Mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala shule za Msingi inawachanganya wanafunzi

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236

stationery-640x350.jpg

BAADHI ya Walimu wa Shule za Msingi katika jiji la Dar es Salaam wamelalamikia mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala kwa shule za msingi pamoja na idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa madarasa yote na kwamba yamekuwa yakiwachanganya wanafunzi na kuwafanya washindwe kumudu masomo yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na FikraPevu jijini humo Novemba 17, 2014 walimu hao wamesema mabadiliko ya mara kwa mara kwa mitaala yanayofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bila maandalizi yamekuwa chanzo na kikwazo kikubwa cha kutofanya vizuri kwa sekta nchini.

Walimu Wakuu katika shule hizo wamesema mabadiliko ya mitaala ya mara kwa mara inawachanganya wanafunzi pamoja na walimu kutokana na walimu kutoandaliwa vyema na kushirikishwa katika uanzishwaji wa mitaala hiyo na hivyo kuwa kikwazo kufikisha ujumbe kwa hadhira.

Kwa mujibu wa walimu hao ambao baadhi yao (hawakutaka majina yao yatajwe) wameshauri kuwepo na maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha walimu ambao ndio wanakabiliana na hali ya kufikisha elimu hitajika kwa wanafunzi. Wanataka washirikishwe kwani sekta ya elimu ni muhimu na kwamba kabla ya mabadiliko ya mitaala hiyo haijaanza kutumika itasaidia kuwepo kwa usawa katika masomo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mashujaa ya Sinza ‘B', Triphonia Kahwili, amesema pamoja na hali hiyo mabadiliko ya vitabu vya masomo bila utaratibu mahususi ni tatizo pia katika mafanikio ya sekta hiyo kitaaluma.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela, ameema utofauti uliopo kwa mtaala unaotumika hivi sasa na ilivyokuwa hapo awali, amesema mitaala ya sasa imevurugwa kiasi kikubwa jambo ambalo linawachanganya walimu na hata wanafunzi hivyo kushindwa kufanya vizuri.

"…Hii mitaala haieleweki kwamaana tangu mwaka 2005 ilipoanza kutumika unakuta mwalimu mmoja katika mkoa au wilaya ndiye aliyepewa mafunzo ya mabadiliko ya hii mitaala kwahiyo ni vigumu kumfundisha mwanafunzi masomo kama ya Tehama nawakati mwalimu mwenyewe hata komputa haijui" alieleza Mkuu wa shule moja wapo ya shule zilizopo jijini humo.

Hata hivyo, wamelalamikia baadhi ya masomo kuwa


Habari zaidi, Soma=>Mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala shule za Msingi inawachanganya wanafunzi
 
Back
Top Bottom