Mabadiliko ni fikra yakinifu kuelekea vitendo halisia

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
The best thing about the future is that it comes one day at a time.

Ni maneno ya Abraham Lincoln nguli wa falsafa na aliyekuwa rais wa Marekani.
Tuna swali la kujiuliza ni lini future yetu itakuja kwa wakati,wakati tumewekeza kwenye ubinafsi zaidi kuliko maslahi ya umma.

Tunapozungumzia mabadiliko, hatulitazami jambo hili kwa mtazamo chanya, mabadiliko ni fikra zilizofanyiwa upembuzi yakinifu kwa wakati katika kujikita kwenye tafiti sahihi kuelekea kwenye uhalisia wa vitendo.

Dunia ilipokuwa ikitoka kwenye mifumo mbali mbali ya kimaisha kuanzia ujima na sasa ubepari, wanadamu walifanya mapinduzi ya kifikra kufikia malengo sawia. Hawakulala, walipambana na nyakati zao kupingana na mazoea ya hali walizokuwa nazo toka stone ages na sasa capitalism.

Kwa uchochezi wa fikra yakinifu mapinduzi ya viwanda huko Ulaya na Asia yalichochewa na ugunduzi wa chuma huko Meroe Egypt, japo kasi ya matumizi ya chuma ilinufaisha sana soko la Ulaya.

Lakini sisi Waafrika hususani Tanzania tumeichukulia dhana ya mabadiliko kinadharia(thesis) zaidi kuliko kivitendo tukiwaaminisha wananchi kuwa tupo kwenye kipindi cha mabadiliko, yapi!!!!

Tumejikita kwenye matumizi makubwa yasiyo na tija kwa maendeleo ya wananchi, kwa kuliingiza taifa kwenye madeni yasiyo lipika kwa kiwango cha zaidi ya tilioni 20 kwa miaka minne bila kujali uimara wa uchumi wetu.,huku tukinadi nadharia ya mabadiliko.

Tumewekeza kwenye vitu visivyo na tija kwa taifa na kuzichezea huduma zetu za kijamii kwa kuwekeza bajeti ndogo kwenye sekta ya afya, elimu na kilimo.

Matokeo yake Deni la taifa limekuwa kwa kasi kubwa sana kuliko pato la taifa, tunakopa sana kuliko kuzalisha.

Kuelekea uchumi wa viwanda China waliwekeza kwenye sekta ya kilimo kwa zaidi ya 15% ya bajeti yao, walifunga mkanda kweli kweli kuhakikisha utekelezaji wa mapinduzi hayo yana tija kwa taifa na watu wake.

Kufikia maendeleo ya leo huko China, wananchi waliumia Kama taifa zima, si leo tunazungumzia wanyonge wafunge mikanda wakubwa wanalegeza.

Kwa kutambua nguvu ya vuguvugu la mabadiliko Watanzania halikadhalika walinadi mapinduzi ya viwanda kuelekea uchumi wa kati, lakini uhalisia huo upo pamoja na kutengewa Economic zone as tumejikita kwenye maneno matupu!!!!

Tumekuwa mabingwa wa kauli mbiu kila kukicha lakini mbona hatuoni juhudi zozote za serikali kujikwamua na kauli mbiu zake, HAPA KAZI TU imekosa tija kwa kuwa imejaa siasa tupu bila economic strategies.

Tunaweka mikakati kwenye makaratasi zaidi na kuwahadaa wananchi kila tunapo elekea kwenye chaguzi, lakini hakuna upembuzi yakinifu ya mikakati hiyo.

Wakulima wanajitahidi,changamoto soko la mazao yao. Hatuna soko imara japo kwa mazao ya biashara ambayo tungekuwa na black market kwa viwanda vyetu, tungeongeza soko la ajira.

Sekta ya kilimo ambayo ndiyo sekta mama kwa mapinduzi ya viwanda imetengewa fedha chini ya 10% ya bajeti yote. Ndiyo pale tunapoambiwa thinking globally acting locally. Lakini bado tunaambiwa Magufuli for change(M4C).

Kauli mbiu ya serikali ya viwanda imepotezwa ghafla kwa kuwa nadharia imekosa vitendo. Leo sera ya viwanda inatambua cherehani 2 kuwa kiwanda.

Fikra yakinifu zinapingana na utitiri wa kodi kwa sekta nzima ya viwanda, mwekezaji wa viwanda anaweza kupata grace period ya msamaha wa kodi, lakini mkulima akarundikiwa tozo za ushuru wa mazao ilihali sekta hizi mbili zinategemeana.

Ni muhimu tunapotaka mabadiliko tujifunze kuweka vipau mbele vya nini tunakitaka. Kuingiza nchi kwenye mikopo mikubwa ya kibiashara ni kujirudisha kwenye ukoloni.

Rais wa china aliwahi kusema nchi nyingi za Kiafrika zinataka tuzinunue, tumeanza na Zambia na zingine zinafuata, tuna washabikia waliokuwa wakominist na wajamaa zaidi yetu, ambao kwa sera zile zile za kijamaa leo tunaomba mikopo kwao. Bahati mbaya sana mikopo yenyewe ya kibiashara. Wanaoumia wananchi kutokana na kodi zao kukosa tija ya kujikwamua katika ustawi wa Taifa.

Bahati mbaya sana maendeleo yanaendana na demokrasia, kwa kuwa tumeshindwa kuisimamia demokrasia ipasavyo kwa kutanguliza utamu wa madaraka, tumejikuta tunawekeza zaidi kuuwa demokrasia na matokeo yake tunakwamisha maendeleo.

Wahisani wanapo tupatia misaada wanatuwekea masharti ya kusimamia misingi ya haki, kukuza demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, kwa kuwa kauli mbiu zetu haziendani na dhamira zetu tumekuwa kama mwanamke malaya, kila bwana tunamtaka, matokeo yake tunaumiza taifa kwa mikopo siyo na tija.

Tumekuwa tukiwabeza jirani zetu Kenya, lakini wao wanapiga hatua mbele kila kukicha wakitazama maendeleo ya Wakenya, ndiyo maana wameweza kuzindua kampeni ya maridhiano kwa jina la BBI,sisi tunaendeleza siasa za chuki, ukanda, ukabila na ubinafsi.

Tusipo kubali fikra yakinifu, tutaendelea kuendeleza ubinafsi wa kimadaraka kwa kupeleka maendeleo sehemu tunazo ungwa mkono tu kutokana na itikadi zetu za kisiasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom