2 hadi 3
Mwisho kila unapooshea na antibacteria paka hiyo dawa yako na tumia hiyo si chini ya miezi sita hadi mwaka
na lazima iwe 2 times a day. na ni everyday so kuoga ni lazima kila siku

Natumaini utapona.
 
Tumia poda ya mycodem...! Ni nzuri sana na inakausha mara moja...! Usitumia cream huwa zinaongezabsana fungus kwa sababu ya unyevunyevu...!
 
Ushauri wangu ni kama ufuatao:-

Hakikisha sehemu husika inakuwa kavu masaa 24,pili pakaa poda yoyote ya kutibu fangasi asubuhi na usiku kwa wiki 4 mfululizo.

tatu,tafuta na meza antibiotic eg cloxacillin 250mg(2 x 3 siku 5) kama sehemu yenyewe imekwa kama kidonda ili uweze kukausha haraka.

Nne usivae boxer/chupi bali vaa bukta yenye kuruhusu hewa kupita na jikaushe vizuri baada ya kuoga(ni vizuri kusubiri ukauke kabla ya kuvaa nguo).

Usitumie sabuni zenye dawa kwani zitakusaidia kwa muda lakini zitafanya ngozi kupoteza uwezo wake wa asili wa kujilinda dhidi ya vijidudu(ngozi ina uwezo wa kujilinda kiasili,haiitaji msaada, na uwezo wake unaongezeka kadiri inavyoshambuliwa na vijidudu-)

Tano hakikisha unabadili nguo ya ndani kila siku na unavaa nguo safi na ikibidi uipige pasi kila siku.
Sita,tumia cream inayoitwa QUADRIDERM X 2 KWA SIKU 14 lakini ipake sehemu ikiwa kavu na kaa dk 15-30 kabla ya kuvaa nguo

Mwisho,unaweza kwenda hospitali kwa uchunguzi na ushauri zaidi!
 
Jamani msaidieni huyu dada amekuwa na Vaginal discharge kwa muda mrefu karibia mwaka sasa, vipimo vinaonyesha ni candidiasis. Ametumia dawa nyingi lakini tatizo linajirudia.
 
inawezekana hatumii dawa kwa usahihi,pia azingatie masharti anayopewa na dactari.

pia aende kwa wataalamu wa magonjwa ya kinamama atapata msaada huko
 
Asante kwa ushauri. Ameonana na wataalam hao ndo waliomwandikia dawa hizo mbalimbali zikiwemo za kumeza, kupaka na kupachika. Anapona kwa muda halaf tatzo linajirudia,
 
Hakuna ugonjwa mgumu kupona ukiingia kwenye mwili kama Fungus, unaweza kujikuta unamalza hospital na dawa zote bila mafanikio. Mwambie asichoke aendelee kutumia dawa, zitamsaidia. Ila kweli ni mgumu kupona, cjui ni kwa nini. Labda kama kuna wataalam humu watatupa majib zaid.

Inawezekana anatumia dawa lakini anajiosha sana ukeni akiingiza maji yakiwa/yasiyo na sabuni/dettol (douching)....wanawake wengi huwa wanafikiri hii ni njia sahihi ya kutunza usafi wa uke na kujiepusha na maginjwa kama hayo ya candidiasis na bacterial vaginosis, lakini si kweli. Kuosha kwa kuingiza vidole ukeni ukitumia maji + sabuni/dettol ndio kunaongeza tatizo hata kama unatumia dawa! Kama anafanya hivyo aache, aoge tu kawaida na kuweka dawa.
 
Pia ajaribu kutumia dawa hii ya kupaka TOLNAFTATE TOPICAL SOLUTION ni nzuri sana kwa fungus.
 
Kuongezea kwa yaliyosemwa,afue/aloweke nguo za ndani na maji ya moto na sabuni,then azianike juani na kupiga pas kila wakati.fungus hubaki kwa chup na mara umalalizapo doz hushangaa wanarud tena,nguo za ndani zisibane sana hewa inahitajika kunako ikulu, wakati wa mwezini asishinde na pad siku nzima bila kubAdilisha.ajitahidi kuvaa nguo za cotton [chupi]kwani zinafyonza majimaji vizuri.wadada wengi huona nguo za cotton ni ghali na hazina mvuto lla ndo nzuri kiafya.atumie dawa bil kuacha dozi au kupitiliza masaa au cku .
 
Inawezekana anatumia dawa lakini anajiosha sana ukeni akiingiza maji yakiwa/yasiyo na sabuni/dettol (douching)....wanawake wengi huwa wanafikiri hii ni njia sahihi ya kutunza usafi wa uke na kujiepusha na maginjwa kama hayo ya candidiasis na bacterial vaginosis, lakini si kweli. Kuosha kwa kuingiza vidole ukeni ukitumia maji + sabuni/dettol ndio kunaongeza tatizo hata kama unatumia dawa! Kama anafanya hivyo aache, aoge tu kawaida na kuweka dawa.
Ndugu yangu Riwa,
Umezungumza kitaalamu kabisa.....naomba niongeze kidogo;KATIKA BODY ORGANS ZA MWANADAMU NI KIUNGO KIMOJA TU NDIO KINACHOJISAFISHA CHENYEWE.NI ''UKE''
NDANI YA UKE KUNA''GOOD BACTERIA'' AND ''BAD BACTERIA''-Sasa unapokuwa unaosha kila mara(kama alivyoeleza hapo RIWA) unawauwa good bacteria ambao ndio wanafanya ulinzi sehemu hiyo especially ukiwa mwezini kwani body tissues zinakuwa dhaifu sana kukukinga na magonjwa.
Uke wenyewe una''control'' ''Ph level kulingana na mazingila.
Kama utakuwa unataka maelezo zaidi ni ''PM-i will do the best kukushauri.
 
Mshauri akatibiwe na mwenza wake kwani kama ana mwenza na anatibiwa peke yake akipona wakikutana tena ana-pick ugonjwa upya.
 
Habari zenu wanaJF doc's.,
Naombeni msaada in that thing, imetoka kama ni fungus flani hivi juu ya kichwa cha u*me, yaani inakuwa ka punye flani, ikipona kuna kuwa ka kagamba kalaini but ukikatoa panaanza upya.,
Just wanned to know if this Ant-bacteria medicine can cure this thing..!
Any aidia plz!
 
Nenda kapime hosptal wewe inaweza ikawa STD inaitwa kaswende hiyo at early stages. Kimbia haraka huko na kama vipi nenda na mwanadani wako mkapime woote,..

NB: Kumbuka condom kuepeukana na magonjwa kama haya!
 
Habari zenu wanaJF doc's.,
Naombeni msaada in that thing, imetoka kama ni fungus flani hivi juu ya kichwa cha u*me, yaani inakuwa ka punye flani, ikipona kuna kuwa ka kagamba kalaini but ukikatoa panaanza upya.,
Just wanned to know if this Ant-bacteria medicine can cure this thing..!
Any aidia plz!

Heading yako na aticle yako ni tofauti, heading ni vagina, na aticle is all about uume wa kichwa.
unanichanganya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom