Mabadiliko yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Jan 1, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vijana tulio wengi tumekuwa tukilalamika sana kuhusu hali ya maisha. Ni ukweli kuwa serikali imechangia kufika hapa tulipo kwa asilimia zaidi ya tisini. Kwanza kwa kuingiza wawekezaji na kuua viwanda vyetu na hatimaye uzalishaji wa ndani, kitu kilichopelekea kushusha thamani ya fedha ya Tanzania kwa sababu tuna - import zaidi ya tunavyo -export. Hali hii imepelekea uchumi kupolomoka na kwa upande mwingine mfumuko wa bei kuwa juu kila jua linapotoka.

  Wakati haya yote yakitokea chini ya serikali ya CCM hakuna dalili zozote ambazo zinaonesha kuwa kuna kiongozi hata mmoja wa serikali ambaye anahisi uchungu au maumivu juu ya hali ya Tanzania ya sasa. Kila mmoja anafikiria familia yake na hasa tumbo lake.

  Sisi tulio Watanzania wengi, tunafanya nini? Kila siku kulalamika humu Jamvini kunatusaidia nini? Hali ya maisha nchini hauwaumizi wana CDM wala wana CCM au NCCR mageuzi, Wala hata siyo CUF peke yao.

  Nimetembea katika mji wa Moshi, hakuna maduka ya watu wa CCM peke yao, wala maduka ya CDM wenyewe. Kifupi, hali ngumu ya maisha inatuumiza sisi sote bila kujali itikadi zetu za chama, dili wala kabila. Ni hadi hapo tutakapotambua kuwa mabadiliko yanaanza kwa kila mmoja wetu kwa kusema sasa basi!!! Ndipo hali ya mambo itakuwa nzuri.

  Tukiendelea kurumbana kwa itikadi za vyma na kuutanguliza udini ambao mimi nauita UDUNI... hali itazidi kuwa mbaya na CCM kuondoka madarakani kwa njia ya kura, bado sana, kila kitu ambacho kinafanywa na serikali ya Kikwete tunachokiona kuwa ni kizuri, Ni KIINI MACHO TU. Mfano mzuri ni MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

  Kwa mtazamo wangu, sifikiri kama kwa sheria iliyopitishwa na serikali ya CCM chini ya mwenyekiti wake na rais wake Kikwete inaweza kuleta katiba ya Watanzania tunayoitaka. Ni kiini macho tu.

  Tunisia alianza mtu mmoja tu na wengine wakafuata. Tusisubiri Mbowe na Dk Slaa waanze ndio tufuate, kulalamika kila siku bila kuchukua hatua ni sawa na Kelele za chura.....

  ...CHANGANYA NA ZAKO....
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna mantinki ktk thread yako Mwanajamvi!
   
Loading...