Mabadiliko ya Tabianchi na ukame/njaa Tanzania: Rais hazungumzi na wataalamu?

Je, wewe au ndugu yako/zako (sehemu fulani Tanzania) ame/wameathirika na njaa itokanayo na ukame?

  • Ndiyo, kuna njaa

    Votes: 2 100.0%
  • Hapana, hakuna njaa

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    2

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
Ni siku chache tu zilizopita tumemsikia Rais wetu akisisitiza kuwa hakuna njaa Tanzania bali ni wanasiasa na wafanyabiashara wanaonunua vyombo vya habari ili kupotosha. Amesema yeye tu ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza njaa. Tumemsikia pia akihoji kwa mshangao kuwa, wale wanaopoteza mifugo yao walikuwa wapi kuuza mifugo mpaka inakufa? Viongozi wake katika Kanisa lake Katoliki, wametoa tamko lao ambalo linakwenda kinyume na mamlaka yake. Pitia uzi huu hapa. Kanisa linapata wapi taarifa zake kiasi cha kuthubutu kupingana na mamlaka ya Rais? Ya Kaizari tumpe Kaizari au ya Mungu tumpe Mungu? Au Kaizari naye ni "mungu" mdogo?

Pia, ikumbukwe kuwa mwezi Agosti mwaka jana (2016) akiwa Sengerema mkoani Mwanza Rais alitoa agizo kuwa kwa miaka yake mitano serikali haitotoa chakula cha msaada kwa Wananchi wake kwa madai ya kukabiliwa na baa la njaa. (Chanzo: StarTV). Je, iwapo hali itazidi kuwa mbaya na nchi kuwa na baa la njaa (au kwa maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa chakula), serikali isipotoa chakula cha msaada, wahanga wafanyaje?

Wataalamu wa ndani mfano mamlaka ya hali ya hewa (Rejea ripoti ya TMA kuhusu msimu wa mvua za vuli hapa) pamoja na wataalamu wa Kilimo waliopo wizarani na wadau wengine ndani na nje ya serikali, uchambuzi wao (ushauri) haumfikii Rais? Mfano, taarifa za kituo cha utabiri wa tabianchi na mtazamo wa majanga Africa kupitia NOAA ya Marekani, kwa wiki hii hali bado inaonesha kuwa Tanzania kuna hali ya ukame na sehemu kubwa ikiwa kavu pasipo kawaida. (Tazama hapo nchini, chanzo hapa). Maana yake ni nini?

Mwisho, mabadiliko haya ya tabianchi (ambapo ukame/njaa ni miongoni mwa athari zake), Rais wetu ambaye ana wataalamu wa kutosha, je, hazungumzi nao? Kama anazungumza nao, ni kwa nini baadhi yetu tunaendelea kupanick?

Screen_Shot_2017_01_14_at_10_16_27_PM.png
 
Na amehoji tena, kuna njaa kwa hiyo tunataka atupikie?
 
Back
Top Bottom