Mabadiliko ya kushika dola zima ili kusafisha uozo Tanzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko ya kushika dola zima ili kusafisha uozo Tanzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 9, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mataifa mengi duniani yameendelea kutokana na siasa za kiushindani. Panapokosekana ushindani basi mengi hudumaa na aliyekabidhiwa majukumu huwa hana msukumo wa kujituma kwa vile hakuna khofu ya kuenguliwa inayojengeka na siasa za ushindani huwa haipo, na kwa vile huwajibika moja kwa moja kwa mkubwa aliyejuu yake, basi jitihada ni kujiweka sawa kwa mkuu wake. Na hata aliye na wajibu wa jukumu la kulinda haki za vyama vyote utaona anakuwa golikipa wa goli la waliomadarakani badala ya kazi yake ya urefarii.

  Kwa utaratibu huu utakuta uozo ndani ya mashirika ya umma, taasisi za umma na serikali, na idara mbalimbali za serikali hujengeka uozo kwa vile aliyekatika nafasi anajua kama ni haki yake. Hali hiyo hujenga mpoozo wa kujituma na wajibu wake kwa umma anaoutumikia.

  Tunachoshuhudia na kuwaona wakati wa kampeni za kuomba kura, na waombapo kura wako tayari kwa staili ya kila aina hata kukaa chini mavumbini na viwete ili kuuza sura zao kwa wapiga kura. Ahadi nyingi ambazo kwa mwenye mtazamo wa utashi wa kweli zinaonyesha kila dalili ya uwezekano hafifu wa kuzitimiza, lakini wanaendelea kuwahadaa wananchi hasa wa vijijini ambao wengi wao utambuzi wa masula ya kisiasa ni bado na elimu ya uraia huwa haijawafikia kwa kiwango cha uelewa kama wa watu wa mijini ambao ni waathirika wa huduma za msingi kama maji, umeme, usafiri nk.

  Viongozi wengi katika nchi zetu za kiafrika wanaakisi mtindo wa kitemi kwa kujifanya wako juu ya wale wanaowatumikia na hivyo waliowachagua waendelee kuwaimbia nyimbi za kuwasifu kama ilivyozoeleka kumwabudu mfalme. Wakienda kutembelea mashambani kwenye madimba ya mpunga wanahitaji kujengewa mahema yaliyoezekwa na watandikiwe mikeka na mashuka huku wamevaa tai shingoni badala ya kuvaa t-shirt na mabuti ya shambani na kushika jembe kuonyesha mfano zoezi ambalo litadumu kwa dakika 20 tu. Wanashindwa kusoma mazingira wanakokwenda kama kuiga mfano wa Rais wa zamani wa Marekani George Bush alipowatembelea Wamasai huko arusha alivaa suruali ya jeans ili wamasai wasimwone mtu wa pekee na ilikuwa rahisi kwake pia kujichanganya na kucheza ngoma ya kimasai. Sisi tuliokulia umasaini tunakwenda kwa wamasai na tai zikining'inia shingoni.

  Kuzeeka kwa mfumo huu uliozoeleka ambao waliobahatika kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali na mashirika mbalimbali kwa kukosa msukumo wa siasa za ushindani kwa miaka 50 iliyopita, mfumo huo umeendekeza rushwa iliyokithiri, hali ambayo imeleta aibu kubwa isiyo kawaida mwaka jana katika kura za maoni na kampeni za urais, ubunge nk. kutoka Chama Cha CCM. Hakuna malalamiko kutoka vyama vya upinzani kuhusu rushwa. Na laiti CCM pesa nyingi walizoelekeza kwenye rushwa kama kununua magari ya kampeni, kununu caps, kanga, kukodi malori ya kusomba watu wahudhuria mikutano yao, ingetosha kununua mtambo wa umeme na hivyo kupunguza tatizo la mgao wa umeme unaoendelea sasa.

  Na kibaya zaidi unapoona hakuna umoja na mshikamamo katika serikali ujue hapo jipu ndio limevunda. Ni rahisi kuzuia jipu unaposikia maumivu ya awali, lakini likishavunda hakuna jinsi ni kuacha lipasuke tu na kutazamia kuuguza donda. Kila mmoja anatoa kauli inayopingana na mwingine wakati wana vikao vya pamoja. Mwingine anapojaribu kufuata sheria mwingine anampinga hadharani bila kuitana kwenye vikao wakashaurina njia bora ya kufanya. Kila mmoja ni msemaji na hakuna utaratibu maalum wa kutoa kauli yenye msimamo mmoja. Na wataalam wa masuala ya elimu ya tabia na mahusiano ya kijamii huanisha kwamba ukiona watoto katika famili kila mmoja anafanya kivyake tu bila utaratibu wenye unganiko la kifamili maana yake mzazi au wazazi wana kasoro katika malezi kwenye familia yao. Kwa falsafa hiyo tunaweza kutafsiri kwamba mfumo umeoza kuanzia ngazi ya juu na tunayoona chini ni dalili za wazi za wozo uliofichika.

  Dawa ya kutibu uozo uliopo sasa hivi serikalini na mashirika ya umma ni ushindani wa siasa za kidemokrasia. Hakuna atakayeweza safisha wozo huo isipokuwa chama kingine cha siasa kushika hatamu za uongo, na hivyo safu yote ya utawala uliopo itatoka na kuingisa safu mpya. Ni uozo wa miaka nenda rudi na majina ni yale yale tangu tunasoma shule za msingi hadi leo. Unaona wengine wanaondoka nje kisha wanatafuita njia wanarudi tena, sasa nini kinaendelea?
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwasemaje wanajamii forums?
   
Loading...