Mabadiliko ya vipaumbele vya serikali vyatajwa kuwa na athari kwa mipango ya TANESCO

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,147
2,000
TANESCO wametaja mabadiliko ya mara kwa mara ya vipaumbele vya serikali kama moja kati ya kitu ambacho huathiri mpango wa TANESCO. Hayo yameandikwa katika mpango wa TANESCO wa 2020 hadi 2025. Pia wametaja mahusiano ya kimataifa na makubaliano ambayo huwa yanakuwa tofauti tofauti.

Katika mambo ya kijamii, TANESCO wametaja hali ya kutothamini vitu vya umma kama vitu vya wananchi kunafanya watu waharibu miundombinu ya TANESCO na kusababisha athari kwa mipango yao ya kuwafikia raia.

Matumizi ya nishati mbadala kama gesi, kuni, umeme wa jua nk vimetajwa kama kitu kingine kinachoathiri mauzo ya umeme wa TANESCO mbali na kuwa na idadi kubwa ya watu walioelimika ambao wanahitaji huduma ya umeme.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom