Mabadiliko ya muundo wa shirika la TPDC wageuka chochoro wa vigogo kuwaingiza watu wao

ejoka

Member
Feb 17, 2010
13
0
Mchakato wa mabadiliko ya muundo wa Shirika la T.P.D.C uliolenga kuleta ufanisi wa uendeshaji kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi, umegeuka kuwa kilio kwa wafanyakazi waliotumikia shirika hili kwa uaminifu na ustadi mkubwa na kufanikisha utafiti na ugunduzi wa gesi na kuwafanya viongozi wa Wizara mama ya Nishati kutembea kifua mbele na kujigamba kwa mafanikio haya.

La kushangaza ni kwamba Bodi ya shirika hili kwa kushirikiana na vigogo wa Wizara ya nishati na madini wakimtumia Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, wameamua kuwaondoa wafanyakazi wa shirika hilo kiujanja kwa kutangaza nafasi zao gazetini kinyume na sharia namba 8 ya utumishi wa pamoja na sharia namba 6 ya ajira ya mwaka 2004.

Mabadiliko haya yanafanywa kwa kificho na usiri mkubwa bila kuwashirikisha wafanyakazi pamoja na chama cha wafanyakazi.

Lengo la vigogo hao ni kuingiza watu wao watakao wasaidia kujinufaisha kwa matakwa yao binafsi. Tayari katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ameshinikiza bodi ya T.P.D.C kumwingiza mtu wake na kupewa nafasi ya ukurugenzi na utawala bila kufanyiwa usaili wowote wakati hapo mwanzo nafasi hio ilitangazwa na baadae tangazo likaondolowa na kuletwa mtu kimyakimya tofauti na nafasi nyingine zimeendelea kutangazwa wakati waliokuwa wanazishikilia wapo na wanaambiwa na wao waombe na masharti ya umri wa miaka 45 wafanyakazi wanaoshikilia nafasi hizo karibu wote wameishazidi tangu bodi hii izinduliwe kumekuwa na ubabaishaji mkubwa katika ajira za wafanyakazi.

Mfano palitangazwa nafasi ya Mkurugenzi wa fedha kwa watu wa ndani na wan je wote wakaomba, bodi haikuwahi kutoa majibu na sasa nafasi hio imetangazwa tena na kuwataka wale walioomba wakati ule waombe upya; hali hii ni ufujaji wa raslimali za shirika na kuwajengea hali ya wasiwasi wafanyakazi na kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Wakati taifa linakosa ajira kwa vijana wake wasomi, bodi ya T.P.D.C kwa kushinikizwa na kurubuniwa na vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini, hasa Waziri Sospeter Muhongo na Katibu wake Bwana Maswi, imetangaza nafasi za kazi za shirika hili nje ya nchi(Diaspora) kwa kutumia dharau ile ile ya kudai kuwa Watanzania hawana uwezo wa kusimamia na kuendesha mambo yao wenyewe.

Mawazo haya ni matusi na kejeli kwa wafanyakazi wa shirika kama T.P.D.C ambalo lina wasomi wengi waliobobea katika Nyanja ya utafutaji wa mafuta na gesi na kufanikisha upatikanaji wa gesi nyingi katika nchi kavu pamoja na kina kirefu cha bahari(deep sea) pia wamewezesha uanzishaji wa mradi mkubwa wa bomba la gesi wa mitandao, miwili na kuwafanya vigogo hao kutembea kifua mbele na kujitapa kwa mafanikio ambayo malipo yake yamekuwa ni njama za kuwaondoa na kuwanyanyasa waliofanya kazi hii kubwa kwa maendeleo ya taifa letu.

Katika nchi nyingine zinazothamini michango ya wataalamu wake, wafanyakazi hawa wangeshukuriwa na kupewa marupurupu kwa kazi yao njema. Kinyume chake wanakatishwa tama na kutangaza nafasi zao kana kwamba ni wahalifu, ambao hawakutoa mchango wowote katika shirika hili na taifa kwa ujumla.

La kushangaza ni kwamba mambo yote hayo yanaendelea wakati Mkurugenzi mkuu wa T.P.D.C ambaye muda wake wa utumishi umeshakwisha yupo anaendelea kutumiwa na bodi kuwanyanyasa wafanyakazi wenzake ambao amefanya nao kazi kwa muda mrefu kama ni mafanikio au kushindwa kwa maendeleo ya shirika yeye ni mhusika mkuu. Lakini bado inazidi kumpa rushwa ya kuendelea kuwepo kazini ili atimize na kufanikisha matakwa ya wakubwa.

Kutokana na muda wa Mkurugenzi kuisha nafasi yake ilitangazwa na kusababisha sintofahamu kuwa kubwa katika bodi yenyewe baada ya wajumbe kugawanyika, baadhi walishinikiza watu wao wapewe nafasi hio na wajumbe wengine wakitaka mwenzao kati yao wakati huo huo Waziri Sospeter Muhongo akitaka Mkurugenzi atoke nje ya nchi. Katibu Mkuu wa wizara yeye anataka apewe mtu kutoka katika kabila lake.

Hali hii inaelekea kulidhoofisha shirika ambalo ni tegemeo pekee la uzalishaji wa nishati yenye uhakika, Rais wan chi anaombwa kuingilia kati haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, ili kufanikisha azma hii chafu, uongozi wa wizara ukishirikiana na bodi umempa katibu mkuu kiongozi taarifa za uongo kuhusu utendaji wa wafanyakazi wa T.P.D.C ili vigogo hao waweze kupata ridhaa mianya ya kuingiza watu wao. Vilevile kamati ya Bunge ya Nishati imepatiwa taarifa za uongo kuhusu mchakato mzima wa muundo mpya wa T.P.D.C imedanganywa kuhusu ushiriki wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wa T.P.D.C Ukweli ni kwamba vyama vya wafanyakazi hawakushirikishwa hata kidogo mchakato umefanywa kwa siri kubwa kati ya bodi na vigogo wa wizara ya nishati na madini.

Muundo huu umekua ukishinikizwa na makampuni ya nje pamoja na wale wanaojiita wabia wa maendeleo. Nia yao sio kujenga bali wanatafuta mianya ya kujinufaisha wao baada ya kuondoa mfumo unaoipa nafasi T.P.D.C kuwa msimamizi na mtekelezaji kwa manufaa ya taifa.

Ikumbukwe wakati wa kuanzisha biashara huria ya mafuta, wafanyakazi walitoa mawazo ya kuibakiza T.P.D.C kufanya biashara ya kuagiza na kusambaza mafuta lakini wafanya biashara wakubwa wa mafuta walisimama kidete na kuhakikisha T.P.D.C inanyanganywa uwezo huo na kusimamisha mitambo ya kuchuja mafuta(TIPER) matokeo yake Taifa limeingia katika matatizo ya kupanda kwa mafuta na bidhaa zitokanazo na mafuta ghafi. Hali hii ndio inajitokeza sasa wakati wa biashara ya gesi; viongozi wetu wanatiwa upofu na ahadi hewa na wanatumia nafasi walizo nazo katika mchakato huu usiokuwa na tija kupenyeza watu wao wasio kuwa na sifa wala wazoefu. Hii ni laana ya gesi.

Tusikubali kuingizwa katika migogoro inayotengenezwa na viongozi wenye tamaa, upendeleo kiburi na dharau kwa wale waliokaa chini yao.

Mwenyekiti wa bodi ambae alitegemewa kulisaidia shirika, ameonekana kukosa mwelekeo amebaki kulambishwa utamu wa safari za kwenda nje ya nchi kila kukicha. Tangu mwaka huu uanze alishakwenda safari zaidi ya sita nje ya nchi, kana kwamba yeye ni mtaalamu au Mkurugenzi mtendaji wa shirika. Kweli tutafika, tunamshauri mheshimiwa Rais, aimulike bodi ya T.P.D.C kabla mambo hayajawa mabaya zaidi ama sivyo shirika limo katika hatari ya kutekwa na mafisadi/wahujumu wa kimataifa wakishirikiana na vigogo waliopewa dhamana ya kusimamia raslimali nchi.
 
S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Wakati taifa linakosa ajira kwa vijana wake wasomi, bodi ya T.P.D.C kwa kushinikizwa na kurubuniwa na vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini, hasa Waziri Sospeter Muhongo na Katibu wake Bwana Maswi, imetangaza nafasi za kazi za shirika hili nje ya nchi(Diaspora) kwa kutumia dharau ile ile ya kudai kuwa Watanzania hawana uwezo wa kusimamia na kuendesha mambo yao wenyewe.

Kwa akili ya muandishi wa makala hii na mhariri wake hapo wanamaanisha Tanzania Diaspora SIO WATANZANIA..!!!
 
TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,601
2,000
Kama kweli hayo mabadiliko yanafanyika kwa nia njema, basi itakuwa ni vizuri. TPDC ina wataalamu wa madigrii tu, hawana field exposure kabisa. Ningeweza onana na Muhongo, ningemshauri nafasi za DG na Director of Upstream Operations zijazwe na world class Oil&gas industry professionals wenye uzoefu usio pungua 15yrs kuendesha shirika la mafuta na gesi kwenye mazingira ya ushindani. Hizo nafasi mbili ndio center point ya TPDC bussiness. Serikali kwa nia njema kabisa itoke nje itafute wataalamu hao iwalipa vizuri, waweze kustructure shirika na develope capacity kwa local manpower.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,024
2,000
Wakati taifa linakosa ajira kwa vijana wake wasomi, bodi ya T.P.D.C kwa kushinikizwa na kurubuniwa na vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini, hasa Waziri Sospeter Muhongo na Katibu wake Bwana Maswi, imetangaza nafasi za kazi za shirika hili nje ya nchi(Diaspora) kwa kutumia dharau ile ile ya kudai kuwa Watanzania hawana uwezo wa kusimamia na kuendesha mambo yao wenyewe.

Mwenyekiti wa bodi ambae alitegemewa kulisaidia shirika, ameonekana kukosa mwelekeo amebaki kulambishwa utamu wa safari za kwenda nje ya nchi kila kukicha. Tangu mwaka huu uanze alishakwenda safari zaidi ya sita nje ya nchi, ................

Sifahamu undani wa ofisi yenu hii ya TPDC lakini naelewa ni shirika ambalo limekuwa na mkurugenzi mkuu useless kabisa! Mbaya zaidi amekaa nafasi hiyo kwa miaka isiyoelezeka. naona amestaafu na miaka 80. Tangu miaka ya 80 yeye amekuwa mkurugenzi mkuu. Kama huyo ndo alikuwa mtendaji mkuu, na wengine wako chini yake, basi nahofia uwezo wao unaweza kuwa chini zaidi.

Kuhusu bodi, hilo ni tatizo la nchi nzima. Ni tatizo la serikali yetu. ni dhaifu! Kuna watu wanateuliwa bila kutegemea mafanikio yoyote toka kwao. Hiyo TPDC ni mafuta na gesi. HIzo ni sekata zenye matatizo ya watalaamu wa ki Tanzania. Kama wataálamu hakuna ni vigumu kabisa kupata watu wanaoweza kuingia kwenye bodi na wakatoa mchango wa kueleweka. Hivyo nasema bila hata kujua wajumbe wa bodi yenu, hao ni buree tu!

Kuteua mkurugenzi kutoka nje ya TPDC siyo kosa lakini tuombe isifanyike tu kwa sababu ya dhalau. Naikumbuka Muhimbili yenye mkurugenzi toka UK. Alipigiwa kelele bila sababu zozote na kumbe wa-TZ waliitaka nafasi hiyo. Alipoondoka ndo ulikuwa mwisho wa mabadiliko. Walioingia ikawa ni ukabila. Uchaga, uchaga, uchaga na baadaye ameingia mama huyu akaaanza pia kupigwa vita!

Tuna Matatizo na ajabu unaomba msaada kutoka kwa Rais aingilie kati. Rais unamjuwa? ni wateule wangapi wa Rais unaweza kuwtaja kama mfano mwema? Tumekwisha na kama tumeanza hovyo hovyo kiasi hicho, subiri ile inayoitwa the curse of oil inakuja.
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,144
1,500

Hivi wewe ukiambiwa uthibitishe miaka themanini ya mkurugenzi mkuu utaweza thibitisha?
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,865
1,500
Muhongo ni Janga kwa Rasilimali za nchi yetu! Soon utasikia kuna Agency inafanyakazi kwa niaba ya TPDC kama alivyofanya Tibaijuka ... CCM hakuna mwenye afadhali ...
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,024
2,000
Hivi wewe ukiambiwa uthibitishe miaka themanini ya mkurugenzi mkuu utaweza thibitisha?

Uzembe kama kawaida. Unaiga unayoyasikia bungeni na serikalini. Watu wanaambiwa nchi inaibiwa wanasema lete ushahidi. Ni hao hao wakiambiwa hawala yako anachukuliwa na Patriot wanainama kuomba siri zaidi.
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,144
1,500
Uzembe kama kawaida. Unaiga unayoyasikia bungeni na serikalini. Watu wanaambiwa nchi inaibiwa wanasema lete ushahidi. Ni hao hao wakiambiwa hawala yako anachukuliwa na Patriot wanainama kuomba siri zaidi.
Duniani kote hoja inathibitishwa na ushahidi,wewe.unaanza kuleta ngonjera za akina wanaukawa hapa sheme on you
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,024
2,000
Duniani kote hoja inathibitishwa na ushahidi,wewe.unaanza kuleta ngonjera za akina wanaukawa hapa sheme on you

Duniani kote wapi? What is Dunia. Achana na JF rudi Shuleni. Sijui ngonjera na wala sijawahi kuandika ngonjera wala maigizo. Ninayo mengi ya kukufundisha kuliko simulizi zako. Why are you curious to know the useless? You better apply the useless and intensify to know the useful. You seem to be weak, useless and a less well-meaning learner. Why is the happiness of your boss stealing your joy?

Rudi kwenye TPDC kuliko kuhangaika na tunaokuzidi ufahamu.
 
Ufahamu wa kukadiria watu umri ndio ufahamu gani huo ,wenye ufahamu hawajitangazi bali wanaonekana kwa walioyafanya mkuu,
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
Kweli uozo upo sana na wanasiasa wanashiriki kwa kiasi kikubwa kuligharim taifa hili.

Especially bodi ya shirika imekuwa haina msaada.

Hilo suala la mwenyekiti wa bodi kuwa mtalii nje ya nchi kana kwamba yeye ni miongoni mwa wataalamu wa shirika nalo limekuwa kero iliyopitiliza.

Bodi na wizara ya nishati wamehodhi kila kitu ktk shirika.

Wanalipeleka pabaya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom