Mabadiliko mapya ya Sheria 2022: Bila upelelezi kukamilika hakuna kupeleka kesi mahakamani

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
MABADILIKO MAPYA YA SHERIA, BILA UPELELEZI KUKAMILIKA HAKUNA KUPELEKA KESI MAHAKAMANI.

Na Bashir Yakub. WAKILI.
+255 714 047 241

Mabadiliko muhimu ya Sheria yanakuja kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria No. 7 /2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinaongezewa kifungu kipya ambacho kitajulikana kama Kifungu cha 131A.

Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali(DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kupeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika.

Maana yake yale mambo ya nenda rudi kila siku upelelezi haujakamilika yamefika mwisho.

Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi hadi miaka sita huku kila siku akiambiwa upelelezi haujakamilika.

Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani. Akikamilisha upelelezi ndio alete kesi yako mahakamani.
Hivyo ndivyo kinavyosema Kifungu kipya cha 131A( 1 ).

Pengine mtu atawaza ama atasema, kama wamekatazwa kukupeleka mahakamani bila upelelezi kukamilika sasa si watakuweka tu huko polisi selo mda wanaotaka mpaka upelelezi ukamilike ndo wakupeleke mahakamani.

Jibu ni hapana , Mabadiliko hayohayo kifungu cha 131A(2) kinaongeza kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi hata hapo polisi aliposhikiliwa asikae, bali apewe dhamana wakati polisi ama mamlaka inayokushikilia ikiendelea kukamilisha upelelezi.

Maana yake bila upelelezi kukamilika hautakuwa polisi selo wala mahakamani. Na kwa maana hiyo hiyo ikiwa upelelezi utakamilika na hivyo kufikishwa mahakamani basi kesi yako itaanza kusikilizwa moja kwa moja bila kuchelewa. Sio tena imeahirishwa mpaka sijui lini,mara sijui upelelezi unaendelea, mara sijui nini, hakuna tena hayo.

Hata hivyo katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa Makosa ya Kubaka, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana, kosa la kuhatarisha usalama wa taifa , usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa na mahakama kuu tu.

Maana yake nini kama unataka kuelewa vizur ni hivi, Mosi ni kwamba kama hujatenda kosa lolote kati ya niliyotaja hapa juu, basi hutakiwi kufikishwa mahakama ya Mwanzo, au ya Wilaya, au ya Hakimu Mkazi(wengine mnaiita Mahakama ya Mkoa) bila upelelezi kukamilika, ama kukalishwa kituo chochote cha polisi eti kwasababu upelelezi unaendelea. Kwa urahisi tu hili ulielewe hivyo.

Pili, kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi hiyo haihusiki na hiki nilichoeleza humu, hata hivyo huko nako zile taratibu za kawaida za dhamana zitaendelea kama kawaida kwa wanaostahili.

Zaidi, Mabadiliko hayohayo kifungu cha 131A(3) kinatoa msisitizo kwa kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kuwa, Kwa makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama basi angehukumiwa kulipa ya faini ya pesa za Tanzania zisizozidi shilingi Laki Mbili basi mtu huyo akiri kosa hapo hapo polisi, alipe hiyo faini hapo kituoni, na mambo yaishie hapo.

Maana yake ni kuwa. kwa makosa ya aina hiyo, ambayo hata unegefikishwa mahakamani ukapatikana na hatia bado ungeadhibiwa kwa kulipa faini kiasi kisichozidi Laki Mbili za Kitanzania basi yaishie polisi.

Isipokuwa kwanza ukiri kosa kwa maandishi hapohapo polisi, kisha ulipe fedha hizo,na kisha uachiliwe huru uendelee na shughuli zako.

Lengo ni kuwa hakuna haja ya kupeleka kila kitu mahakamani. Makosa mengine madogomadogo yaweza kuishia hukohuko tukaipunguzia mzigo mahakama.

Hata hivyo hapo kwenye kulipa faini kuna maelekezo kidogo. Usimpe mkononi hiyo hela ya faini askari. Mwambie akupe nambari ya malipo(control number) ama akaunti ya serikali ulipe huko moja kwa moja. Yeye mpe tu nakala ya risiti. Nadhani mnajua hapa namaanisha nini msitake niseme zaidi.

Ni hayo tu, pia kuna mabadiliko ya katazo la kumkamata mtu baada ya kufutiwa mashitaka.

Mnajua hii tabia unafutiwa mashtaka ndani ya mahakama ukitoka nje unakamatwa tena. Hilo nalo limekatazwa lakini nitalieleza kwa kina katika Makala nyingine.
 
Nakumbuka wimbo flan hiv, mashairi yake yapo hivi

Ndio baasi... Ndio basi tena
Ndio basi ndio basi... Ndio basi tena
Mambo ya kutekana tekana... Ndio basi tena
Kesi za kubambikiana... Ndio basi tena
 
Ni mabadiliko yenye kupunguza unyanuasaji wa polisi.

Lakini wanawezakutumia makosa hayo hayo tajwa hapo juu.
Kuendelea kuwanyanyasa watu.

Ukiwasikiliza askari wengi hutishia watukuwafungulia shitaka la
Uhujumu uchumi kwa kuwa halina dhamana

Pengine sasa watahamia kwenye mashitaka mengine hatari yaliyopo
 
Maana yake yale mambo ya nenda rudi kila siku upelelezi haujakamilika yamefika mwisho.

Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi hadi miaka sita huku kila siku akiambiwa upelelezi haujakamilika.
 
Umeandika vitu vingi utazani Vina maana; Hivi Hakuna sheria ambayo inakinzana na kina covid-19 Kuwa hungeni?

Sheria hazina ladha au utamu maana zinakanyagwa! kaporwa mtu hela Mtwara, kauwawa; Police naye kauwawa, Tabu Tabu tupu!

Kesi ya Mbowe? Sheria inazingatiwa? Hakuna la maana hata sijui wanazitungia nini! Dhuluma imeshamiri Sana!
 
kosa la kuhatarisha usalama wa taifa. mizizi yake mingi kwa kuwabana wapigania demokrasia.
 
Naona hiki kifungu kilichoongezwa ndio cha maana zaidi, sasa watakosa watu wa kuwashikilia kwa tuhuma za ugaidi au utakatishaji fedha.

Napendekeza na wale walioko magerezani kwa tuhuma za ugaidi na nyinginezo ambao kesi zao hazijaanza kusikilizwa wote waachiwe huru.
 
MABADILIKO MAPYA YA SHERIA, BILA UPELELEZI KUKAMILIKA HAKUNA KUPELEKA KESI MAHAKAMANI.

Na Bashir Yakub. WAKILI.
+255 714 047 241

Mabadiliko muhimu ya Sheria yanakuja kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria No. 7 /2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinaongezewa kifungu kipya ambacho kitajulikana kama Kifungu cha 131A.

Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali(DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kupeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika.

Maana yake yale mambo ya nenda rudi kila siku upelelezi haujakamilika yamefika mwisho.

Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi hadi miaka sita huku kila siku akiambiwa upelelezi haujakamilika.

Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani. Akikamilisha upelelezi ndio alete kesi yako mahakamani.
Hivyo ndivyo kinavyosema Kifungu kipya cha 131A( 1 ).

Pengine mtu atawaza ama atasema, kama wamekatazwa kukupeleka mahakamani bila upelelezi kukamilika sasa si watakuweka tu huko polisi selo mda wanaotaka mpaka upelelezi ukamilike ndo wakupeleke mahakamani.

Jibu ni hapana , Mabadiliko hayohayo kifungu cha 131A(2) kinaongeza kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi hata hapo polisi aliposhikiliwa asikae, bali apewe dhamana wakati polisi ama mamlaka inayokushikilia ikiendelea kukamilisha upelelezi.

Maana yake bila upelelezi kukamilika hautakuwa polisi selo wala mahakamani. Na kwa maana hiyo hiyo ikiwa upelelezi utakamilika na hivyo kufikishwa mahakamani basi kesi yako itaanza kusikilizwa moja kwa moja bila kuchelewa. Sio tena imeahirishwa mpaka sijui lini,mara sijui upelelezi unaendelea, mara sijui nini, hakuna tena hayo.

Hata hivyo katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa Makosa ya Kubaka, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana, kosa la kuhatarisha usalama wa taifa , usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa na mahakama kuu tu.

Maana yake nini kama unataka kuelewa vizur ni hivi, Mosi ni kwamba kama hujatenda kosa lolote kati ya niliyotaja hapa juu, basi hutakiwi kufikishwa mahakama ya Mwanzo, au ya Wilaya, au ya Hakimu Mkazi(wengine mnaiita Mahakama ya Mkoa) bila upelelezi kukamilika, ama kukalishwa kituo chochote cha polisi eti kwasababu upelelezi unaendelea. Kwa urahisi tu hili ulielewe hivyo.

Pili, kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi hiyo haihusiki na hiki nilichoeleza humu, hata hivyo huko nako zile taratibu za kawaida za dhamana zitaendelea kama kawaida kwa wanaostahili.

Zaidi, Mabadiliko hayohayo kifungu cha 131A(3) kinatoa msisitizo kwa kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kuwa, Kwa makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama basi angehukumiwa kulipa ya faini ya pesa za Tanzania zisizozidi shilingi Laki Mbili basi mtu huyo akiri kosa hapo hapo polisi, alipe hiyo faini hapo kituoni, na mambo yaishie hapo.

Maana yake ni kuwa. kwa makosa ya aina hiyo, ambayo hata unegefikishwa mahakamani ukapatikana na hatia bado ungeadhibiwa kwa kulipa faini kiasi kisichozidi Laki Mbili za Kitanzania basi yaishie polisi.

Isipokuwa kwanza ukiri kosa kwa maandishi hapohapo polisi, kisha ulipe fedha hizo,na kisha uachiliwe huru uendelee na shughuli zako.

Lengo ni kuwa hakuna haja ya kupeleka kila kitu mahakamani. Makosa mengine madogomadogo yaweza kuishia hukohuko tukaipunguzia mzigo mahakama.

Hata hivyo hapo kwenye kulipa faini kuna maelekezo kidogo. Usimpe mkononi hiyo hela ya faini askari. Mwambie akupe nambari ya malipo(control number) ama akaunti ya serikali ulipe huko moja kwa moja. Yeye mpe tu nakala ya risiti. Nadhani mnajua hapa namaanisha nini msitake niseme zaidi.

Ni hayo tu, pia kuna mabadiliko ya katazo la kumkamata mtu baada ya kufutiwa mashitaka.

Mnajua hii tabia unafutiwa mashtaka ndani ya mahakama ukitoka nje unakamatwa tena. Hilo nalo limekatazwa lakini nitalieleza kwa kina katika Makala nyingine.
kwa tz hayo yataendelea ooh atahatarsha usalama wake
 
Hii itachochea uhalifu, yaani dereva ahatarishe maisha afu akalipe faini tuu basi? Vibaka nk?
 
Naona hiki kifungu kilichoongezwa ndio cha maana zaidi, sasa watakosa watu wa kuwashikilia kwa tuhuma za ugaidi au utakatishaji fedha.

Napendekeza na wale walioko magerezani kwa tuhuma za ugaidi na nyinginezo ambao kesi zao hazijaanza kusikilizwa wote waachiwe huru.
Hayo ni makosa makubwa boss,selo kama kawaida yaani ni jinai hizo.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom