Mzee Uchwara
Senior Member
- Oct 28, 2013
- 119
- 35
Ndugu wana Jf, kutokana na hali ya kiuchumi ya nchi yetu kuwa katika hali isiyoridhisha tunahitaji mabadiliko ya haraka ya kiuongozi. Lakini inashindikana kutokana na unafiki wa wanasiasa. Ndani ya chadema kuna sinto fahamu inayoendelea kuhusu kuvuliwa madaraka bwana zito na wenzake, tumeshuhudia matamko mengi sana kila kukicha, Embu tujikumbushe toka nyuma kuhushu shutuma ambazo zito zilimrenga hazikuanza leo zilianza toka zamani na zilitokana na yeye kutaka kugombea U/kiti. Pia hali hii ilimtokea marehe chacha wangwe. Mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu chadema kilichukua uongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Nakumbuka hakukuwa na shutuma za zito kuuza majimbo ya uchaguzi. Embu tujiulize je kama zito aliuza majimbo na hakushiriki kikamilifu ktk kumpigie dr slaa kampeni kwa nini alichaguliwa kuwa naibu kiongozi wa upinzani? Na kuhusu suala la posho chadema hao hao walimshambulia sana shibuda kipindi kile alipo kataa msimamo wa kutochukua posho je mmesahau? Na pia chadema waliitaka serikali ipunguze matumizi ikiwa pamoja na kutotumia magari yenye gharama kubwa na mh mbowe alirudisha gari la KUB lakini kutokana na unafiki wa wanasiasa wa kuto simamia yale wanayoongea alilifata kimiya kimiya na kuanza kulitumia. Pia tumeshuhudia mh lema akisahau na kuanza kutetea posho na kuanza kumshambulia zito. Embu tujiulize hivi hawa akina yericko, ben, nasari hizi nguvu za kumzushia na kumkashfu zito wanatoa wapi? Na kwa nini hawachukuriwi hatua? Mbona wale wanaomsema mbowe huchukuliwa hatua na kuitwa wasaliti! Ukitazama kwa makini utagundua unafiki wa wanasiasa kwa kuchochea migogoro kwa maslai yao binafsi na kuwazuia na kuwakwamisha wale wanaotaka madiliko ya kweli katika nchi yetu.