Mabadiliko nchini yataletwa na mambo mawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko nchini yataletwa na mambo mawili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Sep 8, 2012.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mabadiliko ya kweli yananukia, na kweli yapo. Mabadiliko ambayo yataubadilisha mfumo wa uongozi wa sasa na kuweka mfumo mpya kabisa. Ndipo ninapoona dhahiri kabisa kuwa kuna nguvu mbili muhimu zenye kuweza kufanya hayo. Moja ni M4C na la pili ni uislam.

  M4C imekuwa na nguvu ambayo kwa sasa haielezeki. Pale watawala wanapodhani kuwa hii nguvu itayumba ndipo nguvu zake zinapoongezeka. Tangu uchaguzi mkuu uliopita hii nguvu imekuwa kazini hadi wakati huu tukiwa tunaelekea uchaguzi mwingine. Ni harakati ambazo zinawafungua watanzania wengi akili na ufahamu wa hali halisi; kwamba chama kilichopo madarakani kwa sasa kina porojo tu, na kweli kina porojo, tena na vitisho juu. Watanzania awali walikuwa hawana mbadala wa mfumo lakini sasa ni wazi kuwa mbadala huo umepatikana na ni suala la muda na maamuzi tu ili kuung'oa mfumo uliopo na kuweka mwingine, chini ya chama kingine. Hilo liko wazi.

  Jambo la pili ni uislam. Waislam popote duniani wamekuwa ni chachu ya mabadiliko na vuguvugu la mifumo mipya ya kiutawala. Hili lipo wazi hasa tukitazama harakati za Arab Spring. Wameweza kung'oa mifumo mingi kandamizi katika mataifa yao na hatimaye wakawa na punje za ahueni.

  Tunapowatazama waislam wa nchi hii, binafsi sioni tofauti na ninayoyaona huko kwingine. Tofauti kubwa ni kuwa hapa kwetu tuna imani mchanganyiko zaidi kuliko wenzetu.

  Jana wakati napata hizi taarifa za waislam kuungana na kuandamana, tena bila umma wa watanzania kujua kabla kuwa haya yatatokea, nilijiwa na wazo kuwa hawa NDUGU zetu wanaweza kuwa ni chachu ya mabadiliko.

  Sasa basi, ili kuona kuwa hili linawezekana, waislam wana madai yao ya msingi kabisa. Moja kuu ni Mahakama ya Qadhi. Hili halina athari yoyote katika secular state kama Tanzania. M4C ichukue hii ajenda na itoe ahadi kwa waislam kuwa mahakama ya kadhi ni halali yao pale cdm itakaposhika Dola. Kwa mwendo huu hizi nguvu mbili zikiungana mabadiliko yapo. Pia muungano huu utaondoa dhana ya udini iliyopandikizwa na mahasimu wa kisiasa wa M4C. Hakika hii itakuwa ni jambo jema sana kwani pia itapunguza msuguano wa kiimani katika Taifa hili Teule. Na wote tuseme 'Na iwe hivyo'.
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Na iwe hivyo!

  However kwa upande wa pili wa coin,hayo mambo mawili ili mabadiliko yaje,yanatakiwe yasikinzane,ama kwa maana nyingine,yasiingiliane kwa kupingana.
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na ndio maana yangu hasa. Pasiwe na mikingamo baina ya pande hizi mbili
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Raia Fulani bandiko lako limeenda shule ! Subiria wale great thinker waje kuharibu
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ndungu zangu waislam, I know their strength kwenye jambo wanaloliamini, tatizo ni mimi. Siwaamini sana maana wanabadilika badilika sana. Kaupepo tu, kanawabeba wote!
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Hapo pa kupendekeza CHADEMA ibebe wimbo wa mahakama ya kadhi ni kutaka CHADEMA ibebe mbegu ya kujiangamiza yenyewe.
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Tukumbuke ukimruhusu ngamia aingize kichwa kwenye kibanda,basi atang'ang'ania aingize mwili wote.
  Ndio maana tulio wengi tunapinga mahkama ya kadhi kuendeshwa na serikali kwani huu ni mwanzo wa kuipeleka nchi yetu kuwa ya kiislamu,ambapo kwa mtazamo wa wengine wetu ni sawa na kumkabidhi shetani utawala wa nchi.
  Jambo hili halikubaliki hata kidogo.
   
 8. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  A Change to What.. ?
  Different Cast Same Script....

  Tunachohitaji ni Change za mfumo, tunachohitaji ni uwajibikaji, tunachohitaji ni miundombinu bora, na ajira kwa vijana (iwe viwanda n.k.)

  Hizi labels za sisi na wao au kutaka kuingiza siasa kwenye mambo muhimu ya maisha its creating more division kuliko umoja.., just one of your point nikiichukua hii mahakama ya kadhi hivi ni wapi imekatazwa ?, tafadhali epuka kuchanganya mambo ya imani, au mambo yanayoweza kutenga watu na kuingiza siasa kwenye mambo ya imani mwisho wake sio mwema (its a pandora's box)

  By the way don't get me wrong ninaamini kwamba nchi bila upinzani wa nguvu haiwezi kwenda mbele (ndio maana naamini fika kwamba CCM ni janga la taifa.., sababu ina nguvu sana kwahio inafanya inachotaka hivyo kifo chake na kuwa na upinzani wa kweli ndio njia pekee bora).., CHADEMA au Chama kimoja pekee hakiwezi kuwa a magic pill (cause power corrupts nao wanaweza kufanya madudu yale yale.., ila pakiwa na vyama vyenye nguvu sawa na kupingana kila anayechemka atakuwa anajua kwamba next term anapigwa chini.., hapo tu ndio kutakuwa kuna ukombozi wa kweli
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Yawezekana serikali ikatoa fungu fulani na wao wenyewe kupitia vyanzo vyao vya nje wakajazia kilichobaki. Hili ni suala la kimjadala zaidi kabla ya kukubaliana. Kwamba serikali itakayoingia madarakani itahusikaje na mahakama hiyo pamoja na mipaka yake. Hayo yakizungumzika, basi laweza kuwezekana. Pia yawezekana isiwe ni mahakama ya kadhi bali ahadi zingine muhimu pamoja na fursa ambazo waislam wanahisi kuzikosa au kunyimwa. Mfano mfumo bora wa elimu
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mahakama haijakatazwa bali haijapata sapoti wanayohitaji. Mara nyingi kuifikia Dola huambatana na taratibu kadhaa ikiwa ni pamoja na ahadi unazopenda na usizopenda. Bora lipi; kuruhusu hali iliyopo kuendelea ikiwa ni pamoja na wizi wa kutupwa na ubakaji wa rasilimali uliokithiri au kuthubutu kutoa fungu toka mfuko wa serikali na kuwapatia waislam kuendesha shughuli zao? Sina tatizo na wakristo kwani mfumo wa Haki uliopo kwao si tatizo. Suala ni kupata sapoti ya kuuondoa mfumo uliopo, ila sapoti iwe na faida pande zote
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nakubaliana na wewe sana, ila hapo kwenye red naona hiyo lugha sio "rafiki!"
   
 12. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Hiyo tu inatosha. Lazima tuelewane kuhusu aina ya madiliko tunayotaka ili tujue ni njia ipi na ni "maajenti" gani wa mabadiliko ndio sahihi kutufikisha huko.
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama unaishi Tanzania utajua tu ni mabadiliko gani. Pia mfumo wa uongozi wa Taifa hili umezungumziwa vya kutosha hapo juu na kwenye mada zingine. Lakini awali ya yote ni kuking'oa chama kilichoko madarakani kwanza
   
 14. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu waliosema nchi haina dini wala isijihusishe na mambo ya imani hawakuwa wajinga.., hivi unataka kuniambia this is the only way ya kuiondoa CCM ?,

  Kwa kupitia mambo ya imani (ambayo yatagawa watu) ni sawa na kulika majivu na kukanyaga moto.., na serikali / chama ambacho kitatumia imani za watu kuwahadaa ili kupata wanachotaka mwisho wa siku wataombwa what they can't provide.

  What happens hii CCM ambayo bado imeiba rasilimali zetu nyingi na ina nguvu za kutosha pamoja na a lot of source of incomes wakija baada ya miaka mitano na wao wakasema wanatoa hiki au kile kwa kundi fulani la dini au kabila fulani (then what..?)

  Mkuu dawa ni kwa njia ya wananchi wenyewe kuelewa kwamba (Nguvu ya CCM na Monopoly yao) ndio mwiba wa upinzani wa kweli hence maendeleo ya kweli., sio kuona kwamba sababu hawa wanatuonea sisi wa Imani hii (Hindu, wapagani au wakristo) basi tuchague wale ambao wanaweza wakakataza kula nyama ya ng'ombe sababu imani yetu hairuhusu...
   
 15. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pengine nikubaliane na Mtoa hoja kwa 48% tu.
  Ikumbukwe kuwa kuna mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya (Marejeo ya katiba) Umakini wa hali ya juu unahitajika kwa vyama vya siasa katika kuandaa Ilani za vyama vyao kuelekea uchaguzi mkuu hapo 2015. Kama ni umakini wa kutengeneza ilani za vyama vya siasa hapo ndipo utakapoonekana. Ni kipimo kikubwa sana kwa vyama makini vya siasa. Ukizungumzia issue ya Mahakama ya Qadhi ina mabawa mawili. Bawa la kwanza lipo ndani ya mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya na bawa la pili lipo mikononi mwa wanasiasa. Hapo kama kuna chama kitakachoona kuwa ni issue kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla basi itabidi lobbying isubiri mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya upite ndipo kulingana na maamuzi ya kura ya maoni ndipo wanaweza kujua lobbying iweje.
  Thats all
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nilitaka kuchangia lakini kutokana na haya maneno imenibidi nibakie kuwa msomaji wa hii thread..:tape2:
   
 17. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  "In matters of conscience, the law of the majority has no place." - Mahatma Gandhi

  Mkuu what is wrong na serikali kutokujihusiha na mambo ya imani ?, hivi kuna ubaya gani kama mtu unataka kutambikia au una-issue zako za imani yako kwanini usifanye wewe peke yako na watu wa imani yako kuliko kuhusisha serikali inajumuisha watu wenye imani tofauti ? (nadhani nikienda hapo deep takuwa natoka kwenye issue at hand..)

  Issue at hand hapa mtoa mada anataka kutuambia kwamba ili kikundi fulani kiingie madarakani kitumie / kiweke kwenye agenda yao jambo ambalo litavuta watu wa imani fulani ili kusaidia kuingia kwao madarakani (nadhani this is a wrong way to go.., cha maana kabla ya yote ni kuangalia kuingiza au kutokuingiza jambo fulani kama litaleta tija kwa taifa) na personally nadhani kufanya hivi kutaongeza nyufa zaidi kwa watanzania (its just a price too high to pay) wakati kuna njia za kutosha za kuleta mabadiliko bila kugombanisha kina Hawa na kina James kuishi kama ndugu na kina Patel na Sanjay
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  dangerous route..inanikumbusha video game mojaniliwahi cheza, mwanzo wa game unakuwa na wengine,ila somewhere in the game wanageuka na kuanza kukushambulia.Route ya dini na mageuzi itakwenda hivyo hivyo, baada ya kummaliza common enemy.Mkibaki wenyewe ndio mtagundua kuwa nanyi ni tofauti.Then kwa walio wajanja watajikutwa wamfaidika zaidi njiani na hivyo kuwa na nguvu zaidi kiasi cha kuweza anzisha vurugu kubwa.

  Hapa hata kiongozi wa Dini akiingia katik mchakato inabidi asijitambulishe hivyo katik uwanja wa mapambano.Ila baada ya hapo anweza endelea mcha Mungu wake
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa upande wa Kenya mahakama ya kadhi ipo kwenye katiba na wala hatusikii kelele zozote za maana. Iweje hapa kwetu lishindikane hili? Serikali ya ccm imeruhusu mahakama hiyo lakini kwa gharama za waislam wenyewe. Si vibaya kama cdm nao wakasema kuwa nao wanaikubali na kisha wakaenda some extra mile kuahidi kutoa ruzuku kwa baadhi ya shughuli za mahakama hiyo. Kama alivyosema Deus, ni suala la lobbying zaidi. Kama unatafuta kuungwa mkono na jamii fulani ambayo imelishwa sumu ya uongo juu yako, dawa ni kuwahusisha kwenye majadiliano hao ambao wanaonekana kuweza kuongeza nguvu ya mabadiliko, japo kwa gharama kiasi. Lakini katika hayo si lazima pia kuchukulia hilo kama ajenda kama pataonekana kutofikiwa muafaka. Basi nguvu zitaelekezwa katika M4C
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  dangerous route..inanikumbusha video game mojaniliwahi cheza, mwanzo wa game unakuwa na wengine,ila somewhere in the game wanageuka na kuanza kukushambulia.Route ya dini na mageuzi itakwenda hivyo hivyo, baada ya kummaliza common enemy.Mkibaki wenyewe ndio mtagundua kuwa nanyi ni tofauti.Then kwa walio wajanja watajikutwa wamfaidika zaidi njiani na hivyo kuwa na nguvu zaidi kiasi cha kuweza anzisha vurugu kubwa.

  Hapa hata kiongozi wa Dini akiingia katik mchakato inabidi asijitambulishe hivyo katik uwanja wa mapambano.Ila baada ya hapo anweza endelea mcha Mungu wake
   
Loading...