Mabadiliko ya uongozi kwa nchi za afrika hayaleti mabadiliko yoyote

chegreyson

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
974
434
Kuna kitu nakiona cha hatari kwa Watanzania wenzangu kwa tabia yetu ya kukurupuka,bila kuwa na utafiti au hata uchunguzi wa kina juu ya tunachokitaka.Kwanza nitoe angalizo kuwa mimi si shabiki au mwanachama wa chama cho chote cha siasa. Ila ni Mtanzania ninayeiombea mema nchi yangu pamoja wa watu wake.
Kwa kawaida sisi Watanzania huwa hatupimi viongozi wetu kwa kujua historia yao,pamoja na utendaji na ufanisi wao kikazi chama cha siasa kikimchaguwa mgombea hiyo ndio imetoka.
Mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu,asilimia kubwa ya Watanzania walifurahia uzuri wa sura wa mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais.
Hakuna aliyekuwa tayari kuchimba historia halisi ya mgombea, ili kuweza kujiridhisha juu ya usafi halisi wa mgombea pamoja na itikadi yake .
Tuliloliona ni watu wa media kumpamba mgombea huyo na akapambika,viongozi wa dini wakapata maono ya kuwa yule alikuwa ndiyo hasa changu la Mungu,na kwenye uchaguzi akashinda ushindi wa kimbunga.
Kuna kundi la watu wachache ambao walitaadharisha juu ya mgombea huyo aonekanavyo sivyo alivyo, na kwamba kila king'aacho sio dhahabu ,kama kawaida watu hao walionekana ni wasaliti na hawafai kusikilizwa katika jamii ya kitanzania.
Baada ya muda tukaanza kuona ugeugeu wa Watanzania na minong'ono ya hapa na pale juu wa uwezo wake,kwa vile matarajio yao hayakukudhiwa.
Leo hii uzuri wa sura hauonekani na wala hauzungumzwi tena kinachoonekana leo ni matatizo juu ya matatizo, mfumko wa bei juu ya mfumko wa bei, shida juu ya shida, malalamiko juu ya malamiko,migomo juu ya migomo.
Katika uteuzi wa wasaidizi wa rais , badala ya kumsaidia mkuu wa nchi kutekeleza ahadi za kampeni,tunashuhudia wakijiandaa kugombea urais miaka minne kabla ya wakati wake,kibaya zaidi hakuna aliye na nguvu za kuzuia.

Mada yangu ilianzia nyuma ili nijenge hoja ya kuwa kwa vile watawala wanaonekana kushindwa kuongoza, basi POLE POLE, BILA KISHINDO CCM INAUZA UTAWALA WAKE KWA CHADEMA.
Hili ndilo angalizo langu ni kuwa Watanzania tujiandae ana kwa machungu zaidi kwenye utawala mpya au kwa mazuri au ahuweni .
Utafiti niliuofanya unaonyesha ya kwamba hakuna nchi ya Kiafrika ambapo opposition imechukuwa madaraka wananchi wake wakawa afadhali kuliko watawala walioondolewa kwa njia ya kura.
Kenya opposition iliposhinda hali ya wananchi imekuwa mbaya zaidi ya Moi.
Zambia opposition imechukuwa utawala mara mbili,lakini hali ya maisha ya wananchi ni afadhali wakati wa Kaunda.
Malawi hali ni hiyo hiyo,Senegal hali ni kama Kenya,Ghana nayo hivyo hivyo na majina yataendelea.
Kwa bahati mbaya wengi wetu badala ya kuchangia kwa ajili ya kujenga ,tunaegemea matusi, kwa vile mawazo yako yanatofutiana na mtoa hoja.
 
Umeandika makala nzuri ila ingependeza kama heading ungeiandika hivi : Kwa mawazo yangu Mabadiliko ya uongozi kwa nchi za afrika hayaleti mabadiliko yo yote. Nasema hivyo kwa kuwa hayo ni mawazo binafsi na heading yako ime generalise mambo as if ni mawazo ya watu wengi ama as if ndio ukweli halisi.Sina maana ya kupingana na makala yako hapana.

Turudi kwenye makala yako, nikupongeze tena kwa uchambuzi ulioufanya mimi nimevutiwa sana na makala hiyo kwani ni kweli kuna tatizo kubwa kwenye mfumo wetu wa kuchagua viongozi na hasa kwenye vigezo sisi wananchi tunavyovitumia kumchagua kiongozi wetu, tumekuwa hatumchagui mtu ila tunachagua chama na hilo ni tatizo ifike mahala tumchague mtu kwa uwezo alionao sio kwa kuangalia sura ama chama ama jinsia ama kabila ama dini ama jambo jingine lolote lile ambalo halina tija katika kuonyesha ubora wa kiongozi.

Ila napata mashaka kidogo na makala yako hapo ulipotoa mifano ya Kenya, Zambia na Ghana sijui umetumia kigezo gani kusema kwamba katika nchi hizi hali imekuwa mbaya zaidi, unaposema hali imekuwa nzuri ama imekuwa mbaya kuna kuwa na vigezo fulani unavitumia labda ungeweza kusema kwa nchi hizo umetumia kigezo gani, si lengo langu kukosoa ila tunaelemishana.
 
Wanaume labda ukiwaambia ukichagua CCM utapungukiwa nguvu za kiume ndo wataacha kuichagua as ndo kitu muhim kwao kuliko kitu kingine,wanawake waambie mfuko wa Uzazi utahama,hakuna lugha unayoweza kuitumia wakakuelewa.umejifanya kutumia Akili za chuo chenu cha kivukoni kuwatisha watu wasichague upinzani.hivi kuna hali mbaya zaid ya hii mtu anaweza kuipata,hana ajira,maji,umeme,dawa,miundombinu,elimu,fursa za kujiajiri na njaa,hivi labda tumia siasa yako ya kivukoni kutushawishi hali mbaya zaid ya tuliyo nayo inakuaje? Tatizo kuu lililopo ni kushindwa kufanya kazi mifumo ya akili ya wa TZ
 
Back
Top Bottom