Mabadiliko ya vifurushi: Kwa staili hii ushindani utatoka wapi?

DR SANTOS

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
10,509
21,399
Habari wana jamvi

Tanzania ndio nchi ambayo tunanunua bando kwa bei rahisi sana ukilinganisha na mataifa mengine, kumekua na tendency kubadili huduma za vifurushi hasa internet kwa makampuni hilo halina tatizo kwani lengo lao ni kuongeza income.

Mfano kupunguza idadi ya megabyte kwa asilimia kadhaa huku bei ikibaki ile ile.

Lakini unakuta zikitokea changes mtandao mmoja basi mabadiliko hua kote, mfano halotel walikua wanatoa GB 3 kwa shilingi elf 3 lakini sasa wanatoa GB 2 kwa elf tatu pia gb moja kwa shilingi elf moja sahizi ni MB's 600.

Vodacom walikua wakitoa GB 1 kwa shilingi elf moja lakini sasa wanatoa gb 1 kwa shilingi elf mbili! TTCL nao wamebadili bei sambamba na Tigo

Swali ni je, wanatumua busness plan moja? Kwanini isitokee kampuni ya kuleta ushindani wa kibiashara kwa kutobadili bei zake ili kampuni zingine zishtuke.

Kwa staili hii ushindani utatoka wapi?

Screenshot_2021-10-19-12-12-57.jpg
View attachment 1979593
 
Ushindani utatokana na quality of service
Pia mabadiliko ya bei hawaamui wao, regulatory authority wako nyuma ya mabadiliko unayoona, ni vile tu serikali haiwezi kutangaza hadharani kuwa inapandisha bei za huduma za mawasiliano. Ndio maana unaona mabadiliko yenyewe huwa yanafanana
 
Wale wanaji organise wamkabili mlaji japo kila kampuni inataka kuwapiku washindani wake, wanaona wasitofautiane sana ili wawe kitu kimoja pindi mmojawao atakapokabiliwa na magumu yake kama rungu la serikali likishuka miongoni mwao, halafu wanachotaka zaidi ni faida kubwa tu, japo yupo anaetamani kushusha gharama ili awe na wateja wengi ila anaogopa kusaliti wenzake
 
Hii inapelekea huduma ziwe mbovu
 
Back
Top Bottom