Mabaharia kutoka Syria waliokwama katika Bandari ya Mombasa wauza meli yao

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Mwenye meli aliwatelekeza mabaharia hao tisa na kukataa kuwalipa mishahara yao. Mabaharia hao kutoka Syria wamekwama katika bandari ya Mombasa kwa muda wa mwaka moja na miezi tisa.

Mahakama ya Kenya imewaruhusu kuuza meli hio na kujilipa mishahara ambayo mwenye meli alikataa kuwalipa. Meli hio imeuzwa kwa bei ya ksh 50 million na mabaharia hao wanatarajia kulipwa pesa yao kabla ya kuondoka nchini.

Walikuwa wanategemea chakula cha msaada kutoka kwa Wakenya. Hii inaonyesha kwamba Kenya kuna sheria na mwenye meli akiwatelekeza mabaharia wake basi mahakama ya Kenya ina uwezo wa kuwaruhusu mabaharia hao kuuza meli na kujilipa mishahara waliostahili kulipwa.

Hii kesi itakuwa ni funzo kali sana kwa wamiliki meli wengine watundu wanaokataa kuwalipa mabaharia wao.

 
Kwenye wizi mnasema Kenya Kuna sheria,Ila kwenye kushugulikia mafisadi,hiyo sheria haipo.
 
Back
Top Bottom