Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984: Kipi Hasa Kilichobadilika?

Ni Kenya walio na katiba mpya sio Zanzibar. Katiba ya Zanzibar ilitiwa kiraka juzi juzi hapa.
 
WanaJF,
Kwa wale mliofuatilia mijadala mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambayo yamezaa kitu kiitwacho "Nchi ya Zanzibar," ningependa kupitia vipengele kadhaa vya Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar 1984, Na. 9/2010 ili kujua mambo kadhaa yaliyobadilika, ikiwa ni pamoja na status ya Zanzibar kuwa "nchi kati ya nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," vilevile nitagusia mambo mengine yanayogusa Muungano wa Tanzania!

Kifungu cha 3: Kinazungumzia kuwa Zanzibar ni Nchi ambayo mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kifungu cha 4: Kinadai kwamba: Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vifungu cha 9, 10 Vinagusa Muhimili wa Mahakama: Kifungu hiki kimerekebisha Ibara ya 24 (3) na ya 25A ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na kinadai kwamba kama haki ya mtu yeyote inavunjwa au inaelekea kuvunjwa anatakiwa afungue shauri katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na kilichoongezeka katika mabadiliko haya ni kwamba shauri hilo halitafikishwa katika mahakama ya Rufani ya Tanzania. Haijulikani ni kwa nini hakuna Rufaa tena kama ilivyokuwa awali!

Kifungu cha 11 kinamtaja Rais wa Zanzibar kama "Mkuu wa Nchi ya Zanzibar," Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Kifungu cha 14 kimerekebisha Ibara ya 29 ambayo ilikuwa inalitaka BLW kuongeza muda wa uhai wake endapo Tanzania ipo kwenye vita "ikiwa Zanzibar inahusika na vita hiyo" sasa hivi maneno "ikiwa Zanzibar inahusika" yameondolewa. Hapa ilikuwa inaonesha wazi kwamba endapo ingetokea vita dhidi ya Tanzania kama ilivyokuwa vita ya Uganda, Zanzibar ingejiweka pembeni kama eti haikuhusika na vita hiyo!

Kifungu cha 19 kimefuta allegiance ya Rais wa Zanzibar kwa Muungano kwa kurekebisha Ibara ya 37 (2) ya Katiba ya Zanzibar, 1984. Kabla ya Mabadiliko Ibara hiyo ilikuwa inasema kwamba Rais wa Zanzibar anaweza kushtakiwa na BLW kwa kuwa "na mwenendo unaodhalilisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar," katika hali ya kushangaza maneno hayo yameondolewa na badala yake yamewekwa maneno "au amekuwa na mwenendo unaokidhalilisha kiti cha Rais."

Kifungu cha 37 kimeondoa ulazima wa Rais wa Zanzibar kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kugawa mikoa ya Zanzibar!

Kifungu cha 48 kinaelezea kuhusu mabadiliko ya Katiba yanayohitaji kwanza kura za maoni ambayo ni kama ifuatavyo:
- Vifungu vyote vya Sura ya Kwanza ya Katiba ambavyo vinazungumzia Zanzibar na Watu,
- Kifungu cha 9 ambacho kinazungumzia Serikali na Watu.
- Vifungu vyote vya Sura ya Tatu ambavyo vinazungumzia "Kinga ya Haki za Lazima na Uhuru wa Mtu Binafsi."
- Kifungu cha 26 ambacho kinazungumzia Ofisi ya Rais,
- Kifungu cha 28 ambacho kinazungumzia muda wa kuendelea urais,
- Vifungu vyote vya Sehemu ya Pili na Sehemu ya Tatu ya Sura ya Nne isipokuwa kifungu cha 49 na 50,
- Kifungu cha 80A na 123 vya Sura ya Kumi.
Hata hivyo BLW linaweza kuweka Azimio la Kurekebisha vifungu husika bila kupitia kura za maoni.

Kifungu cha 64 kimerekebisha Ibara ya 124 (2) ya Katiba ya Zanzibar, 1984 kwa kuongeza idadi ya vyombo vya Muungano ambavyo vinapaswa kuwa na Mamlaka Zanzibar. Kabla ya marekebisho vyombo hivyo vilikuwa hivi vifuatavyo:
- Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,
- Tume ya Kudumu ya Uchunguzi,
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano.
Chombo kilichoongezeka kwa sasa ni "Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano."

Hayo ndiyo baadhi ya Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na ambayo yanagusa Muungano kwa namna moja au nyingine! Mabadiliko hayo tumeambiwa kwamba yanalenga "kuimarisha Muungano!" Sijui kama kuna ukweli kiasi gani kuhusu hili!

Tujadili!
 
HAYO YAMEPIKA KAKA HAYO! WACHA TUZUNGUMZIE KAMPENI NA UCHAGUZI.

KAMA WALIUNGANA BASI PIA WANAYO HAKI YA KUJITENGA
:playball:
 
ivi haya mabadiliko yalishapita?so as of now is znz a country?

Ndiyo yalishapita, Karume alisaini Muswada kuwa Sheria tarehe 13/08/2010. Kwa mujibu wa Wazanzibari, Zanzibar ni Nchi na ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
HAYO YAMEPIKA KAKA HAYO! WACHA TUZUNGUMZIE KAMPENI NA UCHAGUZI.

KAMA WALIUNGANA BASI PIA WANAYO HAKI YA KUJITENGA
:playball:

Ni kweli yamepita lakini ni vizuri tukaelimishana kuwa kuna mgogoro wa kikatiba (kati ya Katiba ya JMT, 1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984) ambao unatakiwa ushughulikiwe na Mahakama ya Katiba (kama ipo anyway)!
 
Ndiyo yalishapita, Karume alisaini Muswada kuwa Sheria tarehe 13/08/2010. Kwa mujibu wa Wazanzibari, Zanzibar ni Nchi na ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

thinking aloud....Sasa Katiba ya Tanganyika (kama ipo) nayo inasema Tanganyika ni nchi?maana kama katiba ya znz inasema kuna nchi mbili, na hakuna katiba nyingine inayoitambua hiyo nchi ya pili, doesnt the provision become reduntant?
 
Hakuna kitu kama "Katiba ya Tanganyika," ni kama Wazanzibari wameamua kuiunda Tanganyika kiaina!
 
How do u reconcile kifungu cha 3 na kifungu cha 14? Kama znz ni nchi - as kifungu cha 3, basi nadhani hichi kifungu kingeendana zaidi na hiyo ibara ya 29, kuipa znz uwezo wa kujitoa kwenye hiyo vita! Naona hichi kifungu kinaonyesha dependance yake kwa Tanzania, alafu papo hapo, kifungu cha 3 kinataka independence!!
 
WanaJF,
Kwa wale mliofuatilia mijadala mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambayo yamezaa kitu kiitwacho "Nchi ya Zanzibar," ningependa kupitia vipengele kadhaa vya Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar 1984, Na. 9/2010 ili kujua mambo kadhaa yaliyobadilika, ikiwa ni pamoja na status ya Zanzibar kuwa "nchi kati ya nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," vilevile nitagusia mambo mengine yanayogusa Muungano wa Tanzania!

Kifungu cha 3: Kinazungumzia kuwa Zanzibar ni Nchi ambayo mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kifungu cha 4: Kinadai kwamba: Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vifungu cha 9, 10 Vinagusa Muhimili wa Mahakama: Kifungu hiki kimerekebisha Ibara ya 24 (3) na ya 25A ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na kinadai kwamba kama haki ya mtu yeyote inavunjwa au inaelekea kuvunjwa anatakiwa afungue shauri katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na kilichoongezeka katika mabadiliko haya ni kwamba shauri hilo halitafikishwa katika mahakama ya Rufani ya Tanzania. Haijulikani ni kwa nini hakuna Rufaa tena kama ilivyokuwa awali!

Kifungu cha 11 kinamtaja Rais wa Zanzibar kama "Mkuu wa Nchi ya Zanzibar," Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Kifungu cha 14 kimerekebisha Ibara ya 29 ambayo ilikuwa inalitaka BLW kuongeza muda wa uhai wake endapo Tanzania ipo kwenye vita "ikiwa Zanzibar inahusika na vita hiyo" sasa hivi maneno "ikiwa Zanzibar inahusika" yameondolewa. Hapa ilikuwa inaonesha wazi kwamba endapo ingetokea vita dhidi ya Tanzania kama ilivyokuwa vita ya Uganda, Zanzibar ingejiweka pembeni kama eti haikuhusika na vita hiyo!

Kifungu cha 19 kimefuta allegiance ya Rais wa Zanzibar kwa Muungano kwa kurekebisha Ibara ya 37 (2) ya Katiba ya Zanzibar, 1984. Kabla ya Mabadiliko Ibara hiyo ilikuwa inasema kwamba Rais wa Zanzibar anaweza kushtakiwa na BLW kwa kuwa "na mwenendo unaodhalilisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar," katika hali ya kushangaza maneno hayo yameondolewa na badala yake yamewekwa maneno "au amekuwa na mwenendo unaokidhalilisha kiti cha Rais."

Kifungu cha 37 kimeondoa ulazima wa Rais wa Zanzibar kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kugawa mikoa ya Zanzibar!

Kifungu cha 48 kinaelezea kuhusu mabadiliko ya Katiba yanayohitaji kwanza kura za maoni ambayo ni kama ifuatavyo:
- Vifungu vyote vya Sura ya Kwanza ya Katiba ambavyo vinazungumzia Zanzibar na Watu,
- Kifungu cha 9 ambacho kinazungumzia Serikali na Watu.
- Vifungu vyote vya Sura ya Tatu ambavyo vinazungumzia "Kinga ya Haki za Lazima na Uhuru wa Mtu Binafsi."
- Kifungu cha 26 ambacho kinazungumzia Ofisi ya Rais,
- Kifungu cha 28 ambacho kinazungumzia muda wa kuendelea urais,
- Vifungu vyote vya Sehemu ya Pili na Sehemu ya Tatu ya Sura ya Nne isipokuwa kifungu cha 49 na 50,
- Kifungu cha 80A na 123 vya Sura ya Kumi.
Hata hivyo BLW linaweza kuweka Azimio la Kurekebisha vifungu husika bila kupitia kura za maoni.

Kifungu cha 64 kimerekebisha Ibara ya 124 (2) ya Katiba ya Zanzibar, 1984 kwa kuongeza idadi ya vyombo vya Muungano ambavyo vinapaswa kuwa na Mamlaka Zanzibar. Kabla ya marekebisho vyombo hivyo vilikuwa hivi vifuatavyo:
- Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,
- Tume ya Kudumu ya Uchunguzi,
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano.
Chombo kilichoongezeka kwa sasa ni "Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano."

Hayo ndiyo baadhi ya Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na ambayo yanagusa Muungano kwa namna moja au nyingine! Mabadiliko hayo tumeambiwa kwamba yanalenga "kuimarisha Muungano!" Sijui kama kuna ukweli kiasi gani kuhusu hili!

Tujadili!

Swali la msingi ni je Zanzibar wanaweza kufanya mabadiliko ya katiba 'unilaterally'? Kwa ufahamu wangu Katiba ya Zanzibar ni sehemu ndogo ya Katiba ya JMT na kwa maana hiyo mabadiliko yoyote lazima yaridhiwe na Chombo kinachosimamia muungano!

Lakini kwa upande mwingine, Katiba ya Zanzibar Ibara ya 106(3) inasema wazi hivi:

Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya
mambo yote yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononi
mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Basi kwa utangulizo huo utaona ya kwamba sehemu ya kwanza ya Katiba ya JMT imevunjwa na 'mabadiliko' ya katiba ya zanzibar kwa kuitafsiri upya JMT.
 
How do u reconcile kifungu cha 3 na kifungu cha 14? Kama znz ni nchi - as kifungu cha 3, basi nadhani hichi kifungu kingeendana zaidi na hiyo ibara ya 29, kuipa znz uwezo wa kujitoa kwenye hiyo vita! Naona hichi kifungu kinaonyesha dependance yake kwa Tanzania, alafu papo hapo, kifungu cha 3 kinataka independence!!

Unapodai Zanzibar ijitoe kwenye vita na yenyewe ikivamiwa ijilinde yenyewe wakati haina Jeshi la Ulinzi? Suala la ulinzi na usalama ni la Muungano! Kwa hiyo itashangaza sana kama kutakuwa na "independence" hata kwenye mambo ya Muungano! Kama mambo yatakuwa ndio hivyo basi Muungano wenyewe utakuwa haupo, kama alivyodai siku moja Dkt Sengodo Mvungi wa UDSM kwamba "Muungano Ulishavunjika" baada ya kuzaliwa kwa "Nchi ya Zanzibar!"
 
Swali la msingi ni je Zanzibar wanaweza kufanya mabadiliko ya katiba 'unilaterally'? Kwa ufahamu wangu Katiba ya Zanzibar ni sehemu ndogo ya Katiba ya JMT na kwa maana hiyo mabadiliko yoyote lazima yaridhiwe na Chombo kinachosimamia muungano!

Lakini kwa upande mwingine, Katiba ya Zanzibar Ibara ya 106(3) inasema wazi hivi:
Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya
mambo yote yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononi
mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Basi kwa utangulizo huo utaona ya kwamba sehemu ya kwanza ya Katiba ya JMT imevunjwa na 'mabadiliko' ya katiba ya zanzibar kwa kuitafsiri upya JMT. Mambo ya Muungano ndio nilivyoyaorodhesha hapa chini, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ndio jambo la kwanza la Muungano!

Zanzibar wanaweza kufanya mabadiliko ya Katiba "unilaterally" lakini wasivunje Katiba ambayo imetengeneza Muungano wenyewe!
NYONGEZA YA KWANZA
(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano​
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13. Leseni ya viwanda na takwimu.
14. Elimu ya juu.
15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16. Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17. Usafiri na usafirishaji wa anga.
18. Utafiti.
19. Utafiti wa Hali ya Hewa.
20. Takwimu.
21. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22. Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo.
 
Ni kweli yamepita lakini ni vizuri tukaelimishana kuwa kuna mgogoro wa kikatiba (kati ya Katiba ya JMT, 1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984) ambao unatakiwa ushughulikiwe na Mahakama ya Katiba (kama ipo anyway)!

Buchanan kama ukiiosoma katiba ya Muungano vizuri baadhi ya mabadiliko hayo yatahusisha mabadiliko ya katiba ya Muungano na hili haliwezi kufanyika mpaka bunge la muungano likae. Pia mabadiliko hayo lazima yaidhinishwe na theluthi mbili yawabunge wa zanzibar na theluthi 2 ya wabunge wa Tanzania Bara.

Kwa hiyo mchakato bado unaendelea.

Baadhi ya mambo sidhani kama yatapita katiaka bunge la Muungano (Ingawa nina wasiwasi sana na wabunge wa CCM kama watachaguliwa kwa wingi) kwa hiyo tutarajie mgogoro mkubwa zaidi wa kimuungano.

By the way ulipata nafasi ya kuhudhuria Mjadala wa mabadiliko haya uliofanyika jana Diamond Jubilee? Ulikuwa ni njadala wa wazi na haya mambo yalijadiliwa kwa kina. Tulikubaliana kuendeleza mjadala na kuhamasisha ufufuaji wa serikali ya Tanganyika. Nitakujuza kama kuna mjadala mwingine maana tulikubaliana iwepo ili kujenga hamasa.
 
Unapodai Zanzibar ijitoe kwenye vita na yenyewe ikivamiwa ijilinde yenyewe wakati haina Jeshi la Ulinzi? Suala la ulinzi na usalama ni la Muungano! Kwa hiyo itashangaza sana kama kutakuwa na "independence" hata kwenye mambo ya Muungano! Kama mambo yatakuwa ndio hivyo basi Muungano wenyewe utakuwa haupo, kama alivyodai siku moja Dkt Sengodo Mvungi wa UDSM kwamba "Muungano Ulishavunjika" baada ya kuzaliwa kwa "Nchi ya Zanzibar!"

kwani kifungu cha zamani kilikuwa kinasemaje? si kilikuwa kinawapa huo uwezo wa kujitoa?sasa haya mabadiliko yanaonyesha kuwa sio mtiririko mmoja wa kutaka kuwa nchi. Maana kwa upande mmoja wamedai kuwa nchi, na upande mwingine wamekubali kushiriki katika vita pamoja. Umenipata hapo? Just a point of note.
 
Katika toleo la leo la Habari leo lina moja ya kichwa cha habari kama hapo juu, lkn je kitendo cha BMZ la SMZ kuamua hivyo bila kupingwa nini mwisho wa safari ya SJMTZ? Natabiri kuwa bunge la kwanza baada ya uchaguzi litakuwa gumu sn na baadhi ya wabunge wakutoka Zeenji watakuwa wakitoka bungeni kupinga uchangiaji wa wabunge wakutoka TZ bara kwani G55 kama kuna baadhi waijuao habari hiyo historia inajirudia, sikuona kuwa kama kulikuwa na umhim wa wazenji kuamua vile lkn cr itafichuka kwani usipoziba ufa ni kuanguka kwa nyumba.
Karibuni wachangiaji
 
Me nadhani imeshaanguka,
Huko ni kufunga banda wakati farasi kesha toka.:violin:
 
Kelele za SJMTZ hazitukoseshi usingizi wa karafuu huko visiwani!Katiba ni yetu wenyewe na tumeibadili wenyewe...nawashangaa ndugu zetu bado ati anaita Tanzania Bara badala ya Tanganyika!

This was suppose to be a wake up call!:smile-big:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom