Mabadiliko makubwa yashuhudiwa kwa wanavijiji wa Xinjiang walioondolewa kwenye umasikini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
6.jpg

Nimeishi nchini China kwa miaka 13 sasa. China ni nyumbani kwetu kwa pili na ni nchi ambayo naipenda sana, nchi ambayo naishi, nafanya kazi na hata kumsomesha mwanangu. Kusema kweli najihisi mwenye bahati kuwepo hapa na kushuhudia mabadiliko ya kiwango kikubwa cha maendeleo ya kasi ya Wachina.

Mwaka jana China ilitangaza kuondoa umasikini uliokithiri katika kaunti zote tisa zilizobaki. Kwa kijuujuu unaweza kuona kama ni jambo la masihara lakini hii ni hali halisi kabisa.

Katika safari yetu ya Xinjiang tukiwa bado tupo kwenye wilaya ya Yili, wenyeji wetu walitupeleka hadi kwenye kijiji cha Uzumbrak, kwenye kijiji hiki tulipata fursa ya kushuhudia yale yote ambayo nilikuwa nikiyasikia au hata kuyatangaza mimi mwenyewe redioni. Nasema hivi kwasababu sisi wakazi wa miji mikubwa iliyoendelea kama vile Beijing, mara nyingi huwa tunajua kijuujuu tu na sio kwa undani kuhusu kile kinachoendelea kwenye miji midogo au hata kwenye vijiji. Hivyo kutembelea maeneo kama hayo kunasaidia kupanua upeo pamoja na kujua kwa undani kabisa kinachoendelea katika kila kona nchini China.

Nilipofika kwenye kijiji cha Uzumbrak kusema kweli nilistaajabu sana, kwanza kabisa kujua kwamba ndani ya kijiji hiki wakazi wanatoka makabila sita yakiwemo Wakazakh, Wahan, Wauygur, Wakirgiz na Wahui, na wote wanaishi kwa umoja na mshikamano. Lakini zaidi ni kabila la Wakazakh ambalo ni la wafugaji, waliokuwa wakihamahama ili kutafuta malisho ya mifugo yao.

Serikali katika azma yake ya kupambana na umasikini na kuhakikisha wananchi wote wanaondolewa kwenye dimbwi la umasikini, mbali na kuwapelekea maendeleo pia iliamua kuwajengea nyumba kwenye maeneo mazuri yenye miundo mbinu bora na huduma za kufaa. Ikumbukwe kuwa wafugaji kawaida wanategemea mifugo tu kuendesha maisha yao, na hali ya maisha yao ilikuwa si nzuri, na hawakuwa na utulivu wala kituo maalumu cha kuishi.

Baada ya kuhamia na kukaa katika kijiji kipya mwaka 2012, maisha ya wafugaji hawa yakageuka kabisa. Bahati nzuri nilifika hadi kwenye nyumba ya mmoja wa aliyekuwa mfugaji Bibi Nur’ipa

Kwa maelezo yake Bi. Nur’ipa anasema katika familia yao wako watu wanne na hivi sasa yeye anafanya kazi ya kutengeneza vyakula vya aina mbalimbali, ambapo mume wake anafanya kazi katika kiwanda kinachoshughulikia kutengeneza vifaa vya umwagiliaji, watoto wake wawili mmoja anasoma darasa la tano na mwingine baada ya kumaliza masomo amekuwa mpishi mzuri tu.

Bi. Nur’ipa anasema sasa maisha yao yameboreka kwani zamani familia yao ilikuwa na ng’ombe wawili na shamba la ekari 1.3. Hata hivyo anasema mahali walipokuwa wakiishi zamani, kulikuwa na hali mbaya ambapo mara kwa mara walishuhudia maafa ya maporomoko ya ardhi na hawakuwa na umeme wa uhakika, maji na barabara haikuwa nzuri. Ndio maana familia yake pamoja na wenzake wa kijiji kizima waliitikia wito wa serikali wa kuwahamishia katika kijiji wanachokaa hivi sasa. Katika kijiji kipya, wanapewa shamba la ekari 1.3. Kwa gharama za ujenzi wa nyumba mpya kiasi cha Yuan laki 1.6 sawa na dola za kimarekani elfu 25, theluthi mbili zinatokana na msaada wa serikali. Mwaka 2014 ujenzi wa nyumba ulikamilika na familia yake ilihamia katika nyumba nzuri zenye huduma zote kama vile umeme na maji, sasa anaishi maisha ya furaha na familia yake, pia wamepata fursa ya matibabu mazuri hospitalini pamoja na ajira.

Katika miaka miwili iliyopita, kutokana na ukaribu wa kaunti ya Chabuchar na mji wa Yining, kijiji cha Uzumbrak kimeweza kukuza utalii na miradi yenye ubora wa juu, huku vijiji vya Wakazakh vikiwa ndio kama mhimili. Vijiji hivi vimeanzisha mgahawa wa familia za wakulima, mgahawa wa wafugaji na nyumba ya wageni yenye sifa maalumu za wenyeji.

Na wakati nilipozunguka kwenye kijiji hicho nikashuhudia kwa macho yangu maisha mazuri ya wanakijiji ambao wote wamejengewa nyumba na kuzipaka rangi za buluu au nyeupe, rangi za kutani zinaonesha utamaduni wa jadi wa wenyeji pamoja na barabara safi kabisa.

Siku hizi maisha yamekuwa tofauti kabisa, kwani Bi. Nur’ipa anasema sasa ameamua hata kujifunza kuendesha gari, na siku hii ambayo tumemtembelea nyumbani kwake ametueleza kuwa alichukua mapumziko ili kuwalaki wageni wake pamoja na kupata mafunzo ya kuendesha gari. Bahati nzuri mtihani wa kwanza wa kuendesha gari tayari ameshafaulu na akimaliza mitihani yote na kukabidhiwa leseni yake, yeye atakuwa mtu wa kwanza katika familia yake ambaye anajua kuendesha gari, ambapo anapanga kununua gari baada ya kuhitimu mafunzo yake ya udereva.

Huo ni mfano mmoja tu kuna familia nyingi kama ya Bi. Nur’ipa, ambazo hivi sasa zinaishi maisha ya raha mustarehe baada ya kunasuliwa kwenye umasikini, wahenga wanasema “Mcheza kwao hutuzwa” hivyo juhudi za serikali kuu na serikali za miji zinapaswa kuthaminiwa, kuenziwa na hata kusifiwa.
 
Mkuu,

Hii thread umeandika ww au umeitoa sehem? Kama ni ww ningependa kujua hyo radio nijifunze mambo ya hko.

Na kama ni ww pia naomba mchanganuo wa hii sehem

"Katika kijiji kipya, wanapewa shamba la ekari 1.3. Kwa gharama za ujenzi wa nyumba mpya kiasi cha Yuan laki 1.6 sawa na dola za kimarekani elfu 25, theluthi mbili zinatokana na msaada wa serikali."

Nataka kujua hyo theluthi 1/ ~8k usd inayotolewa na hyu mwnanch maskini inatoka wapi? Asiyekuwa nayo hajengewi?

Gharama za matumizi ya kila siku za umeme, maji, vitu kama bima etc, navyo vinatoka mfuko huo huo wa 2/3 ya inachochangia serikali au? Point yangu nataka kujua strategy Wanazotumia wenzetu kukabiliana na hizi changamoto.
 
Wewe dada! Mchina mrefu ni ming yao tu huyo kwenye picha umemtoa wapi? Halafu ungeweka picha za nje tuone hicho kijiji.
 
Back
Top Bottom