Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yamepoteza maana wa Muungano’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yamepoteza maana wa Muungano’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 18, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 18 June 2012 13:34 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg


  [​IMG]Patience Sekinabo akitoa mada.

  Elias Msuya
  KABLA ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, nchi hizo mbili zilipiganuia uhuru kutoka kwa wakoloni waliokuwepo. Wakati Tanganyika ilitaliwa na Waingereza, Zanzibar ilitawaliwa na Waarabu chini ya Sultan wa Oman ambaye hata hivyo alipewa koloni hilo alitunze kwa niaba ya Waingereza. Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9,1961 huku Zanzibar ikichelewa kupata uhuru hadi Desemba, 1963 baada ya chama cha ZNP kilichoungana na ZPPP kuishinda ASP na kuunda Serikali ambayo ilimtambua Sultan kama mtawala.
  Hali hiyo haikuwafurahisha wanachama wa ASP hivyo waliamua kufanya mapinduzi ya kumpindua Sultan na Serikali iliyokuwa madarakani mnamo Januari 12, 1964.
  Baada ya mapinduzi hayo, April 26, 1964, Zanzibar na Tanganyika ziliungana kwa ridhaa ya Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Zanzibar Abeid Karume.
  Katika hati ya Muungano mambo kadhaa yalikubaliwa ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika mambo ya nje, Jeshi, polisi, mamlaka ya dharura, uraia, uhamiaji, biashara ya nje, utumishi wa umma, kodi ya mapato na forodha, bandari, usafiri wa anga, posta na simu.
  Hata hivyo mambo hayo sasa yameongezeka na kufikia 22. Yaliyoongezeka ni pamoja na mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali (pamoja na noti), benki na shughuli zake na usimamizi wa fedha za kigeni.
  Mengine ni pamoja na leseni ya vuiwanda na takwimu, elimu ya juu, maliasili na mafuta, Baraza la Mitihani la Taifa na kazi zake, Utafiti, Utabiri wa Hali ya Hewa, Takwimu, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Uandikishwaji wa Vyama vya Siasa.
  Muungano huo umeundwa na Serikali mbili tendaji ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Muungano huo pia una vyombo viwili vya utaoji wa utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kuna vyombo viwili pia vya utungaji sheria ambavyo Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi.
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano inatekeleza masuala la muungano na yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika, wakati mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar yanashughulikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshapitia katika vipindi vitano tangu mwaka 1961. Katiba ya kwanza ni ya uhuru mwaka 1961 ikafuatiwa na ya mwaka 1962 iliyounda Jamhuri ya Tanganyika.
  Mwaka 1964 baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana iliundwa Katiba ya Muungano. Katiba ya nne ilifuatia mwaka 1965 ikiwa ni ya mpito ambapo pia ilifuta mfumo wa vyama vingi na kuvifanya vyama vya TANU na ASP kushika hatamu za uongozi.
  Katiba hiyo ya muda ilidumu hadi mwaka 1977 ambapo ilindwa Katiba ya kudumu hadi leo. Katiba hiyo imeshafanyiwa marekebisho mara 14.
  Zanzibar
  Tangu imepata uhuru wake mwaka 1963, Zanzibar imekuwa na Katiba tatu. Katiba ya kwanza ilikuwa ya uhuru ambayo ilitungwa na Waingereza.
  Hata hivyo Katiba hiyo haikudumu hata kwa mwezi mmoja, kwani mapinduzi ya January 12, 1964 yaliifuta na kuweka amri za rais (Presidential decrees).
  Licha ya kutokuwepo kwa katiba, amri za rais ziliwezesha kuwepo kwa mfumo wa mahakama na Baraza la Wawakilishi.
  Amri hizo zilidumu hadi mwaka 1979 baada ya Zanzibar kupata Katiba yake inayosemekana kuwa ya kwanza, ikifuatiwa na ya pili ya mwaka 1984 iliyoendeleza yaliyoanzishwa mwaka 1979 ikiwa pamoja na kuongeza suala la haki za binadamu.
  Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeshafanyiwa marekebisho 10 kulingana na mahitaji yaliyokuwapo.
  Mkanganyiko wa Katiba ya Zanzibar Katika muungano
  Katika marekebisho 10 yaliyofanyika katika Katiba ya Zanzibar, marekebisho makubwa yaliyotikisa ni pamoja nay a nane ambayo yaliwezesha kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoviunganisha vyama vya CCM na CUF baada ya kupigwa kwa kura ya maoni.
  Mabadiliko ya 10 ndiyo yameingiza utawala mpya wa Zanzibar ambao kimsingi unaopingana na muungano.
  Akitoa mada katika kongamano la mjadala wa Katiba linaloendeshwa kila wiki na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), mwanaharakati kutoka katika asasi ya Fordia Patience Sekinabo anaelezea marekebisho hayo na jinsi yalivyokiuka makubaliano ya Muungano.
  “Katiba ya Muungano ni Katiba mama inayoongoza mambo yote ya Muungano. Misingi ya Katiba hiyo imekiukwa na mabadiliko ya 10 ya Katiba hiyo,” anasema Sekinabo.
  Anataja baadhi ya mambo yaliyoingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar na ambayo yanakinzana na Katiba ya Muungano kuwa ni pamoja na ibara ya kwanza na ya pili zinazotambulisha nchi na mipaka yake.
  “Katiba imeingiza kifungu kinachompa rais wa Zanzibar kuigawa nchi katika wilaya na mikoa mipya kinyume na awali ambapo jukumu hilo lilikuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye kwa mujibu wa Katiba alitakiwakushauriana na rais wa Zanzibar kabla ya kufanya hivyo,” anasema Sekinabo na kuongeza,
  “Mabadiliko ya 10 yameitambua Zanzibar kama nchi yenye mipaka yake, wimbo wake wa taifa, bendera na vikosi vyake wakati Katiba ya Muungano inasema Zanzibar siyo nchi bali ni sehemu ya Tanzania,”
  Mbali na hilo, Sekinabo ameongeza kuwa suala la Rais wa Zanzibar kuteua wakuu wa mikoa na wilaya wa Zanzibar ni kinyume na Katiba ya Muungano inayompa jukumu hilo Rais wa Muungano.
  Anataja pia suala la mahakama ya rufani ambayo iko kwenye muungano lakini kwa mabadiliko hayo sasa Zanzibar ina mahakama yake ya rufani.
  “Hivyo basi, Wazanzibari watakaosindwa kuridhika na maamuzi ya mahakama kuu ya Zanzibar hawatalazimika kupeleka mashauri yao katika Mahakama ya rufani ya muungano hasa kama shauri hilo linahusu uvunjifu wa haki za binadamu. Wataishia huko huko,” anasema Sekinabo.
  Hata hivyo ameisifu Katiba hiyo kwa kuongeza idadi ya viti maalum kutoka asilimia 30 hadi 40 akisema kuwa imejali usawa wa kijinsia, lakini akaikosoa kwa kutokubaloiana na ile ya Muungano ambayo inatambua idadi hiyo kwa asilimia 30 tu.
  Ameongeza kuwa katiba hiyo imeweka wigo kwa Baraza la wawakilishi kutobadilisha Katiba hiyo kirahisi hasa kwenye sehemu zinazohusu Muungano.
  Sekinabo ameitaka Serikali kutowazyuia wananchi kujadili muungano badala yake wapewe nafasi ya kutosha ili kurekebisha kasoro zilizopo.
  “Watanzania wanautakiwa mema Muungano wetu, wanaomba serikali kuruhusu mjadala mpana ili atanzania wote washiriki kuuboresha Katiba hii mpya,” anasema.
  Hatma ya Muungano
  Kutokana na mkinzano huo, Sekinabo anasema kuwa muungano umetikiswa kwa kuwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar hayakuwa na ridhaa ya Watanzania wote.
  Anashauri Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa Katiba na kujadili kwa upana Muungano huo ili kujenga upya hatima yake.
  “Baada ya kutungwa kwa sheria ya Katiba mpya, suala la muungano limewekea mipaka kujadiliwa. Kitendo cha kuzuia mijadala inayolenga kurekebisha kasoro za muungano ndiyo chanzo cha vurugu….”
  “Serikali ina wajibu wa kutoa elimu juu ya Muungano hasa kwa kizazi hiki kipya ambacho kinaona kuwapo kwa Muungano kunawanyima fursa ya kuwa huru kiuchumi, kisiasa na uhusiano hasa kwa upande wa Zanzibar,” anasema Sekinabo.


  Chanzo Mwananchi
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Muungano is no more
   
 3. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Patience Sekinabo

  Usijichanganye Muungano ni fake tokea hapo awali,kama ulikuwa na nia safi basi Nyerere asingali waulia nchi yenu muliopigania uhuru na katiba yake yenye kulinda mambo yake ya sio ya Muungano.


  Hii leo imekuwa ujuba wenu wa kujifanya Master Mind imekuwa ndio ubovu wenu wa kuto kutumia akili,akili zenu hutumika kulinda Muungano na kuuenzi kwa nguvu zote na kutumisha na kidumu chama kitakatifu ccm.

  Sera kubwa za ccm ni kuimarisha na kudumisha matajiri na wageni huku Watanganyika wenye kujita watanzania kuwa na maisha duni ya ufukara.


  Tukiachana na Wazanzibar kuwa matajiri wakubwa Tanganyika wako wageni kutoka nje ya Tanzania wanapeta huku wenyeji kula yao tabu, hii ndio kidumu chama cha mapinduzi na ccm oyee.
  Patience Sekinabo

  Nivikao vingapi vya Bunge vilivyo kaa kujadili maswala yasio ya Muungano? hii yote ni kuchanganya mambo na kujichanganya wenyewe, Aliomchaguwa Shamsu Nahoza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Hossen Mwinyi Kuwa Waziri wa afya ni kikwete wenu kwa urafiki mwema wa Chama .


  Jee afya na mambo ya Ndani niya Muungano, Kazi ya Bilali Haribu ni nini kama sikula Bure Pencheni za Watanganyika.


  Nyiyi hujifanya muna akili lakini kumbe vichwa usaha kila ccm ikiwa kadika madaraka ndio heri kwa walaji.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Muungano ulikufa mara tu baada ya kuzalika.

  Kilochobaki ni mvungano.
   
Loading...