Mabadiliko ya bei ya saruji: Tupe bei mpya ya saruji kwenye wilaya yako

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,478
2,301
Jana katika habari ya saa 2 usiku ITV nimeona mmoja kati ya wafanyabiashara wa cement alikalalamika kupanda kwa cement toka 11,000 hadi 15,000. Hii ikiwa inatokana na kiwanda cha dangote kusimama kupisha ukarabati wa kiwanda.

Ni wakati muafaka sasa kuona impact ya uwepo au kutokuwepo kwa dangote kwenye bei za cement. Ili kujua haya naomba kila mwanajukwaa atupe mpya ya cement kutoka eneo alipo
 
Watanzania tunakuwa masikini kwa fikra zetu za kuwaza kushusha vitu bei chini ili tumudu gharama zake kwa umasikini wetu.

hatuwezi kupiga hatua kwa staili hiyo.

tulizoea wakulima wakilima viongozi wanatumia madaraka kuharibu soko, utasikia wanapiga marufuku kuuza mfano watu wa mipakani kuuza nje ya nchi, utasikia wanapiga marufuku utengenezaji wa pombe, yaani wanachotafuta ni mazao ya kilimo yawe mengi bei zishuke, hivi mkulima anayezalisha anatumia nguvu, pembejeo na kila kitu lakini mafanikio tuliyoyatizama ni bei za vyakula zishuke.

tuna bogus economics na tumerithi mentality za bogus uchumi.

madini tumepoteza kwa ujinga huohuo watu wanaangalia kutoa ajira na huduma za jamii.

huu ni upuuzi mtupu na hatuwezi kufanya ujinga kwenye gesi, makaa ya mawe eti tunachotarget ni kupunguza bei ya cement.

tutumie rasilimali zetu kujenga uchumi kwa kuwawezesha watanzania wazalishe wamudu bei za vitu na sio kutumia rasilimali zetu kama ruzuku ya kushusha bei vitu.
 
Mliwachagua wenyewe acheni sasa kulakamikaaa mlijuwa maisha yatakuwa mteremko tu???miaka 10 mtaisoma number sio kidogo....mpaka baba magufuli aondoke aijui sijui nchi itakuwaje.....
 
Watanzania tunakuwa masikini kwa fikra zetu za kuwaza kushusha vitu bei chini ili tumudu gharama zake kwa umasikini wetu.
We jaa vp.. Tunataka bei ambayo hata mtanzania wa kawaida ataimudu.
kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hai reflect yanayotendeka, kod juu na zimekua nyingii had wawekezaji washindwa kumudu wengine wanaamua kuwekeza Kenya yan shida tupuuu...
 
Cx2uzfyWEAAeFzw.jpg:large
 
Dar kuna Viwanda 3 ninavyovifahamu, Twiga, Kisarawe na Camel.
Mtwara kuna viwanda viwili pia, yaani Mtwara Cement(kiko eneo la Mikindani, kinamilikiwa na Wachina) pamoja na Dangote. Vyote viko Barabara ya kuja Dar es Salaam. Lakini jana Mtwara Cement iliuzwa kwa Tdh 15000 kwa mujibu wa mahojiano ya ITV na wananchi wa Mtwara
 
Duh, balaa.
 
sitaki kutaja jina ila huku nilipo imefika mfuko 22500 kwa mfuko hali ni mbaya
 
We jaa vp.. Tunataka bei ambayo hata mtanzania wa kawaida ataimudu.
kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hai reflect yanayotendeka, kod juu na zimekua nyingii had wawekezaji washindwa kumudu wengine wanaamua kuwekeza Kenya yan shida tupuuu...

Tatizo ni sisi wananchi kutumia "ignorance" ku judge mambo. waachie wachumi wenye ujuzi lakini wakae watafakari watumie vipi rasilimali zetu kuondoa umasikini na sio nyinyi kukumbatia umasikini kwa kigezo cha kushusha bidhaa bei.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom