comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana jamvi salaam,
Ninapenda tujadili kwa pamoja haya yafuatayo:
Ninahisi na ninawaza kwa sauti kuwa na ni mawazo yangu kuwa:
Mabadiliko yanayochanganya na yasioisha katika sekta ya elimu ni moja ya vyanzo vilivyopelekea wanafunzi wasifaulu kwa wingi wao.
Kukata tamaa na vitisho vya kuwashusha vyeo walimu wakuu endapo matokeo yatakua mabaya bila kujali maslahi ya walimu wa shule za serikali pia huenda ndio sababu.
Uhaba wa walimu kwa baadhi ya shule za serikali ni moja sababu kubwa pia maana walimu wa masomo husika hawakuwepo.
Uhakiki usioisha pia uliwanyima nafasi ya kushughulikia masomo na maandalizi ya vipindi walimu, wengi walitoka shule za mbali wasijikite katika kufundisha wanafunzi wao maana walikua kila mara wanakwenda kuripoti katika halmashauri zao na kuacha majukumu yao.