Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi husababishwa na nini?

Tuk

New Member
Sep 10, 2021
1
1
Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi husababishwa na nini. Je, ni kweli husababishwa kutokushika mimba?

Naomba tiba yake
 
Tayari mimba ishanasa.
Mjiandae kulea.
Hakuna mabadiliko ya mzunguko was hedhi hapo bali mimba
 
Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi husababishwa na nini,je ni kweli husababishwa kutokushika mimba?

Naomba tiba yake
Yanaweza kutokana na:
1: Mabadiliko ya hali ya hewa/kusafiri
2: Msongo wa mawazo/stress
3: Maambukizi kwenye viungo vya uzazi
4: Kutokupata lishe bora
5: Kazi ngumu/mazoezi
6: Kunyonyesha
7: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango
8: Kuwa mjamzito bila kutarajia

Tiba: hutegemea na chanzo husika, fika hospitali.
 
Yanaweza kutokana na:
1: Mabadiliko ya hali ya hewa/kusafiri
2: Msongo wa mawazo/stress...

Ni Sababu zipi husababisha mabadiliko ya hedhi?​

Ni hali ya kawaida kwa hedhi kubadilika mara kwa mara kutokana na sababu kama ugonjwa, dhiki, ujauzito, kunyonyesha, kusafiri safari ndefu, kufanya kazi kupita kiasi, ama kubadili mlo. Ila mfumo wa hedhi ukibadilika ghafla, kuchelewa kwa miezi kadhaa, au kuambatana na shida nyingine, huenda ikawa ni ishara ya tatizo kubwa.

Ikiwa siku za hedhi zitabadili mfumo ghafla, kila wakati inapaswa ufikirie uwezekano wa kupatwa na ujauzito wakati wowote- licha ya kutumia njia ya upangaji uzazi.

wakati mwingine Ovari haitoi yai. Wakati jambo hili linapotokea, mwili unapunguza kiwango cha hedhi, ambacho husababisha mabadiliko ya mara ngapi au kiasi gani mwanamke hutokwa na damu. Wasichana ambao hedhi zao ndio zinaanza- au wanawake ambao hivi karibuni wamesimamisha kunyonyesha-wana uwezekano wa kutokwa na damu kwa muda wa miezi michache, au kupata kiwango kidogo cha kutokwa na damu, au kuongezeka kutokwa na damu. Hedhi zao hurudi za kawaida baada ya mud fulani.

Wanawake ambao hutumia homoni kama njia ya upangaji uzazi mara nyingine hupata hedhi katikati ya mwezi.

Wanawake wenye umri mkubwa ambao hawajafika kikomo kupata hedhi wanao uwezekano wa kupata hedhi inayoambatana na utokaji mwingi wa damu au kutoka kwa damu mara kwa mara kuliko wakati wa ujana wao. Wanapokaribia uzee, huenda wakakosa kupata hedhi kwa muda wa miezi michache ndipo wapate hedhi tena.
 
Naomba kuuliza
Kwanza kabisa nlikua na mzunguko wa hedhi wa siku 28
Kwa kumbukumbu zangu mwaka jana kila ikifika tarehe 21 nlikua napata hedhi nkabadilisha mazingira tokea january mpaka sasa naingia period kila baada ya siku 35 nahitaji kushika mimba kwa sasa .
Je ni siku zipi ntapata mimba nilijarbu siku ya 14 imegoma.
Yanaweza kutokana na:
1: Mabadiliko ya hali ya hewa/kusafiri
2: Msongo wa mawazo/stress
3: Maambukizi kwenye viungo vya uzazi
4: Kutokupata lishe bora
5: Kazi ngumu/mazoezi
6: Kunyonyesha
7: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango
8: Kuwa mjamzito bila kutarajia

Tiba: hutegemea na chanzo husika, fika hospitali.
 
Naomba kuuliza
Kwanza kabisa nlikua na mzunguko wa hedhi wa siku 28
Kwa kumbukumbu zangu mwaka jana kila ikifika tarehe 21 nlikua napata hedhi nkabadilisha mazingira tokea january mpaka sasa naingia period kila baada ya siku 35 nahitaji kushika mimba kwa sasa .
Je ni siku zipi ntapata mimba nilijarbu siku ya 14 imegoma.

Kama mzunguko wako ni siku 35, basi siku muhimu kwako ni ile ya 21 ya mzunguko. Hii huanza kuhesabiwa tangu siku ya kwanza damu inapoanza kutoka.

Ili kuwa na wigo mzuri, unaifanyia kazi siku ya 20 na 22.
Usipofanikiwa, waone wataalamu kujua kama kuna shida tofauti.
 
Back
Top Bottom