Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu sehemu za siri: Dalili na Matibabu yake

JamiiForums

Official Robot
Joined
Nov 9, 2006
Messages
5,477
Points
2,000

JamiiForums

Official Robot
Joined Nov 9, 2006
5,477 2,000
Wakuu,

Tunaomba ushauri wenu, kwa wale ambao specialists wa magonjwa haya ya ngozi. Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi ambao wamekuwa wanahangaika kupata suluhu ya matatizo haya ya MBA, Fangasi na mabaka (hasa kwenye sehemu za siri, yakiwemo mapaja).

Shukrani

Tafadhari tunaomba ushauri wenu:

A. Kuhusu Fungus za sehemu za siri:
Zinatibiwa vipi au na dawa gani? Mdau anadai amefanya yafuatayo mpaka sasa:
1. Kunyoa muda wote
2. Kukausha vizuri kwa taulo baada ya kuoga
3. Kutumia gentriderm ya kupaka.
Na ameona kuwa akitumia gentriderm zinapona lakini baada kama ya wiki zinarudi.

B. Mabaka:
Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani na sehemu nyingine za mwili?

C.Mba:
Dawa ya mba please? (Tunafahamu kuna mjadala juu ya MBA tu hapa => Ujue ugonjwa wa Mba na Tiba yake

NB:
Kwa kila moja ya dawa utajazo hapo juu tuambie kama mtoto anaweza kutumia, na kama hawezi; ni umri gani unashauriwa?

Je, kwa magonjwa hayo kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.

===========
Similar Cases:
GOOD DAY ALL,

Habari ya week end members. Ninaomba kujuzwa dawa na matibabu ya tatizo la fungus (any kind of fungus) au kama kuna specialist wa hili eneo mnijulishe.

Binafsi ninatatizo la fungus ambao nikitumia dawa wanapotea wote na it takes about a month or two tatizo linajirudia. Nimetumia dawa nyingi na mara nyingi tu.

Msaada jamani.
Wanajamvi heshima kwenu,

Mimi nilisumbuliwa na fangas kwa muda mrefu sana kwenye sehemu za siri, lakini namshukuru mungu nimepona ila wakati naumwa mapaja yangu yalibadilika na kuwa meusi sana mpaka yanakawa yanatisha sana ila kadri siku zinavyosonga yanaanza kubadilika.

Sasa, naja kwenu JF Doctors kwa ushauri wenu kuwa nawezaje kupata dawa ya kupaka ya kuweza kuondoa huo weusi?

Nitashukuru sana wandugu endapo nitafanikiwa kwa hili
Habari JF DOCTORS,

Nisaidieni kwa mda sasa nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi ya makende kiasi kwamba yakianza kuwasha ni shidaa yanawaka ka moto vile.

Nshajaribu sabuni za rungu, protector, na detal ya maji lakn sijapona.

Jamani, msaada kwa anayejua dawa ya hili tatizo manake linanikosesha raha kwakweli.
==========
MASWALI MUHIMU:
Wataalam naomba kuuliza maswali saba (7) ambayo kwa muda mrefu nimetafuta MAJIBU YA UHAKIKA bila mafaniko.

Naamini wataalamu wetu wa JF mtanisaidia:-

1. Je kitaalamu kuna aina ngapi za fangus? Aina hizi zinatambulika kwa dalili tofauti?
2. Naomba kufahamishwa kama matibabu yake hutofautiana kwa mwanamke na mwanamume.
3. Je, mikorogo kwa wakina-dada huweza kusababisha mashambulizi ya fangus?
4. Dawa za Fangus (tube ama unga) zipatikanazo kwenye Pharmacy zetu zaweza kutumiwa popote penye fangus? Eg hata ukeni/uumeni? na jinsia yoyote?
5. Mwanamke akitumia ya unga/au ya kupaka pana madhara gani kama itaingia mpaka ukeni? Kuna angalizo lolote?
6. Vagina PH inaweza kwa namna yoyote kusababisha fangus kwa mama na dada zetu?
7. Mtu aliyetumia hizi tube almost zote na nyingi kati ya Pawder anashauriwa atumie dawa gani? (Kuna vidonge au sindano?) ambavyo ni effective zaidi?

Majibu yako yatasaidia wengi, hivyo kwa niaba yao na mimi mwenyewe, naomba kutanguliza shukurani kwa wataalam wetu.
==========
Walionufaika na ushauri wa wadau:
Wadau,

Napenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu nyote nimepona ugonjwa wa fungus wa mwili niliokuwa nao kwa muda takribani miaka 12.

Nimetibiwa hospital ya masista Kawe unashukia kituo kinaitwa Kanisani kama ukipanda daladala.

Jaribu nawe kama una tatizo kama langu thanks so much JF
Ushuhuda: Ndimu dawa nzuri ya fangasi

Salaam wadau,
Kwa kweli JF imekuwa na msaada mkubwa sana kwangu binafsi. Nimejifunza vingi hapa.

Mojawapo ya mambo mazuri niliyojifunza hapa ni dawa ya kutibu fungus za sehemu za siri za wanaume. Sehemu iliyojibana kati ya mapaja na mfuko wa korodani. Niseme ukweli nimwtumia dawa nyingi sana lakini tatizo likawa linapona na kurudi.

Nilipoingia hapa kutafuta dawa nikakutana na maoni ya watu wakisema ndimu au limao ni dawa pia. Ukweli nilipoitumia ilinichukua siku 7 tu kupona. Ni sawa na ndimu 7 tu nilizonunua kwa bei ya sh 100 kila moja. Napata kipande asubuhi na kipande jioni.

Hakuna muwasho tena, hakuna kunuka tena, hakuna kubadilika rangi ya makende wala kutokuwa na confidence siku ukiwa faragha na mwenza.

Jamani nashauri dawa ya bure kabisa unapona. Si gharama na ni rahisi kutumia na inapatikana kila mahali. Sasa nimejiweke ulinzi wa kupaka kila week angalau mara 2 kuhakikisha hazirudi tena kabisa.

Zingatia: usafi ni muhimu sana na epuka unyevu nyevu wa aina yoyote. Ikiwezekana anika taulo lako juani kila baada ya kuoga. Au tumia taulo kavu muda wote.
 

Bill

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
5,489
Points
2,000

Bill

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
5,489 2,000
Cha msingi nenda hospitali uonane na dokta. Pia hakikisha unavaa nguo safi na kavu ukibadilisha chupi kila siku pia uhakikishe kabla ya kuvaa nguo umekausha sehemu hizo nyeti. Zingatia kupasafisha vizuri, ondoa mapovu ya sabuni na kausha vizuri pia.
 

Alinda

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2008
Messages
1,683
Points
2,000

Alinda

Platinum Member
Joined Jun 26, 2008
1,683 2,000
Pole sana Mfianchi!

Ushauri bora kabisa ni kwenda kumuona Dokta ingawaje watu wengi huwa na aibu kwenda kwa Dokta hasa linapotokuwa ni swala la mambo ya siri.

Pia inawezekana kabisa ukwa na tatizo la Candidiasis ambalo ni tatizo sugu miongoni mwa jamii. Kitu cha kufanya
jaribu kuwa msafi (kama alivyoshauri na mjumbe hapo juu)

Jaribu kuvaa nguo zisizo bana, ili kuweza kupata hewa na kufanya sehemu iwe dry,
Jaribu kama ikiwezeka kupaka powder (hii itakusaidia kukeep sehemu kuwa dry)
Hunapo onga hiyo sehemu iliyoadhilika (sehemu za sir) Husikutumie sabuni kwani soap ina bacteria fulani wanao huwa wadudu wa kukusaidia kuzuia hiyo fungal. (hapa onga kama kawaida osha na maji na baada ya hapo jipanguse vizuri tu,
Kama una partner wote wawili tumieni dawa na msijaribu kufanya tendo la ndoa mpaka hapo itakapodhibitishwa wote mmepona.

Dawa za kutumia mara nyingi kwa Candidiasis ni Clotrimazole, Ketoconazoleand .... ila ushauri zaid nenda kwa Dk, au nenda Laboratory kapime na peleka majibu kwa dk au kwa Pharmacist na utapa dawa nzuri tu.

Alinda
 

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,144
Points
0

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,144 0
|Nenda famasi lakini tafuta ambayo anauza mwanaume utakuwa free zaidi kujiexpress yourself. Dawa zipo binafsi wakati niko sekondari boarding nilishawahi kupata fangasi za kufa mtu lakini nilipata dawa na shule ikaendelea
 

afkombo

Member
Joined
Feb 9, 2008
Messages
93
Points
95

afkombo

Member
Joined Feb 9, 2008
93 95
Kaka nenda Hospital ukamuone Dr.
Kama unaona soo basi Jaribu Nystatin,Miconazole,Clotrimazole au Econazole km hao fungus wapo More supercially.Kam ni subcutaneous jaribu Amphotericin B,Itraconazole au Fluconazole
Lkn ni vizuri uende hosp au pharmacy ya maana coz dawa zina side effects.
 

Mrbwire

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Messages
201
Points
195

Mrbwire

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2009
201 195
Wataalam naomba kuuliza maswali saba (7) ambayo kwa muda mrefu nimetafuta MAJIBU YA UHAKIKA bila mafaniko.

Naamini wataalamu wetu wa JF mtanisaidia:-

1. Je kitaalamu kuna aina ngapi za fangus? Aina hizi zinatambulika kwa dalili tofauti?
2. Naomba kufahamishwa kama matibabu yake hutofautiana kwa mwanamke na mwanamume.
3. Je, mikorogo kwa wakina-dada huweza kusababisha mashambulizi ya fangus?
4. Dawa za Fangus (tube ama unga) zipatikanazo kwenye Pharmacy zetu zaweza kutumiwa popote penye fangus? Eg hata ukeni/uumeni? na jinsia yoyote?
5. Mwanamke akitumia ya unga/au ya kupaka pana madhara gani kama itaingia mpaka ukeni? Kuna angalizo lolote?
6. Vagina PH inaweza kwa namna yoyote kusababisha fangus kwa mama na dada zetu?
7. Mtu aliyetumia hizi tube almost zote na nyingi kati ya Pawder anashauriwa atumie dawa gani? (Kuna vidonge au sindano?) ambavyo ni effective zaidi?

Majibu yako yatasaidia wengi, hivyo kwa niaba yao na mimi mwenyewe, naomba kutanguliza shukurani kwa wataalam wetu.
 

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Messages
838
Points
0

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2010
838 0
Jitambulishe jinsia yako tukusaidie maana inategemea kwa wanaume mara nyingi ni ktk ngozi za korodani au kende na wanawake inaweza kuwa mpaka ndani ya nanihiii, sasa jitambulishe
 

Smarter

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Messages
463
Points
195

Smarter

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2008
463 195
Nadhani inachangiwa na kutojifuta maji vizuri after kuoga, kutonyoa kabisa sehemu hizo, na wenda nguo za ndani hazikauki vizuri.
 

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Messages
838
Points
0

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2010
838 0
Kama alivyosema Smarter hapo juu ni sahihi. kwanza ukisha maliza kuoga hakikisha unajifuta na kukauka kabisa, hatua nyingine, nyoa mavuzi yote ubaki kipara hasa sehemu za korodani.

Wakati wa kunawa tumia shampoo zilizoandikwa Antidundruf na medicated soap km protex n.k. Ukimaliza jisafishe na dettol liquid (ile ya chupa ya plastic) tumia pamba kujipaka dettol sehemu zilizoathirika.

Pia nakushauri ununue co-trimazole powder uwe unatumia wakati ukienda kazini jinyunyizie hasa ktka corners na mapaja.

Unaweza tumia zote dettol kupaka maana itakauka mara moja kisha jinyunyizie hiyo powder. natumai itakusaidia
 

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Messages
6,328
Points
1,195

Speaker

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2010
6,328 1,195
nadhani inachangiwa na kutojifuta maji vizuri after kuoga, kutonyoa kabisa sehemu hizo, na wenda nguo za ndani hazikauki vizuri.........
Niko smart sana,ila yawezekana bafu mahali hapa napoishi zikawa zina sababisha pia?
maana tupo wapangaji kibao na sina amani na bafu hizi
 

MKUNGA

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Messages
442
Points
195

MKUNGA

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2009
442 195
Mkuu hiyo hali inaitwa kipumbu ilitusumbua sana wkt tunasoma shule moja boarding (anonymous) teacher wa Chemistry msela2 alituma chemical moja nimeisahu tukajipaka.

Sababu kubwa ni mabafu yetu huku uswazi. Cha kufanya tumia sabuni ya dettol ile ya 2500 au 3000 mana hiza za 1000 nyingi zimechakachuliwa.

Vilevile nunua dawa ya kudekia ****** at least unaimwaga kwanza kuu bacteria mana uswahilini vyoo na mabafu vinadekiwa kwa foma ambyo sio antiseptic.

Kanunue dawa inaitwa FINGIDERM itakusaidia. nadhani umenisoma muu.
 

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Messages
6,328
Points
1,195

Speaker

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2010
6,328 1,195
mh! dettol na fungus hua havipatani sana! tumia gentrisone na utapona fasta.
Mkuu hiyo hali inaitwa kipumbu ilitusumbua sana wkt tunasoma shule moja boarding (anonymous) teacher wa Chemistry msela2 alituma chemical moja nimeisahu tukajipaka. Sababu kubwa ni mabafu yetu huku uswazi. Cha kufanya tumia sabuni ya dettol ile ya 2500 au 3000 mana hiza za 1000 nyingi zimechakachuliwa. Vile2 nunua dawa ya kudekia ****** at least unaimwaga kwanza kuu bacteria mana uswahilini vyoo na mabafu vinadekiwa kwa foma ambyo sio antiseptic. kanunue dawa inaitwa FINGIDERM itakusaidia. nadhani umenisoma muu.
Sana mkunga,asante sana mkuu nimekusoma!
Uswazi huku bafu ni chafu balaa duh nadhani ndio sababu,...vipi ndo mambo ya pugu nini?
 

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Messages
6,328
Points
1,195

Speaker

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2010
6,328 1,195
Inaelekea umeukubali ushauri wote uliopewa. Kuwa makini sana na ushauri wa kitabibu unaoupata JF.

KAMUONE DAKTARI HARAKA AKUPE USHAURI.
Kwanza nimependa signature yako,
asante sana mkuu,uzuri wa ushauri sio kwamba ndicho utakacho fanya,unaangalia kilicho bora unabeba na hata kama hakikufai basi unashukuru kwa walio jitahidi walau kujibu maana utakuta "123 views" na "3 replies" you must thank and appreciate these 3!

Nashukuru sana kwa kujali,hofu yako ni muhimu sana kwangu
 

Nanren

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Messages
1,849
Points
1,500

Nanren

JF-Expert Member
Joined May 11, 2009
1,849 1,500
Niko smart sana,ila yawezekana bafu mahali hapa napoishi zikawa zina sababisha pia?
maana tupo wapangaji kibao na sina amani na bafu hizi


Mbali na uliyoshauriwa na wadau hapo juu, kumbuka kuhakikisha chupi unayovaa wakati wote ni kavu. Ikifuliwa, lazima ipigwe pasi. Kama huna uwezo wa kupiga pasi ya umeme au mkaa, hakikisha chupi hiyo inakauka kwenye jua (direct sunlight) kwa masaa yasiyopungua sita. Tatizo litakwisha.
 

Forum statistics

Threads 1,390,914
Members 528,291
Posts 34,066,445
Top