Mabadiliko ya kweli tanzania yataletwa na watanzania wenyewe siyo vyama vya siasa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko ya kweli tanzania yataletwa na watanzania wenyewe siyo vyama vya siasa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtalae72, May 28, 2012.

 1. mtalae72

  mtalae72 Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania kwa muda mrefu na watanzania wengi wamekuwa na matumaini ya kupata chama mbadala yaani CHADEMA lakini nina mashaka makubwa kama CHADEMA kama chama wataweza kuleta mabadilikko ya kweli ndani ya Tanzania hasa kama watanzania wenyewe hawatabadilika na kuachana na tabia walizozikumbatia kwa sasa. Kwa mfano, tatizo la rushwa Tanzania siyo la CCM peke yake.. ni tatizo la nchi na mfumo mzima. Kwa wale waliosoma enzi za Mwl. Nyerere wakati wanalipwa hela za nauli kwenda shule watakumbuka jinsi wengi wao walivyokuwa wanadanganya kwamba wanatoka mikoa ya mbali ili walipwe hela nyingi ili hali walikuwa hawatumii hata nusu ya hizo hela walizokuwa wakizidai kusafiria kwenda makwao.

  Tatizo la akina David Jairo, akina Mataka na hata mawaziri wachache waliowajibishwa hivi majuzi halitokani na tabia zao tu kama 'individuals' lakini pia ni tabia za watanzania za kupenda maisha ya gharama na pia kupenda kukata kona na kudanganya ili kujinifaisha wao wenyewe na matumbo yao. Huyo mkurugenzi wa TBS ni mfano mwingine wa karibu. Kwa kifupi ni kwamba uozo, dhuluma na rushwa Tanzania imetapakaa katika kila ngazi. Ndiyo maana Mzee Lowassa alivyowajibishwa kuacha uwaziri mkuu aliweza kupata msafara wa magari zaidi ya 100 kumpokea kula Monduli kama shujaa japo wengi wanajua kwamba hakuwa na uaminifu wa kutosha katika ofisi yake. 'Waheshimiwa' Maige na Ngeleja nao wamepokelewa kama wafalme huko kwenye majimbo yao. Katika mazingira ya namana hiyo huwezi kuamini kwamba CHADEMA kama chama wataweza kuleta mabadiliko ya kweli hata kama nia ya dhati ipo. Sana sana tutaishia kujaza magereza na labda kujenga mengine mapya mengi ili kufunga watu wengi zaidi. Kwa kifupi tunataka mabadiliko ya watanzania wenyewe. Kuna watu hata wanadiriki kusema kwamba CHADEMA hawawezi kutawala Tanzania kwa sababu watafuata fuata watu sana.. kufuata fuata watu katika mantiki ya kujaribu kuondoa rushwa serikalini!!! Hivi karibuini shirika la misaada la marekani USAID walitoa barua ya onyo kali kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo hapo Tanzania. Katika barua hiyo walianisha jinsi ambavyo wafanyakazi watanzania wa shirika hilo wanavyodanganya mfumo wao wa malipo kwa safari za uwongo, risiti za kurudufu, vocha za simu za uowongo ili kujipatia fedha zaidi hata pale ambapo hawastahili! Hili siyo jambo dongo na wala siyo jambo la kujivunia. Inaonyesha jinsi society yetu ilivyooza na vitendo ambavyo tunaviona ni vya sifa wakati kwa wenzetu na mambo ya aibu! Niliwahi kumsikia jamaa mmoja akisema kwa kujisifia kabisa kwamba Mzee Makweta na akina Kunambi waliokuwa viongozi tangu enzi za mwalimu walikuwa wajinga kwa sababu maisha yao ya uzeeni yamekuwa ya kifukara na hawana hata nyumba za kuishi. Yaani kwa uaminifu wao na kujitolea kwao kulitumikia taifa, sasa wanaonekana nongwa na wajinga eti kwa sababu hawakujilimbikizia kama tunavyoona mawaziri wa sasa wanavyofanya..... Haya siyo mambo ya kujivunia bali ni mambo ya aibu. Ndiyo maana bado naona vigumu sana kwa chama mbadala kuleta mabadiliko ya kweli bila watanzania wote kwa ujumla wao kuamua kuamka na kutaka kubadilika. Najua hata humu mtandaoni kuna watu wanalalamika na kutaka mabadiliko lakini wengi wetu pia tunakuwa na chuki na tamaa kwamba nasi tungekuwa kwenye nafasi za kukwapua mali za umma basi tungefanya hivyo hivyo na pengine hata zaidi. Nafikiri ni wakati muafaka kwetu wote kujifikiria na kujiuliza ni mabadiliko yapi hasa tunayataka ambayo yataleta tija kwa taifa letu na siyo kwenye mifuko yetu!!
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  ni kweli yataletwa na watanzania wenyewe lakini kaa ukikumbuka kuwa hawa watanzania wasipohamasishwa na kuachwa kama walivyo haya maneno uliyoyasema hayawezitokea kamwe, je ni nani anayepaswa kumhamasi huyu mtanzania aweze kujiletea hayo maendeleo? Nadhani hapo ndipo unapata jibu kutoka kwa kile unachokidhalau kuwa hakiwezi kuwaletea maendeleo watanzania
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ndio maana ninapinga RUZUKU kwa vyama vya siasa, CHADEMA wanakula zaidi ya 200 milioni, CCM zaidi ya 800 milioni na CUF zaidi ya 117 milioni kwa mwezi. . . hii si sahihi!
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,582
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu yangu!
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kaa Pembeni kama una mashaka Tuache Tusio na Mashaka Tuendelee na CHADEMA yetu! ukombozi ukiletwa tutakuita kwani wewe na Mtanzania mwoga
   
 6. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Siasa zilizopo ni za kupandikiziana utumwa wa fikra, kufanya watu wasifikiri na kuacha dhamana ya maendeleo kwa wanasiasa tu! Kuamini wanasiasa ni sawa na kupigwa sindano ya nusu kaputi, katika kuleta maendeleo!
  Sisi wenyewe ndio wa kuhamasishana katika kutambua tunataka nini na kwa wakati gani na kwanini, pia kwa namna gani. Wanasiasa waliopo ni wanafiki!
  Embu tujiulize ndugu zangu, tangu kuanza kwa mfumo huu wa demokrasia Afrika, ni nchi gani imejikomboa na haimo tena katika majanga ya njaa, vita, magonjwa, ufisadi, rushwa, umasikini, matabaka, nk? Why don't we declare the failure of democracy in Africa? Kisha tukae chini tuumize vichwa ni mfumo upi wa siasa unaweza kutufaa, au tuamini huu ndio mwisho wa ubunifu? Au hadi mzungu aseme?
  "Domokrasia"
  Maisha ni furaha, kama haipo basi ni upuuzi mkubwa! Wazungu wamefanya maisha yawe marefu sana, lakini ni mabaya kuliko!
  Mungu wetu anaita!
   
 7. B

  BARRY JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Tatizo la watanzania wengi ni wezi, wavivu na siyo watu wa kuumiza vichwa. Unakuta graduate anafanya kazi kwa private company huku anawaza kuiba au aende serikalini akaibe, nani aliyeleta haya mawazo ya kuiba? Watu wanaiba muda wa mwajiri, wanaiba risiti, wanadanganya wanaumwa kumbe wanataka kudate! Huu wote ni wizi....
   
Loading...