Mabadiliko yoyote yale yanaanza na mimi, je uko tayari kubadilika kuanzia sasa?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wadau, kuna misemo mingi ambayo huwa tunaisoma na kuilewa inatuasa nini, lakini huwa hatuizingatii. Hii imenifanya niwe natafakari baadhi ya mambo na kujaribu kupata majibu yake.

Mfano, nimekuwa nikitafakari kwa nini baadhi yetu mara nyingi tunapochangia hoja humu jf au hata kwenye majukwaa mengine huwa tunaacha hoja na kumshambulia mtoa hoja kwa kutumia lugha ya kuudhi na wakati mwingine hata kile tunachochangia huwa kinakosa maana kabisa.

Nikaona pengine tatizo liko kwangu na nimeamua kubadilika kabisa - kwamba kwenye michango yangu yote nitatumia siku zote lugha ya staha na sitamshambulia mtoa hoja na kama kuna siku yoyote nitajikuta nafanya kinyume na maelezo haya, basi naomba mni'challenge'. Lengo ni kujenga utamaduni wa 'smart/intelligent/cogent thinking and reasoning'.

Ni matumaini yangu kwamba kwa vile nimebadilika na wewe ungependa kubadilika pia na kama itakupendeza kubadilika, naomba na wewe ufanye kama nilivyofanya na naamini wote tukiamua kubadilika hatimaye Tanzania yetu itaendelea kubadilika na kuwa mahali salama zaidi kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo. Heri tujaribu hivi kuliko kushindwa kujaribu kabisa.

Je, uko tayari kubadilika kuanzia sasa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom