Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 987
Kuna mtu anaweza kuja na nadharia zake dhaifu kupinga lakini huu ndio ukweli. Hakuna mtawala aliyewahi kukubali kukaa chini na kupendekeza mabaliko ya katiba bila msukumo kutoka kwa wananchi kupitia matukio magumu yatakayomlazimu kukaa kupatanishwa na mahasimu wake.
Alipata kuyasoma haya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Prof Kitila Mkumbo akiwa mwenyekiti wa UDASA enzi hizo. Naomba ujumbe huu uwafikie wanaharakati,wanasiasa, wafia nchi yao na wananchi wazalendo. Ni ukweli ulio wazi kua katiba iliyopo ni mbovu na haikidhi kabisa mahitaji ya dunia na mazingira ya sasa.
Tusidai katiba mpya tukifikiria kua serikali itatoa kama zawadi, alitaka kujaribu Zawadi hiyo JK lakini yakamshinda kwa kupelekeshwa na chama chake. Hakuangalia maslahi ya taifa bali ni maslahi ya chama chake, alitanguliza ubinafsi ambao ndio matokeo yake vilio hivi sasa.
Tukubali kama kweli tunawaza Tanzania mpya ijayo kwa faida ya vizazi vyetu, basi tusiogope maumivu yatakayotokana na madai haya.
Msikilize Prof Kitila Mkumbo hapa;👇👇