Mabadiliko Ya Majina Ya Makampuni Yana Tija Gani

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Ni utaratibu uliojengeka hapa nchini Tanzania na kwa nchi nyingi za Kiafrika kubadili majina ya Makampuni yao. Ninashindwa kuelewa ni kwa nini wanafanya hivyo. Ipo mifano mingi ya makampuni yaliyobadili majina yao kwa mfano:
- Mobitel kuwa Buzz na sasa Tigo
- Cetel kuwa Zain
- Sheraton kuwa Movien Peak
- Kilimanjaro Hotel kuwa Kempinsky
na mengineyo. Kuna nini? Au ni kamtindo ka kukwepa kodi kwa kupewa Grace Period ya miaka kadhaa.
 
Kuna nini? Au ni kamtindo ka kukwepa kodi kwa kupewa Grace Period ya miaka kadhaa.

Mimi naungana nawe mkuu katika fikra za kuwa kuna kamtindo fulani ka kukwepa kulipa kodi hapa. Kwani tukiangalia hiyo kampuni ya Celtel imeanzishwa lini?....Pengine ile miaka kadhaa iliyokuwepo kwenye mkataba awali ndo inakaribia kwisha, hivyo inabidi kubadilisha jina fastafasta ikiambatana na kubadilishwa mmiliki ili tuanze tena ajwa katika kuhesabu miaka ya kusamehewa kodi. Mwenye kubisha na atuambie kuna sababu gani za kiufundi zinazopelekea makampuni haya kubadilishwabadilishwa majina kiasi hiki?
 
lazima hii itakua ni mojawapo ya kukwepa kodi mana kampuni mmoja haiwezi badili jina mara mbili kwa kipindi kifupi sasa we watu ndio kwanza tuna anza zoea celtel mara zain!!! sijui lakini hii ni janja moja wapo tu katika biashara
 
Hakuna suala la kukwepa kodi katika hili kumbuka Celtel International imenunuliwa na Zain kwahiyo wameamua kutumia brand name yao kwenye operations zao zote afrika nzima.sasa wanakwepa kodi Uganda,Malawi,Congo na kila mahali walipokuwa na operations? Na ikumbukwe its very costly kubadilisha jina kwasababu inakubidi ufanya matangazo mengi kulifanya jina lijulikane kwa wateja wenu,kuweka billboards mpya,signboards,vipeperushi vipya na kadhalika nchi nzima.kufanya branding mpya kwenye magari na kila kona na mabango yote ya zamani kuyaondoa na kuweka mapya zoezi hili pengine lina gharama kubwa kuliko kodi wanayoikwepa kama kodi ndiyo lingekuwa tatizo. Mambo yaliyokuwa yanafanyika kwa sheraton-royal palm-movenpick ni tofauti na haya ya makampuni ya simu.Mobitel ilinunuliwa na kubadilishwa jina kwa hilo sasa n.k. Kwahiyo siyo kila mabadiliko ya majina yana lengo la kukwepa kodi lazima tufahamu chanzo cha mabadiliko hayo!
 
Tumekubali biashara huria kabla ya kujiandaa na kuelewa biashara watu wanafanyaje sasa wafanyabiashara wameingia tunashangaa wanavyofanya biashara badala ya kuchukua hatua zaidi na kufanya biashara kubwa.

Zipo sababu nyingi za kubadili majina ya biashara na hiyo ya kukwepa kodi inaweza kuwa mojawapo lakini si pekee. Kwa mfano unapobadilisha umiliki wa kampuni au brand,bidhaa au huduma basi mmiliki mpya anayo hiari ya kubadili ya jina au kuendelea na jina la zamani kutokana na biashara kwa wakati huo.

Chukulia mfano wa sigara embassy,sports,nyota na SM zimebamba kishenzi kiasi kwamba mmiliki mpya ameshindwa kubadilisha jina. Hata safari na Konyagi pia majaribio ya kubadilisha majina yalikuwepo lakini bidhaa zinauza kwa majina na wabongo wana ya feel kinoma.

Kuna Bank iliyokuwa ya wakulima CRDB imebadilishwa kuwa CRDB bank Ltd n.k Lakini uzoefu unaonyesha makampuni yaliyobadilika na umiliki wake unahusisha sehemu ya Watanzania yameendelea kuwa na majina yaliyozoeleka. Lakini makampuni yaliyonunuliwa au kuanzishwa na watu wa nje persie jamaa wamebadilisha au kuleta majina mapya kuendana na soko lao la kimataifa. Kama Kempiski kuongezwa katika Kilimanjaro Hotel.

Mo-Ibrahim alishaibana Celtel kitambo sasa aliyenunua kama anabadilisha jina sidhani kama ni kukwepa kodi manake wamefanya kwa Celtel zote Africa na sheria za kodi zinatofautiana.

Wabongo tumeingia katika mfumo wa kibepari, tujifunze zaidi huo mfumo unafanyaje kazi ili nasi tupambane nao kuliko kuendelea kushangaa na kuwa waoga.
 
Kinyamana, I envy you for your response!
Tunapoanzisha mjadala ni vizuri kufanya reseach kidoogo kabla ya kuandika.
Kilichobadilika kwa makampuni kama Celtel to Zain au Mobitel to Tigo ni brand name na siyo kampuni. Makampuni hayo ni yale yale Zain ni Celtel Tanzania Ltd na Tigo ni MIC Tanzania Limited. Brand name ni jina la biashara. Kama ambavyo designers wanavyokuwa na labels! Hakuna ukwepaji wa kodi wala nini!! na kiasi sasa hivi si rahisi kukwepa kodi kwa kubadilisha jina tu! Labda utoe mfano mwingine
 
Ni utaratibu wa makampuni makubwa kununuana. Ili mradi anayenunuliwa akubaliane na bei ya anayenunua. Hakuna suala la kukwepa kodi. Kodi ni dhana iliyojengeka miongoni mwetu wa-Tz, lakini muendelezo wa raslimali unabaki palepale. Kinachobalidilika ni jina, uongozi na umiliki. Je, hamna habari kuwa Microsoft anataka kumnunua Google lakini Googe kakataa? aliona search engine yake (Microsoft) haifui dafu kwa Google. Wengine wananunuana ili wabaki wao tu, mfano ni Tanzania Brewaries na Kibo Brewaries. kwenye maltinational business nai kawaida kununuana ili mwenye nguvu abaki peke yake. Tusishangae iko siku haya makampuni ya simu tunayoyaona leo yatanunuana na kubaki moja.
Tatizo letu wa-Tz kila kitu tunafanya kibinafsi. Hatuna coperate management. Kila mwenye kampuni anataka libaki kuwa lake yeye na sanasana familia yake. Hatupendi kuunganisha mitaji.
 
Asalaaam walleikhum,
Jamani kwani sheraton iliponunuliwa na movenip., si moven p. alikuja kama muwekezaji mpya na kukwa kwake muwekezaji mpya anaenjoy some tax relief? kwanini isiingie akilini kuwa makampuni ya nje yanaamua kuuziana ili kukwepa kodi? tukiachana na Zain maana ni makampuni mengi yametajwa
 
Back
Top Bottom