Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

N'na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa fangasi sehemu za siri na nimetumia dawa nyingi za hospital bila mafanikio.
 
Aina za dawa nilizo tumia ni jamii ya mafuta na vidonge,nili pakaa ikawa imepungua. Nikiacha kupaka kwa muda inarudi.
 
Aina za dawa nilizo tumia ni jamii ya mafuta na vidonge,nili pakaa ikawa imepungua. Nikiacha kupaka kwa muda inarudi.
Nikuulize swali, ndugu wewe ni mnywaji wa bia. Kama jibu ni ndio acha kunywa maliza matibabu kwanza.

Kuna jama yangu alikuwa naye ana matatizo kama hayo ya kwako, na akashauriwa kuacha kunywa bia au pombe na kweli ilikuja msaidia sana. Ila sasa sielewi kwa upande wako ni vipi.
 
Hebu fafanua vizuri ni aina gani ya dawa ulizowahi kutumia. Ili tuweze kukusaidia. Ziandike kwa majina na muda gani ulitumia.
 
maadam umeleta hapa sasa tambua tatizo lako limekwisha.
i had the similar case na Jf ilinisaidia kupata dawa. tumia white fields ointment (ya kupaka) na nunua grussiofluvin (vidonge 30 na utakunywa kimoja kila siku huku ukipaka whitefields ointment mara unapomaliza kuoga).
kikubwa ni kumaliza dozi.
pombe usinywe kwa kipindi chote maana pombe inapunguza nguvu ya dawa. mimi wakati natumia nilibanwa na kiu siku moja nikanywa kiroba kimoja ila nilikomaa mpaka dawa ikaisha na niliongeza vidonge vitano kwa hasira, nipo gado sasa. kwa kifupi nikwamba dozi ni ndefu kama mwezi na nusu maana sikwamba ukimaliza dozi tu uanze ulabu, tulia japo 5 days.
 
kwanza usafi unatakiwa sana, pili yawezekana maji unayotumia kujisafisha pia ukimaliza kujisafisha jikaushe, tatu unatakiwa unywe maji mengi sana atleast lita 3 kwa siku matatizo yote yataisha. Pole sana
 
N'na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa fangasi sehemu za siri na nimetumia dawa nyingi za hospital bila mafanikio.

Pole sana. mbali na njia njinginezo ambazo mtu waweza kupata fangasi,vitu kama

1: kushare mataulo,

2: kutokujikausha vizuri unapotoka kuoga,au haja ndogo/kubwa.

3:kutokumwaga maji ya kutosha unapoenda kutumia choo(kumbuka kama wewe ni msichana hakikisha unamwaga maji ya kutosha unapoenda chooni iwe haja kubwa au ndogo hata kama unaona choo lulichoingia ni kisafi kwa macho kwa sababu mtu akishatumia choo hata tu ile kukojoa mkojo mdodo sana kama vijiko viwili, kama ana fangasi na hakusukuma mkojo wake vizuri ni rahisi sana utakapotumia na wewe kuondoka na bacteria hao.

4: kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri

5: kutumia taulo muda mrefu bila kulifua( kumbuka kupiga pasi taulo unazotumia na hakikisha hutumii mataulo ya kwenye mahoteli kwa hiyo unaposafiri beba taulo lako.

6: kuchangia soap dish(ni vyema ukajitegeme kifaa chako cha kuwekea sabuni zako za kuogea(kama ni mwanamke na una familia wengine wanaweza wasikuelewe,lakini kumbuka kila mtu anapoingia bafuni ana ustarabu anaoujua yeye wa kutumia vifaa vya bafuni so bora ujikinge hapa.

7: kutumia ndoo za kupigia deki kwa kuogea

8: kutumia muda mrefu pedi za kujisitiri siku za heshima kwa msichana

9: kukaa muda mrefu na nguo ya ndani bila kubadilisha n.k n.k
nakutakia matibabu mazuri upone na hizo fangasi zizirudi tena.
 
Tafadhali muone Daktari wa magonjwa ya ngozi, ili aweze kutambua ni aina gani ya FANGASI unayoumwa ili akupe TIBA iliyo sahihi .Pole sana, Mungu atakuongoza umpate Daktari wa magonjwa ya NGOZI
 
Mara nyingi hizi huambukizwa na "partner" wako, kama utajitibu wewe na "partner" hapati tiba ni kazi bure tu. Halafu kubuka kuna maradhi yanaitwa "Male Yeast Infection" ambayo mara nyingi hutibiwa kama fungus lakini tiba huwa haileti tija. Nakushauri u google, utapata jibu.

Tiba mbadala:

1) Ponda vitunguu saum, changanya na ndimu halafu paka sehemu zote zilizoathirika, usiogope haiwashi kihivyo.

2) Kama umeoa/olewa acheni kuingiliana mpaka wote wawili muhakikishe mmepona.

3) Kama hujaoa/olewa, wacha zinaa, tubu kwa Mungu, jitibu, tafuta mume/mke muoane.
 
Jamani jamani vitunguu na ndimu sehemu za siri? Dah Riwa yuko wapi atuambie vizuri.
 
Nashukuru kwa msaada wenu wa mawazo na maelekezo mlio nipa,hakika sasa nitapona fangasi. Ur's mr m
 
Jatropha soap. Jioshee kila mara na paka sehemu iliyoathirika. Fungus will absolutely finished.
 
Pole sana. mbali na njia njinginezo ambazo mtu waweza kupata fangasi,vitu kama

1: kushare mataulo,

2: kutokujikausha vizuri unapotoka kuoga,au haja ndogo/kubwa.

3:kutokumwaga maji ya kutosha unapoenda kutumia choo(kumbuka kama wewe ni msichana hakikisha unamwaga maji ya kutosha unapoenda chooni iwe haja kubwa au ndogo hata kama unaona choo lulichoingia ni kisafi kwa macho kwa sababu mtu akishatumia choo hata tu ile kukojoa mkojo mdodo sana kama vijiko viwili, kama ana fangasi na hakusukuma mkojo wake vizuri ni rahisi sana utakapotumia na wewe kuondoka na bacteria hao.

4: kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri

5: kutumia taulo muda mrefu bila kulifua( kumbuka kupiga pasi taulo unazotumia na hakikisha hutumii mataulo ya kwenye mahoteli kwa hiyo unaposafiri beba taulo lako.

6: kuchangia soap dish(ni vyema ukajitegeme kifaa chako cha kuwekea sabuni zako za kuogea(kama ni mwanamke na una familia wengine wanaweza wasikuelewe,lakini kumbuka kila mtu anapoingia bafuni ana ustarabu anaoujua yeye wa kutumia vifaa vya bafuni so bora ujikinge hapa.

7: kutumia ndoo za kupigia deki kwa kuogea

8: kutumia muda mrefu pedi za kujisitiri siku za heshima kwa msichana

9: kukaa muda mrefu na nguo ya ndani bila kubadilisha n.k n.k
nakutakia matibabu mazuri upone na hizo fangasi zizirudi tena.
Kwa ujumla umemwelewesha vizuri iila hapo kwenye 'red' naomba ufafanuzi muda mrefu unaomaanisha wewe? ni masaa, siku,au muda mrefu wa aina gani? maana mimi kila niogapo nabadilisha haijalishi ni masaa mawili yamepita (kama siko kwenye heshima), na mara nyingi tunatoka nyumbani asubuhi tukiwa safi, Twashinda kazini tunarudi jioni twaoga/twajiswafi twabadilisha. Sasa muda mrefu unaouzungumzia wewe ni upi ufafanuzi tafadhali?

Vile vile tunatofautiana maumbile kuna wengine always wanakuwa wet si kwenye heshima si kwenye kawaida sasa hao pia tuwashaurije.
 
Aina za dawa nilizo tumia ni jamii ya mafuta na vidonge,nili pakaa ikawa imepungua. Nikiacha kupaka kwa muda inarudi.

Jitahidi kuwa msafi wa nguo za ndan,km kubadili kila baada ya masaa 12,piga pas kabla ya kuvaa,zisianikwe chumbani, zianikwe nje zipate jua,usivae ikiwa mbichi (ikiwa na unyevunyevu)Huduma -Kamua juisi ya Limao osha na tia ktk tundu ya kiungo athirika,kisha paka asali,(2)Punguza "KUCHOVYACHOVYA"Hali hiyo ikizidi itakuunguzia mayai usije kosa watoto!
 
Kwa ujumla umemwelewesha vizuri iila hapo kwenye 'red' naomba ufafanuzi muda mrefu unaomaanisha wewe? ni masaa, siku,au muda mrefu wa aina gani? maana mimi kila niogapo nabadilisha haijalishi ni masaa mawili yamepita (kama siko kwenye heshima), na mara nyingi tunatoka nyumbani asubuhi tukiwa safi, Twashinda kazini tunarudi jioni twaoga/twajiswafi twabadilisha. Sasa muda mrefu unaouzungumzia wewe ni upi ufafanuzi tafadhali?

Vile vile tunatofautiana maumbile kuna wengine always wanakuwa wet si kwenye heshima si kwenye kawaida sasa hao pia tuwashaurije.

Asante rubi.Kukaa muda mrefu nilikuwa namaanisha kama mtu si mtokaji wa nyumbani kuanzia asubuhi hadi jioni yaani yupo nyumbani ahakikishe anajiswafi mara kwa mara na kubadili.najua wengi twatoka majumbani mwetu asubuh na kurudi usiku na inakuwa ngumu.

kwa wale ambao wako wet mda wote kwa kweli sifaham wanatakiwa wafanyaje,bila shaka wataalam waliopo hapa watatujuza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom