Mabadiliko ya Sheria Subsection 47A kwenye Criminal Procedure Act (CPA) yanaenda kumuokoa Luteni Urio na Polisi wote wahusika kwenye kesi ya Mbowe

Mimi ni mwana CCM, Lakini kwanini tunabadili sheria kwa kuangalia manufaa ya wachache badala ya manufaa ya Taifa

Sheria inaweza kutumika kwa kurudi nyuma au kwenda mbele, mfano wa sheria zilizotumika kwa kurudi nyuma baada ya kutungwa ni sheria ya Bodi ya MIKOPO ya wanafunzi wa elimu ya juu( HESLB) hii iliathiri hata wale waliochukua mkopo zamani kuanza kulipa 15%

Sasa hii sheria mpya ikipita hasa Kipengele tajwa msije sema hatukusema au tunatetea ccm, Tutasimama na sheria irudi nyuma au iende mbele kwa matumizi

Kipengele cha Undercover kimeongezwa ghafla kwenye sheria ya Criminal procedure Act Cap 20 section 47 Subsection 47A, Lengo kuwa police waliohusika kwa siri kwenye uchunguzi wa uhalifu wasiwe sehemu ya uhalifu huo

Sheria inapasa iangalie mbele na sio kuangalia matukio ya watu wachache

Mapendekezo yanayopelekwa Bungeni tena kwa tangazo la Bunge la ghafla watu wakatoe maoni kwa siku moja Dodoma yanalenga kitu gani?

Someni mabadiliko hayo kwa umakini sana sana, Msije baadae mkaanza kulaumu Serikali.


View attachment 2105978


Serikali imepeleka Bungeni mabadiliko ya sheria mbalimbali, ni muhimu watu mkasome vizuri hizi sheria

Luteni Urio na wenzake baada ya kubanwa mahakamani ilionekana moja kwa moja wao ndio waliotengeneza hiyo picha ya kesi ya Mbowe kwa kuwatafuta Makomandoo ili wakafanye uharifu

Fuatilia vizuri Mahojiano ya Kibatala na Urio utangundua Urio anajitetea yeye kama Undercover

Kwa sheria hii ikipita Urio hiyo kesi haimuhusu anaokoka mapema sana, Ongezeko la neno Undercover kwenye sheria hii moja kwa moja Urio na wenzake hawahusiki na kesi hii ya Mbowe
ACHA ujinga MbowesioGaidi malipo Ni hapa hapa duniani litakutokea na wew usingiziwe Utajuta!mmbw wew
 
Precedence ya kusema uongo imeanzia CCM kwa mfano:
i.Fedha za ESCROW siyo za serikali.
ii.Uchumi wa Tanzania unapaa-uchumi wa kati chini.
iii.Nchi ya viwonder
iv.Tanzania ni tajiri.
v.Tutalipwa US$ 190 Bilion.
vi.etc
Vyote vikawa hewa.CCM Ph.D za uongo zimeenea.
Tahadhari-Watanzania sio wajinga!Wanafahamu tofauti kati ya ukweli na urongo wa kimfumo uliokithiri.Tumefikia hatua ya wananchi kuzuiwa na kuhofia kusema ukweli wa jambo lolote?
sina rais mpaka Leo hii simtambui😄
hamna la maana Wala halina ladha
I'm swear
 
Hivi hatuna bunge ni patikokasi + covid 19 huku tukiwalipa mahela mengi kwa kodi zetu toka jasho letu na damu zetu!!

#hatuna viongozi tuna mavi-ongozi.
...Yanaombwa yajipimie lkn yanakula kuvimbiwa
 
Ndugai alipoanza kuongelea haya mabadiliko ta sheria kwa hati ya dharula uspika wake ukafika kikomo. Nadhani huyu tununu nae atakuwa makini ili asije kosa ugali wake
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom