Mabadiliko ya Profesa Kabudi kwenye sheria ya madini yanalitesa Taifa. Nini kifanyike?

Umeleta kitu kizuri sana, ila umekosea sana kutumia lugha ya matusi kiasi kwamba sisi wazalendo umetufikirisha sana, na hasa ktk kipindi hiki cha mabeberu kuwatumia baadhi ya watanzania kupindisha ukweli. Kwa maoni ya watanzania wengi, acha madini yabaki, acha wanyonyaji waondoke ili tubaki na madini yetu kuliko ule mtindo wa kuibiwa. Prof Kabudi ni mzalendo sana na ndiyo maana hata mabeberu walimtafuta wamuue au wampe hela nyingi sana na hawakuweza maana vijana wa kazi walikuwa kazini 24/7. Pole mleta hii habari najua unaumia sana kwa sababu wezi tumewafukuza
Ndo matatizo ya kuamkia kwenye vijiwe vya kahawa,eti walitaka kumuua Kabudi!!!! Sht

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekaa nawaangalia Hawa wanao kushabikia na kukuunga mkono kwa hoja zako Yan mpaka sasaiv sijawaelewa niwaweke kund Gan sijui wajinga au watu wenye Chuki kiongozi namkumbuka pia kwenye makinikia uliongea kama unavyo ongea sasaiv sijui unaweza kutwambia juu ya makinikia serekal ilifaidika au iliboronga mana ulivyo chambua mwanzo havikutokea na wala hukuja kutuelewesha vip Leo umeamia kwenye mkataba na sheria za madin et hawatuibii dah unaitaji canceling ndugu Nan asie jua sheria za madin apo mwanzo zilikua hazitufaidish sis ila wawekezaj sheria ya madin dunia nzima kwenye nchi zilizo endelea unajua Gavament anatakiwa achukue asilimia ngapi? Au unaropoka tu na je unajua sis tulikua tunapewa asilimia ngap? Unatakiwa uwaambie watu haya sio kuwapotosha tu pia kitu muhim mtu Unatakiwa kufanya nikulinda eshima yako na thamn ya kitu chako et hawaib Kwan unafikir muwekezaj Hua anaibaje haibi ela wala rasilimali anakuibia kwenye maandish tu shenz wewe acha kudanganya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenifanya nimecheka mkuu, mchango wako nimeuona, nakushauri rudi darasani ukajifunze kuandika kwanza kabla ya kujibu hoja ngumu kama hii. Ccm ni wajinga sana, mnaajiri kilaza kama huyu kuwatetea????!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeweza kusoma sehemu ndogo tu unayosema wachimbaji wadogo hutegemea utafiti wa haya makampuni makubwa ndipo na wao waanze kuchimba.

Hivi kwa mfano madini yanayochimbwa Morogoro na wachimbaji wadogo haya makampuni makubwa ndio yaliwasaidia kufanya utafiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliposoma ulielewa lakini? Nakushauri karudie kusoma tena na kama hautoelewa basi hii siyo size yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenifanya nimecheka mkuu, mchango wako nimeuona, nakushauri rudi darasani ukajifunze kuandika kwanza kabla ya kujibu hoja ngumu kama hii. Ccm ni wajinga sana, mnaajiri kilaza kama huyu kuwatetea????!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnapokuaga mnafel siku zote ni kujiona mnajua Sana na mmesoma Sana ndiomana mnafel alafu kila dalili inaonesha mnachambua mambo kisiasa na kwa Upande wa chama ndio mana mnaropoka tu mtu akiwa tofaut na nyie bas yeye ni ccm so hii inaonesha mmeleta hoja umu kuiponda ccm sio kujenga hoja nimekuuliza swal juu uko kuhusu makinikia Lakin naona unakimbia kiambia polen Sana ila mjue ccm mnayoiita wajinga inawatala mwaka wa 53sassiv nyie na Elim zenu kazi kutunga hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waweza kuwa siyo mwana ccm lakini uwezo wako ni sawa na hao ccm, sidhani kama kuwa na uwezo sawa na ccm ni tusi/ kosa
Mnapokuaga mnafel siku zote ni kujiona mnajua Sana na mmesoma Sana ndiomana mnafel alafu kila dalili inaonesha mnachambua mambo kisiasa na kwa Upande wa chama ndio mana mnaropoka tu mtu akiwa tofaut na nyie bas yeye ni ccm so hii inaonesha mmeleta hoja umu kuiponda ccm sio kujenga hoja nimekuuliza swal juu uko kuhusu makinikia Lakin naona unakimbia kiambia polen Sana ila mjue ccm mnayoiita wajinga inawatala mwaka wa 53sassiv nyie na Elim zenu kazi kutunga hoja

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsnte kwa kutushirikisha utaalamu wako.Hakika wewe ni moja kati ya watu muhimu katika sekta hii ya madini hapa nchini.Tumeona nchi kama Botswana zikifaidika ipasavyo na madini yake ya Diamonds, hata kufikia hatua ya kuyataka makampuni yanayochimba diamonds kufanyia stahiki transaction zake katika mabenki ya botswana hivo kuwa na mfumo mzuri wa kuwakeep in check.Hiyo sheria sisi hatukuwa nayo.lakin sasa tunayo.Na kingine ni juu ya usafirishaji wa makinikia.umetuambia kuwa kusafirisha makinikia ni aghali sana lakini Acacia walisafirisha kwa miaka 17 na hawakuwahi kufikiria kuanzisha smelters nchini!! Ni kwamba Acacia walikuwa wanapenda kupata hasara?
Umetoa mfano mzuri wa Botswana. Botswana ni kati ya nchi zenye mfumo mzuri sana na rafiki kwa pande zote, serikali na wawekezaji. Kila mmoja ananufaika. Na wawekezaji wanavutiwa na mazingira ya Botswana.

Botswana, kwenye baadhi ya miradi, serikali inamiliki mpaka 40%. Tofauti yao kubwa na sisi, Botswana asilimia zake inazomiliki kwenye miradi ya madini, wamezilipia. Sisi kwa sheria ya 2010, hisa zetu za 10% ni za bure (free carriwd shares). Kwa sasa tumeweka 16% free shares. Hapo Uganda kwenye mradi wa mafuta, serikali ina 15% lakini ni hisa za kulipia. Hawalipii mwanzo wa mradi bali watalipia kwa kukata malipo ya kodi ambayo mwekezaji angelipa serikalini. Nadhani umeona tofauti.

Kwenye suala la makinikia, sidhani kama nimesema usafirishaji wa makinikia ni aghali sana. Nilichoeleza ni kuwa migodi mingi katika mataifa mbalimbali, yenye refractory gold, wanapeleka concentrates mataifa ya nje, hasa Japan. Makampuni yanayopeleka concentrates nje, yanafanya hivyo kwa kuangalia economics of scale. Nikuuliza tu swali dogo, hivi ukiwa na shamba lako la mahindi. Ukavuna magunia 8, na unataka kupata unga wa mahindi kutoka kwenye magunia yako 8, utaamua kununua mashine ya kusaga, au utayapeleka kwa mwenye mshine ya kusaga ili ukayasage mahindi yako na kupata unga? Unajua ni kwa nini mpaka sasa hakuna concentrates zinazokuwa processed nchini?

Botswana kuyataka makampuni kutumia mabenki ya ndani, siyo kwa sababu walikuwa wanataka kuchunguza usafirishaji fedha. Lengo kuu ilikuwa ni kuongeza ushiriki wa sekta ya madini katika biashara ya ndani. Na imesaidia sana kuhuisha sekta ya fedha na sekta nyingine za uchumi kwa kuwezesha kuwepo fedha nyingi ya kigeni ndani ya nchi yao. Kucopy takwa hilo ni jambo zuri.

Lakini ufahamu pia, hitaji hili lilikuwepo enzi za Mwalimu, baadaye liliondolewa ili kuvutia uwekezaji. Maana baada ya ule utaifishaji wa 1967, hakuna mwekezaji mkubwa aliyekuwa anataka kuja kuwekeza Tanzania. Wengi walikuwa na hofu ya mali zao na fedha yao, siku moja ingeweza kutaifishwa na serikali.

Kasoro ninazoziona kwenye mabadiliko ya sheria ya madini nimeorodhesha.

Mabadiliko ni muhimu kuwepo kwa jamii yoyote inayobadilika lakini hayatakiwa kufanywa kwa dhamira njema na kwa namna iliyo njema pia. Mwekezaji siyo jambazi bali ni patner in your development. Kwa nini kusiwepo na majadiliano rafiki na partner wako? Kila mmoja anamhitaji mwingine, kwa nini ukweli huo usitambuliwe, na kila kinachofanyika kikaenda kwa mtazamo huo?

Mpaka leo hii, makampuni 3 ya madini yaliyonyang'anywa retention licenses zao bila ya kuelezwa wamekosea nini, yametoa notisi kwa serikali ya kusudio la kuifikisha serikali kwenye mahakama za kimataifa. Lakini, hivi kweli kulikuwa na haja ya kufika huko kama tungetumia busara? Ukiona unashtakiwa sana au unapenda kushtaki sana, ujue umepungukiwa na uwezo wa kidiplomasia. Leseni zile nyingine zilibakiza miezi 6 zimalize muda wake. Hivi tulishindwa tu kusibiri hiyo miezi 6 leseni zao zimalize muda wao, kisha wanapoomba leseni tena, tuwape kwa sheria mpya?
 
Hapo nimekuelewa mtaalamu! Hapo mwanzo tulikuwa na tatizo la sheria dhaifu na zisizosimamiwa vizuri lakin hivi sasa tuna tatizo la sheria kali kupitiliza.Haya yote ni matatzo! Tunahitajika kufanya kitu kwa sasa ili kuleta faida kwa pande zote mbili.lakini pia inabidi tufahamu kuwa serikali inafanya mabadiliko haya sio kwa lengo la kukomoa, bali kuhakikisha tunapata fair share! So wakati mwingine kutumia lugha za kejeli na zenye ukali ni jambo baya!!
 
Unachoongea kinatuingia akilini sema wabongo muda mwingine Ni Kama binti wa kisukuma. Katika haya maamuzi Kuna mtu hakutumia hekima aidha kwa makusudi au kwa upumbavu. Haingii akilini unafuta leseni iliyobakiza miezi sita kuisha.

Pia lipo tatizo la misukumo ya kisiasa hasa wapinzani kuwajengea watu Imani potofu kuwa tunaibiwa wakati wanajua sio kweli na watawala wanapata shida kuwaambia wananchi ukweli. Hili la makinikia Lissu alilivalia njuga tangu akiwa LEAT na Rugemarila nchala na watu waliamini maneno ya uongo ya nchala na mpuuzi mwenzie Lissu kibaya na watu waliopewa madaraka nao wakaja na sumu ileile waliolishwa na akina Lissu.
 
Kwa haya maelezo kama bado hajakuelewa ana tatizo tena kubwa.
 
..mnamsingizia TL bila sababu ya msingi.

..TL alionya serikali isichukue hatua za jazba na pupa.

..badala yake mkamuita msaliti na akapigwa risasi.

..TL alionya kwamba tuwe waangalifu tutashitakiwa.

..mawaziri na wabunge wa ccm wakawa wanajigamba kwamba hawaogopi kushtakiwa.
 
Bams ahsante sana kwa andiko zuri lenye elimu toshelevu juu ya tasnia hii ya madini. Nisichokubaliana nawewe ni kumlaumi Mh Prof. Kabudi kuhusiana na sheria mpya ya madini; kwa mtazamo wangu na kwa mujibu wa kazi za mihimili mitatu, wa kulaumiwa kama hiyo sheria ina matokeo hasi ni Bunge la Jamhuri ya Tanzania. Kupitia kamati zake na michango ya Mbunge mmoja mmoja, Bunge lilikuwa na uwezo wa kurekebisha mswada na kuja na sheria yenye matokeo chanya kwa uchumi wa Taifa letu au kuukataa kabisa ukiwa bado muswada.
Bunge lipi unaloongelea? Hili ambalo wazi kabisa linaambiwa kuwa mzizi wake haukujichimbia zaidi? Au lingine?
 
Nimekaa nawaangalia Hawa wanao kushabikia na kukuunga mkono kwa hoja zako Yan mpaka sasaiv sijawaelewa niwaweke kund Gan sijui wajinga au watu wenye Chuki kiongozi namkumbuka pia kwenye makinikia uliongea kama unavyo ongea sasaiv sijui unaweza kutwambia juu ya makinikia serekal ilifaidika au iliboronga mana ulivyo chambua mwanzo havikutokea na wala hukuja kutuelewesha vip Leo umeamia kwenye mkataba na sheria za madin et hawatuibii dah unaitaji canceling ndugu Nan asie jua sheria za madin apo mwanzo zilikua hazitufaidish sis ila wawekezaj sheria ya madin dunia nzima kwenye nchi zilizo endelea unajua Gavament anatakiwa achukue asilimia ngapi? Au unaropoka tu na je unajua sis tulikua tunapewa asilimia ngap? Unatakiwa uwaambie watu haya sio kuwapotosha tu pia kitu muhim mtu Unatakiwa kufanya nikulinda eshima yako na thamn ya kitu chako et hawaib Kwan unafikir muwekezaj Hua anaibaje haibi ela wala rasilimali anakuibia kwenye maandish tu shenz wewe acha kudanganya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesoma au umekurupuka, matusi ya nini? Maswali yako yote yameshajibiwa, tuliza akili soma uelewe acha jazba.
Sio kila hoja ni propaganda.
 
Ahsnte kwa kutushirikisha utaalamu wako.Hakika wewe ni moja kati ya watu muhimu katika sekta hii ya madini hapa nchini.Tumeona nchi kama Botswana zikifaidika ipasavyo na madini yake ya Diamonds, hata kufikia hatua ya kuyataka makampuni yanayochimba diamonds kufanyia stahiki transaction zake katika mabenki ya botswana hivo kuwa na mfumo mzuri wa kuwakeep in check.Hiyo sheria sisi hatukuwa nayo.lakin sasa tunayo.Na kingine ni juu ya usafirishaji wa makinikia.umetuambia kuwa kusafirisha makinikia ni aghali sana lakini Acacia walisafirisha kwa miaka 17 na hawakuwahi kufikiria kuanzisha smelters nchini!! Ni kwamba Acacia walikuwa wanapenda kupata hasara?

Fuatilia hii thread liko jibu la swali lako, usione uvivu kusoma upate maarifa.
 
mleta mada usikatishwe tamaa na wachache! kuna watu wapo kwa ajili ya kusifu tuu!

mfano mdogo ukiwauliza watanzania waliowengi wanajua kwa nini wahindi hawajengi wanapanga nyumba? atakwambia ni wabahili! asijue wanaogopa yaliyotokea miaka ya 80 waliponyang’anywa nyumba zao! yes kwa wakati ule tulishangilia kupata nyumba za bure! je nini kinaendelea kwenye secta ya nyumba nchini??

athari za sasa tunaweza ziona miaka kumi baadaye.
hawa waliopo wanaweza endelea kujikongoja ili warudishe pesa zao. mikataba ikiisha wanasepa na hatupati wapya
 
Katika awamu hii kuna sekta nyingi zimeharibiwa badala ya kuboreshwa ili ziwe na mchango chanya kwenye uchumi na maisha ya Wananchi.

Kusipofanyika mabadiliko ya haraka, kadiri tutakavyoenda, kila mwananchi, hata mwenye mwenye akili ya kawaida kabisa, atapata jibu kama tupo kwenye njia sahihi au tunaelekea shimoni.

Kati ya sekta zilizoharibiwa sana ni sekta ya madini. Hii sekta kabla ya uharibifu ilikuwa inaongoza kwa ukuuaji na uingizaji wa fedha za kigeni. Sekta hii iliharibiwa zaidi na mabadiliko ya sheria ya madini yaliyoandaliwa na kusukumwa kwa kiasi kikubwa na Prof. Kabudi, ambayo aliyafanya bila ya kushirikisha wadau wa sekta na wataalam wa Wizara ya madini kikamilifu.

Kabla sijaenda kwenye makosa yaliyofanyika, napenda nieleze wazi kuwa mimi ni mtaalam mwanasayansi kwenye sekta hii ya madini wa kiwango cha kimataifa ambaye nimekuwa nikijishughulika na usimamizi, uendeshaji, upatikanaji wa miradi ya madini katika nchi nyingi. Lakini pia nimekuwa nikishiriki kwenye upatikanaji wa mitaji kutoka soko la mitaji la Australian Securities Exchange (ASX) kwaajili ya uwekezaji kwenye miradi ya madini. ASX ndiyo soko kubwa kabisa Duniani kwaajili ya upatikanaji wa fedha za kuwekeza kwenye miradi ya madini. Ni kwa kupitia soko hili, matajiri wa mataifa kama Singapore, Hong Kong, Japan na Malaysia, huweza kuwekeza katika miradi ya madini iliyopo Afrika. Kwa hiyo ukilikosa soko la Hisa la Australia, utakuwa umekosa mitaji kutoka mataifa mengi, na siyo Australia pekee yake.

Madini yapo mataifa mengi Duniani. Na kila wakati madini hugundulika. Leo hii hata mataifa ambayo hapo awali hayakuwahi kufikiriwa kuwa na dhahabu, kutokana na teknolojia kukua ugunduzi wa migodi mipya umekuwa ukipatikana katika mataifa hayo.

Tanzania hatuna madini ya aina yoyote ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani. Madini pekee ambayo tumekuwa tukizungumzia kuwepo Tanzania tu ni Tanzanite lakini kitaalam huwezi kusema kuwa madini ya Tanzanite hayapo mahali pengine Duniani. Tanzanite ni sapphire ambayo tofauti na sapphire nyingine, yenyewe ndani yake ina vanadium. Na wala Tanzania, katika uzalishaji wa dhahabu, hatuyakaribii mataifa kama ya China, Australia, South Africa, Peru, Mexico, Brazil, US, Russia au Indonesia. Nimeyasema haya ili Watanzania, na watu wengine kama akina Prof. Kabudi wajue kuwa hatupo pekee yetu Duniani wenye madini, na wala Dunia haiwezi kusimama kwa sababu hawatapata madini toka Tanzania.

Kutokana na uwepo wa madini katika mataifa mbalimbali Duniani, mataifa yote yamekuwa yakinyang'anyana wawekezaji wale wale wakubwa waliopo Duniani - New mont, Barrick, Anglogold, Kinross, Newcrest, Freeport, Polyus na Goldcorp. Ili uweze kuijenga sekta yako ya madini, kama Taifa, ni lazima uwe na wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya madini, na hawa kwa Dunia nzima hawazidi makampuni 15 hivi. Utafiti ni gharama kubwa, na risk ya kupoteza pesa ni zaidi ya 95%. Ni hawa wenye mitaji mikubwa tu ndio wanaoweza kugharamia utafiti. Hawa ndio hufanya utafiti, na pale wanapopata resources ndogo, huziacha kwaajili ya makampuni madogo, na kwa hapa Tanzania maeneo hayo mara nyingi huvamiwa na wachimbaji wadogo.

Kuna watu kutokana na kukosa uelewa wa sekta hii, hudiriki hata kusema kuwa makampuni yamekuwa yakiwafuata wachimbaji wadogo, wakati ukweli ni kinyume chake. Huwa hawaujui ukweli kwa sababu huwa hawajui makampuni yalianza utafiti kwenye maeneo husika wakati gani. Na kwa vile mchimbaji mdogo anapovamia tu huanza kuchimba, watu humtazama anayechimba bila ya kumtazama aliyetafiti alianza lini. Kwa hiyo usipokuwa na makampuni makubwa, makampuni madogo hufa, na sekta ya uchimbaji mdogo nayo hufifia kabisa maana wao hawafanyi utafiti, na hawatapata mahali pa kuvamia.

Makosa aliyoyafanya Kabudi Kwenye Mabadiliko ya Sheria:

1) Masharti Magumu ya Kufanya Utafiti
Utafiti ni risk kubwa. ndiyo maana dunia nzima anayefanya utafiti wa madini hubembelezwa na siyo kumburuza. Kabudi kwenye mabadiliko ya sheria ameweka utaratibu wa kutosafirisha sampuli za madini kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine bila ya kibali cha afisa wa madini mkazi. Maabara ya madini inayotambulika Tanzania ipo moja tu kwa sasa, SGS. Mara ya kwanza maabara za madini zilikuwa kama 4 hivi, na zote zilikuwa Mwanza. Zote kwa sasa zimeondoka, imebakia 1. Unapofanya utafiti kama wa drilling, unahitaji activities continuity, na hivyo samples hutakiwa kupelekwa maabara wakati wote, usiku na mchana. Kuisimamisha rig kusubiria majibu ya maabara, gharama yake huwa ni dola 400 kwa saa. Kabudi anataka usipeleke samples maabara usiku wala siku za mapumziko kwa sababu huwezi kupata kibali. Maana yake ulipe zaidi ya dola 9,000 kwa siku kwa kusimamisha rig. Lakini hiyo sheria ililenga nini? Najua yeye alifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia samples. Jambo ambalo kwa mtu anayejua kinachofanyika, fikra hizo ni za kijinga kabisa maana ni jambo lisilowezekana. Ufafanuzi wake unaweza kuwa makala nyingine.

2) Kufuta Reetention Licenses
Kufuta Retention licenses, nao ulikuwa ni upuuzi wa hali ya juu. Serikali iliweka aina hii ya leseni ili kuyapa nafasi makampuni ambayo yamefanya utafiti na kufikia muda wa kuanza kujenga migodi lakini muda wa leseni zao au umeisha au ni mfupi kiasi cha kutotosheleza kufanya taratibu za kupata leseni ya uchimbaji. Leseni hizi zilitolewa kwa kipindi cha miaka 2 tu na ziliweza kurudiwa kwa kipindi kimoja tu, baada ya hapo ni ama unaanzisha mgodi au unalirudisha eneo serikalini. Serikali ilipendelea zaidi kutoa leseni hizi kuliko kutoa extension kwa sababu annual rent ya leseni hii ilikuwa dola 2,000 kwa kila square kilometre kwa mwaka, ukilinganisha na dola 100 kwa square kilometre kwa mwaka kwa leseni za utafiti. Leseni nyingi za retention zilikuwa na ukubwa wa kati ya square kilometre 10 - 30. Hivyo makampuni yalikuwa yakilipa kati ya dola 20,000 - 60,000 kwa mwaka kwaajili ya leseni tu. Mwekezaji amepewa leseni ya awali, ametumia mamilioni ya dola kufanya utafiti, umempa Retention License, tena mara nyingi kwa kumshahwishi, amekuwa akilipa ada zote, wengine walibakiza miezi tu Retention Licenses zao ziishe, ghafla unafuta leseni ambazo zilikuwepo kwa mujibu wa sheria yenu, unawanyang'anya haki yao uliowapa, na kwa mujibu wa sheria yako hawajavunja sheria yoyote - hiki ni nini, kama siyo ujambazi katika biashara na uwekezaji? Kutokana na tendo la kuwanyang'anya wawekezaji leseni zao bila haki yoyote, na kuzuia usafirishaji wa makinikia kwa sababu za uwongo kuwa kulikuwa na dhahabu inayoibiwa, Tanzania kwenye soko la hisa la ASX, ilitajwa rasmi kama siyo mahali salama kwa uwekezaji wa mitaji ya nje. Leo hii huwezi kupata fedha kwenye masoko makubwa ya fedha Duniani kwaajili ya kuja kuwekeza Tanzania. Unaweza kupata fedha kidogo kutoka kwa matajiri binafsi lakini siyo kutoka kwenye masoko ya fedha.

3) Utaratibu Sumbufu wa Kupeleka Sampuli Maabara za Nje
Kabudi kwenye sheria mpya, aliondoa utarattibu wa zamani ambao maabara za maandalizi zilikuwa zikiandaa sampuli zinazotakiwa kwenda nje ya nchi na kufuata taratibu za customs kwaajili ya kuzipeleka nje. Kwa sasa, ni lazima kwanza zipitie GST halafu ziende customs. Hizi samples, zile kwaajili ya Fire Assay au Aqua Regia (sample pulps) kila moja huwa na uzito wa 50 - 100gm; na zile kwaajili ya MET huwa kati ya 2 - 20kg kila moja. Lakini kwa nini uweke huo utaratibu mgumu? Maana kila ukiritimba unaouweka unaongeza business cost. Sababu ni ujinga ule ule kuamini kuwa kuna wizi wa madini unafanyika kupitia sampuli za madini. Ni fikra za kijinga kabisa za mtu asiyejua nini huwa kinafanyika kwenye suala la samples. Ni mada nyingine, kuna wakati nitaelezea.

4) Kodi za Ajabu
Hapo awali tulikuwa tunatoza mrabaha wa 3%, corporate tax ya 30%. Kikwete alikuja kuongeza mrabaha kwa kupitia majadiliano rafiki, mpaka kufikia 4%. Kabudi akapandisha kwa ubabe bila majadiliano mpaka 7%. Kwa nini alifanya hivyo? Nadhani aliamini kuwa 4% ni ndogo mno. Lakini nchi nyingine zinatoza nini? Mataifa karibu yote Mineral Royalty ni 0 - 5% tu. Ni Zimbabwe pekee yake ndiyo inayotoza 7%. Na hii inatozwa kwenye gross production value, haijalishi umepata faida au hasara. Kama mataifa mengine yanatoza kati ya 0 - 5%, kwa nini sisi tuliokuwa tunatoza 4% tuone kuwa tumekuwa tunaibiwa? Kwenye corporate tax, nchi nyingi zinatoza 20 - 30%. Zimbabwe wanatoza 28%. Kwa nini sisi tuliokuwa tunatoza 30% tuone kuwa tulikuwa tunaonewa? Naamini tuliongozwa na ujinga zaidi kuliko weledi.

5) Kufuta Usafirishaji wa Makinikia (Mineral Concentrate)
Kabudi kwenye mabadiliko ya sheria alifuta usafirishaji wa concentrates. Kwa nini alifuta? Naamini pia ni kwa sababu ya ujinga na kutotaka kushirikisha wataalam wa sekta hii. Kwanza hakuna kampuni inayopenda kusafirisha concentrates. Aina ya ore material, hasa inapokuwa na sulphides, humlazimisha mchimbaji kutafuta njia ya kuchenjua dhahabu inayokuwa imebanwa kwenye sulphides, na ambayo haitoki kwa njia za kawaida zilizozoeleka. Unatoa dhahabu huru (free gold), na ile iliyokuwa locked in, unafanya floatation kwa nia ya kutengeneza concetrates zitakazokuwa na dhahabu nyingi (mara nyingi ni kati ya 100 - 300g/ton, na siyo ule upuuzi walioutaja watu wa bandari kuwa concetrates zilikuwa na dhahabu 90%). Hiki ni kitu kinachofanyika Duniani kote. Zambia, Canada, Indonesia, Australia, Mali, Ghana, Brazil, etc, wote wanapeleka concentrates zao, hasa Japan. Kama hawa wote wanasafirisha concentrates, ni sababu gani inayotufanya sisi pekee yetu tuamini kuwa hawa wengine wote hawaibiwi isipokuwa sisi tu? Athari ya sheria ile mbaya ya Kabudi, deposits zote zenye refractory gold hazitaweza kuja kuwa migodi. Siku zote, kazi ya serikali inayoongozwa na watu wenye hekima ni kujenga mifumo na kuweka taratibu zinazorahisisha na kupunguza gharama za uwkezaji na biashara huku ikiangalia faida pana ya wadau wote.

6) Data Zote za Utafiti Kupelekwa Serikalini
Kabudi kwenye sheria yake ya mabadiliko, anayalazimisha makampuni yote yanayofanya utafiti nchini, kupeleka data za utafiti GST. Jambo hili halipo Duniani kote. Utafiti ni risk kubwa na ni gharama kubwa, na pia ni confidential information. Kampuni ya utafiti wa madini, asset yake kubwa ni data za utafiti. Ni hizo data ndiyo zimeifanya kampuni kutumia mamilioni ya dola. Wewe unasema wafanye utafiti, data wakupe wewe!! Haijawahi kusikika. Utaratibu uliopo mataifa mengi Duniani, kampuni hufanya utafiti, wakiamua kuanzisha mgodi, data zinaendelea kuwa zao, Wakiamua kulirudisha eneo serikalini, wanarudisha eneo, na wanaipatia serikali data zote. Kuyataka makampuni kukabidhi GST raw data ni kati ya hitaji la ovyo kabisa kuwahi kuwepo katika ulimwengu huu.

Makosa haya makubwa yaliyofanywa na Prof. Kabudi yana athari zifuatazo:

1) Taswira Mbaya ya Mazingira ya Uwekezaji ya Nchi Yetu
Leo huwezi kuwapata wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania. Katika kipindi chote cha awamu hii, hakuna mwekezaji mkubwa (>U$500m), aliyeweza kuwekeza Tanzania, awe wa ndani au wa nje.

2) Kifo cha Makampuni
Makampuni yote ya madini yaliyowekeza Tanzania na ambayo yanafanya biashara kwenye masoko makubwa ya fedha, kutokana na mabadiliko yale ya Kabudi yalipoteza kati ya 30 - 60% kwenye capitalization ya makampuni kwa sababu yamewekeza kwenye mazingira hatarishi ya mitaji. Kupoteza capitalization ya kiasi hicho ni kuua kampuni. Makamuni haya yote, kwa kiasi kikubwa yameondoka Tanzania na mengine yamebakia tu kwenye vitabu vya serikali lakini kiuhalisia yameondoka na hayafanyi chochote nchini

3) Kulipa Fidia
Makampuni yote yaliyonyang'anywa maeneo kwa kufutiwa Retention Licenses zao, karibia yote yatataka kulipwa fidia na serikali au kufungua kesi za fidia kwenye mahakama za kimataifa. Tayari makampuni mawili yameipelekea notice serikali. Hata kwa mimi nisiye mwanasheria, nina uhakika wa over 99% kuwa serikali itashindwa katika kesi zote zitakazofunguliwa, na hivyo kutakiwa kulipa fidia

4) Kupungua kwa Mapato ya Serikali
Makampuni makubwa yanayochimba dhahabu kwa sasa, yataendelea kuwa hayo hayo. Lakini makampuni hayo yana uwezekano mkubwa wa kufunga migodi yao mapema zaidi kuliko muda uliotarajiwa kutokana na kuongezeka kwa gharama. Makampuni haya imebidi kuweka cutoff grades mpya ili kuendana na gharama za uzalishaji zinazochangiwa na kodi na tozo kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa. Na wala hakutakuja kuwa na miradi mikubwa mipya.

5) Kudumaa kwa Technology Transfer
Ujio wa makampuni makubwa kabisa yanayotumia teknolojia za kisasa kama Barrick na Anglogold, ulifanya watanzania wengi kupata teknolojia ya juu na ya kisasa kabisa Duniani. Leo hii, nchi zinazoongoza katika utaalam wa madini Afrika, ni South Africa, Ghana kisha Tanzania. Leo hii Watanzania wapo kwenye nafasi za juu kwenye miradi ya madini katika mataifa mbalimbali. Kuondoka kwa makampuni haya makubwa, kutalifanya Taifa kwenda kwenye udumavu wa maarifa kama ilivyokuwa zamani. Katika utaalam, wataalam wa Tanzania kwenye sekta hii, wapo juu maradufu kuzidi wataalam kutoka mataifa kama vile China. Mimi binafsi nimekuwa nikizunguka, pamoja na kazi nyingine, lakini nimekuwa nikitoa mafunzo kwa wataalam wa sekta hii. Wakati mmoja nilipokuwa nikitoa mafunzo kwenye mgodi mmoja wa Waingereza, nilikuwa na wanafunzi 84, na kati ya hao Waafrika walikuwa 29, Waingereza 34, Wairan 2, Waaustralia 2, Wacanada 3, Wachina 3, Wavietinam 5, Waindonesia 6

6) Athari nyinginezo
Nyingine ni zile za kawaida ambazo kila mwenye ABC ya uchumi anazijua - kama vile kupungua kwa ajira, business interactions, na uchangamshashaji wa uchumi, kupungua kwa fedha za kigeni (sekta hii na ya utalii ndizo zinazoingiza fedha za kigeni nyingi kuliko sekta nyingine zote)

NINI KIFANYIKE
1) Kufutwa kwa Mabadiliko
Sheria ile mpya ya Kabudi ifutwe. Na kama kuna haja ya kufanya mabadiliko, yafanyike kwa kushirikisha wadau wote, na yafanyike kwa njia ya maelewano

2) Retention Licenses Zirudishwe
Wamiliki wa Retention Licenses warudishiwe, na wapewe muda wa ama kujenga migodi au kuyarudisha maeneo wanayoyamiliki kwa serikali. Hata wauaji hupelekwa mahakamani kujitetea, lakini Retention License holders, walinyang'anywa rights zao bila ya kupewa sababu, kupewa nafasi ya kurekebisha, kama kweli kulikuwa na makosa.

3) Majadiliano Rafiki
Wamiliki wa Retention Licenses wanaokusudia kuifikisha serikali/nchi kwenye mahakama za usuluhishi za kimataifa ili kulipwa fidia waalikwe kwenye mazungumzo ili wasifanye wanachotarajia kukifanya. Serikali ikiri ilifanya kosa, na iombe ikubaliwe kutolipa fidia yoyote kwa wawekezaji walioathirika na uamuzi wa kuwanyang'anya leseni zao kinyume cha sheria.

4) Wadau Wataalam Watoe Muongozo
Kama nilivyoeleza, sekta hii ina Watanzania wataalam waliobobea, na walioenea Duniani kote, wao kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara, watoe mwongozo kwa serikali namna ya kuihuisha sekta hii baada ya kuidumaza kwa miaka hii minne kutokana na mabadiliko Kabudi. Wataalam hawa watumike kufikisha kwenye masoko ya fedha Duniani na taasisi mbalimbali za kimataifa, kufutwa kwa mabadiliko yaliyoiharibu sekta. Jambo hili siyo geni. Huko Australia, kuna Waziri mkuu mmoja alianzisha Mining Super Profit Tax. Mwanzoni wananchi walimshangilia. Baadaye madhara yalipoanza, wananchi walimchukia Waziri Mkuu na kumwondoa madarakani. Waziri Mkuu mpya akaifuta hiyo kodi, na baada ya muda sekta ya madini ilirejea kwenye utengamano.

JUMUISHO

1) Kuwa msikivu na hekima, siyo unyonge au udhaifu, sawa kama ilivyo, kuwa katili siyo ushujaa

2) Hakuna nchi hata moja iliyowahi kuendelea kwa kuwategemea watu wake tu. Mchangamano wa watu, makampuni na taasisi za mataifa mbalimbali ndiyo hujenga Taifa ka kasi. Mfano mzuri wa karibu ni Dubai, South Africa, Nigeria, Botswana. Kwa upande mwingine, tujifunze toka China. China chini ya kiongozi wao Mao, na mfumo wao wa Maoism, uchumi wao ulikuwa wa kujifungia. Miaka yote waliendelea kuwa Taifa duni, hata nguo wakivaa zenye viraka magotini na makalioni. Mwishoni walirejewa na akili, wakaufungua uchumi wao kwa Dunia. Makampuni ya America na Ulaya, yakawekeza huko kupindukia, hata kuufanya uchumi wa China kupaa. Ni uwekezaji huo ndio ulioingia na teknolojia ambayo Wachina mpaka leo wamekuwa wakiiga kwa kasi kubwa. Japo makampuni makubwa yaliyopo China hayamilikiwi na Wachina, lakini makampuni hayo yameifanya China kukua kwa kasi kiuchumi na kitekinolojia.
Kunywa glasi ya maziwa mbuzi kila siku ili upate afya njema uendelee kutuletea vitu vyenye afya kama hivi vya Leo. Uzi umetulia na ni elimishi
 
..mnamsingizia TL bila sababu ya msingi.

..TL alionya serikali isichukue hatua za jazba na pupa.

..badala yake mkamuita msaliti na akapigwa risasi.

..TL alionya kwamba tuwe waangalifu tutashitakiwa.

..mawaziri na wabunge wa ccm wakawa wanajigamba kwamba hawaogopi kushtakiwa.
Alitoa tahadhari kwasababu alishajua alishatudanganya na tukaamini uongo wake, Lissu na Zitto walizumguka nchi nzima wakiwaambia wananchi kuwa mkataba wa buzwagi Ni batili na ulisainiwa na waziri akiwa bar London. Huyohuyo Zitto alifadhiliwa ujenzi wa shule jimboni kwake akanyamaza kimya ka sio yeye.

Lissu huyuhuyu alidukuliwa kwenye simu yake akiwapigia simu maofisa wa juu wa acacia. Yaani matapeli matupu
 
Hapo nimekuelewa mtaalamu! Hapo mwanzo tulikuwa na tatizo la sheria dhaifu na zisizosimamiwa vizuri lakin hivi sasa tuna tatizo la sheria kali kupitiliza.Haya yote ni matatzo! Tunahitajika kufanya kitu kwa sasa ili kuleta faida kwa pande zote mbili.lakini pia inabidi tufahamu kuwa serikali inafanya mabadiliko haya sio kwa lengo la kukomoa, bali kuhakikisha tunapata fair share! So wakati mwingine kutumia lugha za kejeli na zenye ukali ni jambo baya!!
Mkuu Hawa jamaa wa migodini Wana dharau sana, sishangai huyu jamaa kutumia lugha ya kejeli anasau hata JPM yumo humu na anasoma comments na ana like pia.

Kwanza kwenye uchaguzi 2015 walimponda mawe mama Samia pale kakola akina Ray shilole na jokate walikimbilia hotel ya Jensen Hadi ffu walivyokuja kuwaokoa, JPM hakupiga kampeni Bulyanhulu kwa hofu yakufanyiwa fujo. Lowasa nae hakwenda pale kwa hofu ileile, mjifunze siku nyingine mjue Kuna kesho
 
Alitoa tahadhari kwasababu alishajua alishatudanganya na tukaamini uongo wake, Lissu na Zitto walizumguka nchi nzima wakiwaambia wananchi kuwa mkataba wa buzwagi Ni batili na ulisainiwa na waziri akiwa bar London. Huyohuyo Zitto alifadhiliwa ujenzi wa shule jimboni kwake akanyamaza kimya ka sio yeye.

Lissu huyuhuyu alidukuliwa kwenye simu yake akiwapigia simu maofisa wa juu wa acacia. Yaani matapeli matupu
Andiko zitto unalijibu kwa pumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom